Hoja kuhusu “kufungwa miguu na mikono” anayoitumia mgombea Urais wa CCM

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Hii ni kauli ambayo Dkt. Magufuli alitumia sana jana katika mkoa wa Kilimanjaro na arumeru mkoani Arusha na probably atairudia kwenye mikutano iliyobaki ya kampeni. JPM ana maanisha wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia kumchagua mbunge toka kambi ya upinzani ni kufungwa miguu na mikono hata asiweze kuleta maendeleo katika jimbo husika.

Kauli hii imenifanya nijiulize maswali kadhaa;

  • Je jimbo lenye mbunge toka upinzani ni himaya ya uasi?kiasi kwamba hawezi penyeza miradi ya maendeleo?
  • JPM anapingana na sheria mama ya nchi iliyoruhusu uwepo wa mfumo wa vyama vingi?
  • Kama wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani wameweza kukaa jengo moja la bunge kwa amani na kujadili masuala ya kimaendeleo ya nchi inakuwaje leo unalaumu wananchi wa majimbo yao eti walikufunga mikono na miguu??
  • Kuwepo mbunge kutoka kambi ya upinzani katika jimbo Fulani kuliweka kizuizi gani kwa JPM kufanya lolote la kimaendeleo ktk jimbo husika?.
  • Mbona sources kubwa za mapato yanayochangia kiasi kikubwa cha GDP ya nchi yetu ziko majimbo yanayotawaliwa na upinzani nab ado serikali inaingiza mapato makubwwa kupitia majimbo hayohayo. Mfano sehemu kubwa ya mlima Kilimanjaro na njia nyingi za kupandia mlima zipo kwenye majimbo ya upinzani, mbuga za Wanyama za Ngorongoro, Manyara, Momela, Tarangire, Serengeti, Uwanja wa kimataifa wa KIA nk. Zimewakuwa au kuwahi kuwa kwenye majimbo ambayo yaliongozwa na wapinzani. Je mapato yalishuka kwa sababu wapinzani walikuwa wabunge?
  • Je anaweza thibitisha kwa statistics kuwa uwepo wa wabunge wa upinzani ulipunguza kasi ya maendeleo ya nchi kwa maana ya kufungwa miguu na mikono? Ni vema pia akamalizia kutuambia kama hawa wanaoitwa wabunge wa upinzani ni maadui wakubwa wa maendeleo ya taifa na siyo co-workers wenye mawazo mbadala.
  • Ni kwa jinsi gani watu waliosababisha JPM afungwe mikono na miguu bado wanaachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria na badala yake anarudi kwao tena kuomba kura?
  • Kama wabunge wa upinzani wamekuwa Kamba za kumfungu mtu miguu na mikono inakuwaje chama tawala kinawasaka kuwanunua kwa gharama kubwa kisha kuwafanyia recycling kupitia chama chao? Je wamewawekea moyo mpya, au wamewapa kichwa kipya akili mpya n.k. Kumvisha mtu aliyetoka upinzani vazi la rangi Fulani haitoshi kumfanya awe ameongoka na kubadili mrengo; mtoto wa nyoka ni nyoka na ana sumu ilele walio nayo nyoka wakubwa. Tungetegemea wakitoka upinzani wasipewe hata ujumbe wa nyumba kumi maana kazi yao ni kuzuia maendeleo; lakini wanaokufunga Kamba hawahawa wakija upande wa chama tawala wanakuwa vyombo vitakatifu na wanateuliwa kwenye nafasi za uwaziri, wakuu wa wilaya nk. Hii ni double standard na flaw ki weledi na utashi wa viongozi wetu wa kisiasa.
USHAURI

  • Tunapofanya kampeni tusiwe shortsighted kwenye kushinda uchaguzi ni vema tuangalie long term impacts ya tunayoongea kwenye kampeni kwa watanzania baada ya uchaguzi haswa tunaotarajia watupe dhamana ya kuongoza nchi yetu. Note kuwa mambo mnayoongea yanabaki kwenye kumbukumbu za wapiga kura kwa muda mrefu.
  • Tusiwaamini sana wanaotushauri kuhusu silaha na mikakati ya kutumia ili kushinda uchaguzi lakini busara ituongoze kuchagua maneno ya kuongea kwa umakini maana tutajikuta tunapandikiza chuki na migawanyiko ya kijamii katika nchi yetu.
  • Mtu anapokuwa kwenye kampeni ni sawa ana mlevi aliyelewa na kuongea chochote kinachomjia na ghafla ulevi unamtoka na kuwa sober ghafla na anajikuta amechafuka na amechafua wengine kwa kuwatemea na kuwatapikia pomber lakini anataka kufanya quick fix aonekane normal but its too late umeshaacha kumbukumbu mbaya. Vinvyo hivyo viongozi wa kisiasa hangover ya kampeni ikiisha na akashinda uchaguzi anaweza kushindwa kuongoza vema kwa sababu atatumia mudamwingi kujaribu kufuta kauli za wakati wa kampeni, kurudisha umoja, kujionyesha una upendo wakati damage ilishatokea. Eleweni kuna maisha baada ya kampeni na mliyoongea wakati huo hayatafutika katika mioyo yetu
  • Tuwe na kiasi kwa kila tulitendalo na waswahili husema TUWE TUNAWEKA AKIBA YA MANENO’’
  • Tusiamini sana wale wanaotlamba miguu na kujidai kutufuta jasho kama bibi harusi; ni vema tukapima dhamira na malengo yao. Unaweza ukafikiri wanakutakia memema kumbe wengi wanangalia ugali wa familia zao kupitia mgongoni kwako. Wengi wao hawaoni mbali Zaidi ya usawa wa sahani ya ugali wanaoutafuta kupitia mgongo wa mgombea husika.
  • Marafiki wa kweli wako real, sio limbukeni,ni adimu sana kuwapata kwa sababu wanajua urafiki wa kweli una gharama kubwa na hivyo huwezi wakuta wakijipendekeza kuwafuta watu viatu au kukupigia makofi; hivyo kuweni sana makini na kila anayewazunguka. Kumbuka mwanafunzi kipenzi wa YESU aliyeitwa PETRO ndiye aliyemkana YESU mara tatu. THIS IS THE LAW OF NATURE
 
Mimi naona sehemu walizochagua upinzani ndo wanapelekewa maendeleo kwa wingi mfano Kawe, Kilimanjaro na Arusha na hata akipita Raisi anajidai huko kwa miradi mizuri lakini huku majimbo vya chama tawala hata kutembelea hapiti kabisa na maendeleo tunayasikia tu.
 
Nenda Mtela huko kwa kina Kibajaji ukashuhudie maendeleo makubwa kama Chicago.

Au nenda Kongwa jimbo la spika wa bunge ukashuhudiw maendeleo makubwa na faida za kuchaguwa ccm
 
Ameishiwa hoja huyo mzee.
 
Je anakusanya kodi kutoka kwenye majimbo yanayoongwa na upinzani.....kama jibu ni ndiyo je anakwama wapi huyu mtu....
 
Back
Top Bottom