battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,672
- 2,540
Ilikuw kawaida tokea Mzee Mwinyi alipomaliza muda wake wa Urais, hatukuwa na namna ya kumpata Rais mwingine toka Zanzibar.
Wazanzibar tulibakia na Umakamu tu na mpaka ikawa ndio majaliwa yetu. Lakini kifo cha Magufuli kimeleta jambo lisilozoweleka.
Kazi za Makamu wa Rais ni kufungua makongamano na kutembea na mikasi kufungua miradi na majengo au kuweka mawe ya msingi.
Pili ilikuwa kushughulikia Mazingira.
Uendeshaji wa Serikali ulikuwa chini ya Rais na Waziri Mkuu, sasa kibao kimegeuka. Najua mnatamani mbadili Katiba ili angalau Makamu aongezewe status katika maamuzi, lakini itabidi mvumilie mpaka pale mama atakapoona kuwa inafaa hivyo.
Natamani pia kuona Serikali ya mama akimteua Mkuu wa Usalama Mzanzibari, Mkuu wa Majeshi Mzanzibari na Mkuu wa Polisi Mzanzibari ili combination iwe sawia.
Ndugu zetu watanganyika wabakie na Maboksi ya Mikasi na Makamu wao ili waone ladha ya umuhimu wa Serikali Tatu zilizopendekezwa na Warioba.