Polepole: Siamini Tanzania tuna tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana

Mueleweni muktadha wake

Hapo anamaanisha kuwa kwa Tanzania na Afrika kuna changamoto nyingi sana ambazo ndio zilitakiwa zilete ajira

Yaani nchi kama Norway au Canada huko ambako ndio wasio na ajira wanazamia, ndio kulitakiwa kuwe na tatizo la ajira, sababu changamoto zote almost zipo covered, hakuna tatizo la madaktari, madarasa, umeme, hospitali wala barabara, sasa wasomi watapata vipi ajira?

Ila Tanzania kuna tatizo la madaktari, walimu, maji, umeme, usafiri, zahanati n.k lakini madaktari, mainjinia, walimu, madereva n.k hawana ajira..!

Yaani kwa maneno mengine ni kuwa Tanzania hatuna ukosefu wa ajira, bali ukosefu wa akili..
Taarifa kwa Polepole: Unemployment rate ya Tanzania ni 10.3%. Source: Africa :: Tanzania — The World Factbook - Central Intelligence Agency. Aache kuropoka. Anaaibisha chama chetu cha CCM.
 
Ccm hawa akili yao ndio hii
Kwa hiyo wewe na hao ndio wenye akili za siasa za ujasiriamali, au vipi?

Mwenye akili timamu atakuwa amegundua agenda za kiongozi mkuu wa chama kile. Kama wewe bado, jifikirishe zaidi.
 
Kwa hiyo wewe na hao ndio wenye akili za siasa za ujasiriamali, au vipi?

Mwenye akili timamu atakuwa amegundua agenda za kiongozi mkuu wa chama kile. Kama wewe bado, jifikirishe zaidi.
Agenda yenu ni viwanda... viko wapi?
 
Mueleweni muktadha wake

Hapo anamaanisha kuwa kwa Tanzania na Afrika kuna changamoto nyingi sana ambazo ndio zilitakiwa zilete ajira

Yaani nchi kama Norway au Canada huko ambako ndio wasio na ajira wanazamia, ndio kulitakiwa kuwe na tatizo la ajira, sababu changamoto zote almost zipo covered, hakuna tatizo la madaktari, madarasa, umeme, hospitali wala barabara, sasa wasomi watapata vipi ajira?

Ila Tanzania kuna tatizo la madaktari, walimu, maji, umeme, usafiri, zahanati n.k lakini madaktari, mainjinia, walimu, madereva n.k hawana ajira..!

Yaani kwa maneno mengine ni kuwa Tanzania hatuna ukosefu wa ajira, bali ukosefu wa akili..

Sina hakika mnazungumzia jambo moja. Hata kama ikiwa ni hivo tunarudi palepale - changamoto hutatuliwa na fursa huchukuliwa. Serikali ina jukumu na changamoto (kukuza mahitaji ya huduma na uzalishaji) na wananchi na vyuo kupata na kutoa elimu sahihi kukabiliana na mahitaji. Je anasema kuwa changamoto haziko ila ni wananchi ndio hawana elimu na uwezo sahihi???

Alikusudia kupotosha kwa kutumia maneno mgumu ya falsafa kuzungumzia mambo yaliyo wazi!! Serikali imeshindwa kukuza mahitaji ya huduma na bidhaa!!
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kasema haamini kama tuna tatizo la ajira kwa vijana, bali kuna tatizo la kuoanisha fursa na changamoto

Waliishatuona hatuna la kuwafanya zaidi ya kupiga kelele tu mitandaoni. Yuko sahihi kama akili yake ndio imeona hivyo kwenye suala la ajira tz.
 
Pole pole ameokota mahali desa la enterpreneurship amekariri sasa hata anachoongea yeye mwenyewe haelewi.
Naandaa nondo za hiyo mambo anayoongea hapo nimtumie kwenye email nadhani itamsaidia sana yeye kabla ya kulisha wenzie matango pori. Waliopo hapo nadhani wanahitaji maziwa kuua hiyo sumu waliyonyweshwa
 
Sina hakika mnazungumzia jambo moja. Hata kama ikiwa ni hivo tunarudi palepale - changamoto hutatuliwa na fursa huchukuliwa. Serikali ina jukumu na changamoto (kukuza mahitaji ya huduma na uzalishaji) na wananchi na vyuo kupata na kutoa elimu sahihi kukabiliana na mahitaji. Je anasema kuwa changamoto haziko ila ni wananchi ndio hawana elimu na uwezo sahihi???

Alikusudia kupotosha kwa kutumia maneno mgumu ya falsafa kuzungumzia mambo yaliyo wazi!! Serikali imeshindwa kukuza mahitaji ya huduma na bidhaa!!
Tatizo la ajira lipo complicated zaidi ya hapo kwa serikali kushindwa, japo ina jukumu ndio, nadhani kazi kubwa zaidi ipo kwa wananchi

Serikali inatakiwa iwe mpangaji wa sera na kuweka miundombinu, kisha masuala mengine sasa ya kugeuza changamoto kuwa fursa huku ukipata hela na kutoa ajira linatakiwa kufanywa na sekta binafsi.. Kwa uchumi ambao ni endelevu na wa ushindani serikali haitakiwi kuwa na mkono mkubwa sana

Na nikiangalia, kisera na kimiundombinu serikali haijafanya vibaya sana hadi tuiangushie lawama zote za ukosefu huu wa ajira
 
acheni kuwa brainwashed..yupo sahihi...fursa zipo kibao.....oanisha utoke
Hizo fursa ni Kama zipi zitaje ambayo kijana Toka familia maskini sana aliyemaliza chuo kikuu kwa kusomeshwa kwa mkopo wa serikali aweza asiye Na ajira wala mtaji aweza zitumia
 
