Poleni watu wa Kigamboni hiyo ndio CCM

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,288
2,000
TANESCO wamekata Umeme Eneo la Kurasini mpaka Kigamboni baada ya Mbunge wa (CCM) Ester Bulaya kumtaka Waziri Mkuu atoe maelezo kwa niaba ya Serikali kuhusu tatizo la fidia ya Wananchi wa Kigamboni inayopigwa danadana na Waziri Tibaijuka Poleni sana Wana-Kigamboni.

Hiyo ndio serikali sikivu ya CCM najua 2015 hamtofanya tena makosa kama ya 2010.

Kufanya kosa sio kosa kosa kurudia makosa kila jambo na uonevu wote huu una mwisho wake.
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
TANESCO wamekata Umeme Eneo la Kurasini mpaka Kigamboni baada ya Mbunge wa (CCM) Ester Bulaya kumtaka Waziri Mkuu atoe maelezo kwa niaba ya Serikali kuhusu tatizo la fidia ya Wananchi wa Kigamboni inayopigwa danadana na Waziri Tibaijuka Poleni sana Wana-Kigamboni
Hiyo ndio serekali sikivu ya ccm najuwa 2015 hamtofanya tena makosa kama ya 2010
Kufanya kosa sio kosa kosa kurudia makosa kila jambo na uonevu wote huu una mwisho wake.

Mbona hakuna uhusiano wa matukio hapo?
 

xenaxena

JF-Expert Member
May 20, 2014
2,237
1,500
Dada ester kuwa makini chama kimekulea ni maoni tu
Tunadhani ni bora waingereza walioanzisha shule za middle school ili kupata makarani ,kuliko Mjerumani aliyetawala bila kutoa hata tongotongo za watanganyika,Ninamaana chama unachosema kimemlea ni kipi hicho?, hiki kilichomfanya azaliwe akiwa na upungufu wa IQ?, kutokana na manesi waliochelewa kumsaidia mwanamke asijifungue mapema kwa kukosa mishahara?
Ni hikihiki chama kilichofanya aende shule na kuishia drs la vii nakushindwa kupata elimu bora kutokana na walimu waliokosa elimu nzuri( dv 5),au waliona mshahara duni wa tsh298000/=,?kuishi nyumba duni?,
Ni hiki chama kilichomfanya akose maji safi,matibabu safi ambapo aliandamwa na magonjwa na kumfanya ashindwe kufaulu kwa alama za juu?
Ni chama hiki ambacho kimesababisha mazao yake yakose bei hivyo kumfanya akose ada ya kumlipia mwanae na kujenga nyumba bora kwa sababu ya gharama za vifaa vya ujenzi vinavyouzwa na wezi gwa wa chama hiki?,
Ni hiki chama kilichomfanya akose sehemu ya kudai hski zake wakati ardhi inakombwa na wakubwa huku yeye akiishia kuuza nyanya,sambusa,mchicha,vitunguu na maeneo anayouzia ys chama hiki hufukuzwa? ,na kuibiwa vitu vyake?
Ni kweli chama hiki kimemlea kwa kumpandishia gharama za usafiri ili hela kidogo anazopata baada ya kuuza mchicha aushie kulipa nauli na kula mlo mmoja hivyo kupelekea apatwe na magonjwa ya mara kwa mara?, ni kweki chama kimemlea kwa kutwaa ardhi yake ambayo ingekuwa mkombozi wake kama alivyoliacha Taifa baba yetu mzalendo aliyekuwa siku zote akiona maskini ombaomba anatoa machozi? Daaa umenena chama kimemlegeza hakijamlea!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom