Polepole: Nape ataadhibiwa na CCM kwa kauli ya kusema alikitoa chama shimoni uchaguzi wa 2015

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
pic+nape.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi (KIU) wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa Mwananchi Communications Limited (MCL) wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni hiyo, Tabata Relini jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa UVCCM wa Makao Makuu Idara ya Vyuo Vikuu, Debora Charles. Picha na Salim Shao

  • Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.
  • Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni.

Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa. Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema Nape.

Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa amekengeuka.

“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji Polepole.
 
View attachment 500823 Kwa ufupi:
Msemaji wa ccm bwana Polepole kasema kuwa watamwadhibu mh Nape Nauye kwa kauli zake mitandaoni "hasa inazozikosoa chama na serikali ya ccm" hasa kauli anayoutumia kuwa kaitoa shimoni chama hicho kwenye uchaguzi wa 2015.

Kauli hiyo inamaanisha kuwa ccm ilikuwa ya kuzikwa ila yeye ndo kapigana kufa na kupona kukirudisha chama haina ukweli wowote.
Ni kweli bado ninamshangaa nape kumbe ni dhahabu ambayo haijapitishwa motoni.
 
View attachment 500823 Kwa ufupi:
Msemaji wa ccm bwana Polepole kasema kuwa watamwadhibu mh Nape Nauye kwa kauli zake mitandaoni "hasa inazozikosoa chama na serikali ya ccm" hasa kauli anayoutumia kuwa kaitoa shimoni chama hicho kwenye uchaguzi wa 2015.

Kauli hiyo inamaanisha kuwa ccm ilikuwa ya kuzikwa ila yeye ndo kapigana kufa na kupona kukirudisha chama haina ukweli wowote.
Pole pole acha unafiki! kuna uwongo hapo kwani? shame!!
 
View attachment 500823 Kwa ufupi:
Msemaji wa ccm bwana Polepole kasema kuwa watamwadhibu mh Nape Nauye kwa kauli zake mitandaoni "hasa inazozikosoa chama na serikali ya ccm" hasa kauli anayoutumia kuwa kaitoa shimoni chama hicho kwenye uchaguzi wa 2015.

Kauli hiyo inamaanisha kuwa ccm ilikuwa ya kuzikwa ila yeye ndo kapigana kufa na kupona kukirudisha chama haina ukweli wowote.


Safi sana pia msimsahau Bashe na yeye pia tumpe adhabu!
 
Lakini ni kweli alizunguka nchi nzima yeye na kinana, ni kweli alifanya vikao vingi vya ushawishi kwa wanachama wa ccm, ni kweli walifanikiwa kurudisha uhai wa chama.

Logic inasema ukweli plus ukweli plus ukweli+.... =Ukweli. Kazi aliyoifanya Nape na Kinana ni nani mwingine aliifanya?

Hivyo anayohaki ya kuisifia kazi aliyoifanya, ni kama mtu abishe sasa serikali ya JK haikujenga shule za kata hata kama hazifanyi vizuri haitamwondolea ukweli huo.

Kama ni adhabu apewe labda kwa kukosoa chama nje ya mfumo au pasipo kufuata utaratibu.

Lakini je nini kazi ya maendeleo ya technolojia?
 
Polepole aache unafiki kwani kwa kauli zake alithibitisha kuwa chama kilioza.
Chama kilichoka mpaka akasema kuwa uchaguzi ukiwa wa haki ccm hakitashinda.
Inamaana chama kilioza na yeye alikuwa kwenye upande wa kukibeza chama wakati nape na kinana wakikipigania chama.

Polepole acha unafiki hukua na uchungu na chama kama nape.
Madaraka yasikutie upovu na kujidhalilisha.
Kumbuka kauli zako
 
Kwan kinana nanape kilichowasimamisha kidete ninn?wao ndo wenye polis? Wao ndo wenye usalama wataifa? Wao ndo wenye jeshi? Wao ndo walikua mabingwa wa AT acheni kujidanganya nyie mwenye hivo vyombo kwahuku africa kamwe huta muweza labda aamue kukupa madaraka lakin sijui nape sijui na kinana mnaota mchana kweupe.jifunzen burund nkurunzinza mpaka leo napeta nadunia imekaa kimya nawatu wameuawa natanzania ilimpeleka kule burundi naikamuweka madarakan nampaka leo anadunda.vip kwahapa kwentu itakuaje ccm tawala wla usiwe nawasi makufuli malizia kipindi chako halafu tupe mwingine wakushika bendera achana nahawa wababaishaji.wao wenyewe nimiungu watu kwenye vyama vyao
 
Back
Top Bottom