Tatizo la ajira lipo complicated zaidi ya hapo kwa serikali kushindwa, japo ina jukumu ndio, nadhani kazi kubwa zaidi ipo kwa wananchi

Serikali inatakiwa iwe mpangaji wa sera na kuweka miundombinu, kisha masuala mengine sasa ya kugeuza changamoto kuwa fursa huku ukipata hela na kutoa ajira linatakiwa kufanywa na sekta binafsi.. Kwa uchumi ambao ni endelevu na wa ushindani serikali haitakiwi kuwa na mkono mkubwa sana

Na nikiangalia, kisera na kimiundombinu serikali haijafanya vibaya sana hadi tuiangushie lawama zote za ukosefu huu wa ajira

Uko sahihi kuhusu kutoiangushia lawama zote za ukosefu wa ajira, nyingine ni zetu kama mtu mmoja mmoja. Hata hivo, ukuzaji wa ajira ni swala la policy na strategies kwanza!! Na aliye na wajibu wa kwanza ni serikali kuwa na baada ya hapo watu hufuata. Mifano itakuwa ni kuhusiana na mikataba, umri wa kufanya kazi, kima cha chini, kodi, mafunzo nk. Ni katika haya ndio serikali inalaumiwa. Kama hakuna masoko ya bidhaa na huduma, mtu anajiajiri vipi?? Kma sheria za kuingia katika ushindani si rahisi, mwenye uwezo kidogo anaingiaje?

Baada ya kutengeneza policies na strategies, serikali itakaa pembeni na kuwa regulator. Sikukusudia kuitaka serikali ijiingize katika uchumi. Hata ikijiingiza - isikatae ushindani kama yetu inavofanya sasa. Ushindani ni kidogo sana kiasi aliyepo hata kama hafayi vizuri- they will survive!! Ushindani halisi ni survival of the fittest!
 
Tulipokuwa wadogo tulikuwa mimi na kaka yangu tunakula kwa bibi yetu kwa vile wazee wetu walikuwa.wapo kazini wakato tukirejea shule. Siku moja tulipokuwa TUSHASHIBA sembe kwa mboga, kaka yangu akasema, "Bibi sembe linanuka mavi"

Slowslow keshashiba sasa anaanza kutukana!
 
Tatizo lile lile nililolisema awali. Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao. Hivyo, wote mnaingizwa kwenye behewa kuelekea kwenye combinations ambazo Taifa limechagua yaani PCM, PCB, PGM, CBG, CBN, ECA, EGM, HGL, HGE, HGK. Ukikosa nafasi kwenye behewa sasa ndio ukatafute hizo fursa zingine za NACTE na VETA.

Falsafa hii na mfumo huu una athari za kisaikolojia. Kwanza unafanywa watu wakikosa nafasi kwenye behewa la form five wajione kuwa ni watu waliofeli na waliopoteza ndoto za maisha. Pili, inafanya elimu ya NACTE na VETA kuonekana kama ni sitara na hifadhi kwa waliokosa nafasi behewani. Matokeo yake, tunapeleka huko kwenye NACTE na VETA waliopoteza matumaini. Yaani tumegeuza NACTE na VETA kuwa ni elimu mbadala na si chaguo tu kama kwenda form 5.

Katika hili nitapenda kutoa mfano wa jamii ya watanzania wenye asili ya asia. Hivi hawa wanaishiaga wapi? Mbona wengi hawaendi form 5 na hata wanaoenda hawasomi HGL, HGK na HGE bali utawakuta aidha kwenye PCB, PCM na ECA na EGM? Na je mbona huko chuo hawaonekani kwenye vitivo vya Sheria, Sayansi ya Siasa, Sociolojia na Historia na Archaeology? Mbona ni kama hawapo kabisa kwenye Masters degree zinazotolewa na Chuo Kikuu kipendwa cha UDSM na pia hawapatikani kule kwenye Masters za jioni za Mzumbe wala zile za Open University? Lakini mbona pamoja na kutowaona huko kote hatuwaoni mtaani wakipita na bahasha za khaki zenye photocopy za vyeti na barua za kuomba ajira?

Wenzetu hawa walishajinasua siku nyingi katika mtego wa fikra tuliouingia wa kusomeshea watoto kwenda kujaza nafasi za wanaostaafu na kufa katika sekta ya umma. Wenzetu wanajifunza stadi zaidi. Anayetaka uhasibu, akifika form four anajisajili kwenye mitihani ya Bodi za Uhasibu (NBAA na ACCA) anaendelea huko. Wengine watakwenda kujifunza masuala ya kukatisha tiketi za ndege IATA system, wengine watakwenda kujifunza stadi za Hardware na Software Engineering na stadi nyingine nyingine. Wengine watasomea u-pilot, wengine insurances nk. Leo nenda kwenye nursery schools walimu wengi ni watanzania waasia kwa kuwa wanakwenda kusomea fani hiyo. Kwao behewa la form 5 ni moja tu kati ya mabehewa mengine na si behewa takatifu au la wateule.

Wenzangu na sisi tunakwenda na behewa, tunaingia chuo tunapigwa sumu ya DS 101 tunakuwa wanamapinduzi na wachukia mabeberu huku tukisoma archaeology, Sociology, Political Science na Kiswahili mwisho wa siku tunasubiri Sekretariati ya Ajira itangaze kazi tunajikuta inaajiri asilimia 10 tu ya waliomaliza chuo. Mwishowe hao hao wasomi wanarudi kuajriwa na mabepari waliokuwa wanawachukia wakiwa chuo.
 
Back
Top Bottom