Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Humphrey Polepole akizungumza kwa njia ya Mtandao usiku wa Agosti 13 amesema; "Mama Samia Mungu atamgusa, nchi hii ni kubwa zaidi kuliko yeye na kwamba dhamana ilimtaka yeye ndiyo awe Rais wa nchi yetu baada ya aliyekuwa Rais kutwaliwa na Mungu. Kwahiyo ana Haki ya kulinda maslai mapana ya nchi ya Tanzania, asijitazame yeye kwanza."
"Tunakwenda kwenye Uchaguzi katika mazingira ambayo nchi haiko moja tumegawika wengine hawafanyi Siasa kwasababu wamefungwa mikono, unapataje amani unakwenda kwenye uchaguzi mpinzani wa kweli yupo jela? Haiwezekani."