Polepole asipuuzwe;vyovyote iwavyo

Polepole asipuuzwe;vyovyote iwavyo

iZulu

Senior Member
Joined
Feb 2, 2013
Posts
133
Reaction score
164
Licha ya kwamba sikubaliani na Comrade na mtandao wake walivyofanya uhuni kipindi cha utawala ule...ambapo mambo kadhaa yalijitokeza ikiwepo uporaji wa chaguzi, mauaji na upotezwaji wa raia wapinga serikali na chama dola nk!
Pamoja na makosa waliyoyafanya utawala ule; kitu pekee kilichonivutia na kunishawawishi kuanza kufuatilia speech zake ni baada ya kuandika barua ya kujiudhuru ubalozi kwasababu ambazo kwangu mm nakubaliana na hoja zake alizozitoa juu ya namna nchi inavyoongozwa ikisigina misingi ya waasisi wao.
Nukta pekee ambayo katika speech yake; ni baada ya kuanza kurusha jiwe kwenye nyumba ya kioo na mwenye nyumba kuanza kujitokeza juu ya uhuni uliofanywa.

Lakin hatujakaa sawa tumeona wakati wa harambee ya chama, wale waliokula pesa za IPTL, na fedha kubebwa katika masandarusi...hasa mabagachori wakichangia harambee ya Chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu....hapa nikajiuliza maswali kadhaa? Wanapata wapi moral authority kuchangia shughuli za chama?Kwann mafisadi hawa wanarudi kwa kishindo? Kwann wanajitokeza wakijinadi kama raia wema ilhali wengine wana uraia pacha? Kuna nini nyuma ya harambee na michango yao kuelekea uchaguzi mkuu?
Speech zake zimenifanya kua katika tafakuri ya matukio mbalimbali yanayolingana au matokeo ya kile anachokisema.
Kwakuwa, mwenye macho aambiwi tazama na mamlaka husika kazi kwenu kama mtakaa kimya au kukanusha au kukubaliana na haya yanayosemwa.

Kulingana na ulinganishi wa hoja na matukio yanayoendelea nchini, Polepole ni kama Mtolewa katika Utawala Bi Kirembwe hivyo hoja zake hapaswi kupuuzwa hata kidogo.

Nawasilisha.
 
Licha ya kwamba sikubaliani na Comrade na mtandao wake walivyofanya uhuni kipindi cha utawala ule...ambapo mambo kadhaa yalijitokeza ikiwepo uporaji wa chaguzi, mauaji na upotezwaji wa raia wapinga serikali na chama dola nk!
amekiri na kutubu dhambi!
 
Back
Top Bottom