Polepole asijifanye hamnazo. kauli mbaya na kebehi zinaichonganisha ccm na waTz.

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,995
60,485
..kichwa cha habari kinahusika.

..kila mtu fulani anapofungua kinywa chake basi hutokea taharuki ndani ya nchi.

..haijapita miaka miwili tangu akalie "kiti cha enzi" lakini ameshafurumusha maneno mabaya kuliko viongozi wote waliopata kutokea ktk nchi hii.

..siyo utamaduni wa waTz kuzungumza ngono na katerero mahali palipotokea majanga, au mbele ya watoto na vijana. Hakuna kiongozi aliyepata ku-behave namna hiyo.

..John Malecela aliwahi kusema "they can go to hell". Lakini alisema hayo kwenye kikao na viongozi wenzake siyo ktk mkutano wa hadhara ambapo nchi nzima inasikiliza.

..Cleopa Msuya alipata kusema "kila mtu abebe msalaba wake." Alitoa kauli hiyo bungeni ktk mjadala uliohusu kulipa kodi. Hakutoa kauli hiyo kwa wananchi waliokumbwa na tetemeko na kupoteza wapendwa wao na mali zao.

..kwa muda mrefu viongozi hao walilaumiwa kwa kutoa kauli ambazo zinawafanya wao kama viongozi kuonekana hawawajali wale wanaowaongoza.

..huyu wa sasa hivi amerudia kilekile walichokisema Malecela na Msuya. Lakini yeye amekwenda mbali zaidi kwa kuelekeza kauli zake moja kwa moja kwa wananchi waliokumbwa na maafa.

..Je viongozi hawatakiwi kujifunza kuepuka makosa ya watangulizi wao?

..kuwaambia wananchi MWAFAA kwa maoni yangu ni sawa na kuwaambia they can go to hell. Anayependa kujifunza na kusikiliza ushauri mzuri angeepuka kosa hilo.

..Kwa mtizamo wangu Mh.Polepole angeomba RADHI/MSAMAHA kwa niaba ya CCM. Kujaribu kuwatupia lawama wapinzani au kujaribu kuzifafanua kauli hizo kunaharibu taswira ya chama na ya kwake binafsi Polepole.
 
Nyumbu badala ya kukomaa na kauli za ccm, ni bora mkakomaa kutimiza ahadi zenu kwa wananchi.

Mliahidi Arusha ikiwa chini ya chadema itapaa kimaendeleo kama ulaya, lkn mpaka sasa mwaka umeisha hamna chochote ni porojo tu.

Je mwaka 2020 mtatudanganya na nini wananchi Wa Arusha??
 
Ndio maana ccm wanatumia nguvu udini ukabila na kuweka watu ndani ili wapate jimbo

swissme
 
Hongera mkuu,

Hayo yote uliyoorodhesha katika mada yako, wakati mwenyekiti anayasema wapinzani walikuwa kimya kabisa..

Sasa sijui polepole huo mzigo anawabebesha vipi wapinzani!
Kuna maneno mengine yakitamkwa na mtu mwenye dhamana kubwa kama hiyo nyie wananchi mnainamisha vichwa chini.. Aibu!!
 
Nan amekudanganya ccm inapendwa huku ..yaaan sasa hivi tunavuna ile million tatu ...( miliin 8-6 sawa 2 kwa iyo kwa kauli zao tunavuna tusiposhinda 2020 nahama nchi
 
Hahaha..... Polepole anatuchonganisha Mbona magufuli alisema ni mataji ri na hata waziri mkuu kasema ni matajiri wanaosukuna waandishi waandike kuwa Kuna njaa...... Polepole... Anatafuta Kiki
 
Hahaha..... Polepole anatuchonganisha Mbona magufuli alisema ni mataji ri na hata waziri mkuu kasema ni matajiri wanaosukuna waandishi waandike kuwa Kuna njaa...... Polepole... Anatafuta Kiki
Ni vema ukahama kesho maaa katiba ni ile ile hivyo non maadiliko
 
Nyumbu badala ya kukomaa na kauli za ccm, ni bora mkakomaa kutimiza ahadi zenu kwa wananchi.

Mliahidi Arusha ikiwa chini ya chadema itapaa kimaendeleo kama ulaya, lkn mpaka sasa mwaka umeisha hamna chochote ni porojo tu.

Je mwaka 2020 mtatudanganya na nini wananchi Wa Arusha??
Mwehu wewe, umeona ya Arusha tu!
 
Back
Top Bottom