Polepole: Nape ataadhibiwa na CCM kwa kauli ya kusema alikitoa chama shimoni uchaguzi wa 2015

Katika watu walisababisha ccm iwe katika wakati ngumu,2015 na wewe polepole ulikuepo katika maswala ya katiba yenu
 
Polepole aache unafiki kwani kwa kauli zake alithibitisha kuwa chama kilioza.
Chama kilichoka mpaka akasema kuwa uchaguzi ukiwa wa haki ccm hakitashinda.
Inamaana chama kilioza na yeye alikuwa kwenye upande wa kukibeza chama wakati nape na kinana wakikipigania chama.

Polepole acha unafiki hukua na uchungu na chama kama nape.
Madaraka yasikutie upovu na kujidhalilisha.
Kumbuka kauli zako
Enzi hiyo alikuwa anatetea Serikali 3(tatu) kwenye makongamano tofauti Na msimamo wa Chama.
 
Hata Tanganyika ilikuwepo kabla ya Nyerere. Huenda hakuitoa shimoni, lakini mchango wake kwenye uchaguzi 2015 si wa kubeza.
Kwani alifanya kazi hiyo pekee? Si aliajiriwa kwa kazi hiyo? Nani anayembeza na zawadi ya kazi aliyoifanya alishapewa na kachezea hela kwenye shimo la choo na pesa imetumbukia shimoni. Akafie mbele huko... ati kakitoa chama shimoni.....fankuuuurooo
 
Polepole aache unafiki. Kauli ya Nape ina ubaya gani? Kwani uongo? Kwa nini hakatamka kumwadhibu Mwenyekiti aliyesema Urais aliutafuta mwenyewe wala hakusaidiwa na yoyote! Nani ajui ni CCM ndio ilimpitisha na kumpigania? Polepole halijui hilo?
Huu ni unafiki ambao hata shetani huko aliko anamshangaa!
Nape kama mwanachama unayo haki ya kuusema mchango wake ndani ya chama!
 
Polepole bana!!
Alikuwa anaipigania katiba mpya, akapewa madaraka kaitupilia mbali katiba.
Sasa Nape kusema ukweli anaanza kutapatapa.

Nape akiwa jimboni kwake Mtama wakati anazungumzia sakata la kunyoshewa Bastola alisema yeye ni mchezaji mahiri na mechi bado inaendelea na mapambano yakishika kasi atarudishwa uwanjani tu, hilo linadhihirisha jinsi gani mchango wake ulivyokuwa muhimu kwenye uchaguzi 2015.
 
itasaidia nini muda huu? Ndio atapokewa upinzani? ama ataonesha utoto na uvunjaji wa sheria?? Besides nani atamwamini??
Itasaidia tunaofuata na kutunza historia kuondoa ukungu kutoka katika mdomo wa kada wa CCM.

Upinzani maana yake nini?

Uvunjaji wa sheria gani?

Waliomwamini aliposema goli la mkono akiwa CCM watashindwaje kumuamini akilielezea baada ya kutoka?
 
Hiyo ni kweli,lakini huwez kukataa jitihada za Nape na Mzee Kinana kukiokoa,labda kama kichwa chako kina hitilafu,lakini ukiwa na akili timamu,ukaacha kujitoa ufahamu kishabiki mchango wa Nape au Mzee Kinana wa kuiokoa CCM ya Mzee Mkama huwez kubeza.
Mkuu wanaolima wengine wanaovuna wengine na wanaokula wengine, nape, kinana, mangula walilima. Magufuli, Samia hawa walivuna. H polepole, makonda hawa wanakula
 
pic+nape.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi (KIU) wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa Mwananchi Communications Limited (MCL) wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni hiyo, Tabata Relini jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa UVCCM wa Makao Makuu Idara ya Vyuo Vikuu, Debora Charles. Picha na Salim Shao

  • Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.
  • Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni.

Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa. Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema Nape.

Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa amekengeuka.

“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji Polepole.
Ashugulikiwe Nape. Ikiwezekana AFUKUZWE UANACHAMA
 
Mnyonge mnyongen hak yake mpen. Nape anamchango mkubwa sn UCO mithilika kwa ccm esp 2015 alipambana sn. Pole pole tulikuana kwenye TV mbalimbali ukimponda Lowassa lakn hukuthubutu kufanya ya Nape. Mheshimu kwa jitihada zake huon sahv cdm wanamdoea licha ya kumuita vuvuzela?
 
Back
Top Bottom