Uchaguzi 2020 Poleni wapinzani

Aneth Anton

Member
Nov 22, 2019
20
45
Duniani kuna njia 3 tu za kutwaa uongozi wa taifa.

Njia ya kwanza ni ya mazungumzo. Njia hii mfano mzuri ni Mwalimu Nyerere. Aliitumia akatwaa uongozi wa Taifa.

Ni njia ngumu mno inayohitaji kipaji cha kupanga hoja (power of thinking and analyzing), kuongea (power of oratory), ushawishi (convincing power), uadilifu (integrity) na uhamasushaji umma (mass mobilization).

Mwalimu alikuwa gwiji wa yote haya. Njia hii mpumbavu au mjinga akiitumia hafanikiwi ng'o!

Njia ya pili ni ya kutumia mabavu. Museveni ni mfano mzuri. Unatwaa utawala kwa mabavu.

Njia hii imetumiwa na watawala anuwai duniani. Mtake msitake atatwaa alimradi ana nyenzo za mabavu ambazo ni watu wanaomuunga mkono, silaha na utawala dhaifu.

Njia hii haifui dafu kama hivi vitatu havipo. Ni wehu kuijaribu njia hii ikiwa haya hayapo. Moja ya nchi ambayo haya hayapo ni Tanzania.

Unaweza kukataa lakini tuliza akili utauona ukweli. Ni ngumu mtu kutwaa utawala kimabavu Tanzania.

Try at your own peril. Kuna nchi za wenzetu pia zimefikia hali hii ya kuwa na 'immunity'. Huwezi kutwaa madaraka kwa nguvu mfano US, UK, Japan! Hakuna nafasi!

Kama kuna jambo Mwalimu anapaswa kuenziwa ni hili! Alilisuka Taifa hadi likapata hii immunity. Mimi naiita IMMUNITY AGAINST FORCED ENTRY INTO POWER.

Unaweza kudai unavyotaka au akili yako inavyokutuma! Ukweli utabaki ukweli. Kuingia kwa mabavu Tanzania haiwezekaniki.

Njia ya tatu ni ya sanduku la kura. Njia hii inakubalika kila kona duniani. Hii ni kwa kuwa historia imetufundisha kuwa sio kila mmoja ana uhodari wa kuongea hadi apewe utawala wa taifa.

Pia kuingia madarakani kwa nguvu kuna athari nyingi kuliko faida. Tizama Libya, Iraq, Afghanistan na Yemen. Watu wameingizwa kwa nguvu madarakani matokeo balaa tupu!

Hapo ndio wapinzani Tanzania walipopotea sana.

Njia ya kwanza imewatupa mkono. Hawana karama ya maongezi! Hata wangepewa nafasi ya kuongea kutwa kucha bado njia hii isingewaingiza madarakani.

Ni njia wasiyoiweza kabisa. Nyerere licha ya kufungwa, kushitakiwa, kudhihakiwa, kusumbuliwa na mkoloni hakuwahi kuwatusi au kupinga mipango yao ya maendeleo japo maendeleo yalikuwa yanalenga UK!

Akiongea nao kwa staha. Alijenga hoja. Hebu fikiria kauli za wapinzani wetu? Hebu fikiri wanavyosherehekea ndege kukamatwa? Hebu fikiria wanavyopinga ujenzi wa reli au bandari? Ni tofauti mno. Njia ya mazungumzo haiwafai!

Ukitizama njia ya mabavu ndio kabisaa! Hawana nyenzo hata moja kati ya zile 3 ili waweze kutumia mabavu.

Lakini utasikia "TUSILAUMIANE", "NGUVU YA UMMA" Kichekesho! Njia hii wala wasiiote! Hawana uwezo.

Kwao njia iliyosalia ilikuwa ya sanduku la kura! Sasa kituko wameitupa mkono.Sawa na masikini ana hela ndogo anaichezea kamari!

Sasa hivi wapinzani wamekosa njia yoyote ya kutafutia utawala wa nchi. Njia zote tatu kwao zimekwama.

Na wasipojirekebisha wakaamua kutumia njia pekee ambayo walau wanaweza kufurukuta yaani njia ya sanduku la kura mwaka 2020 watajuta milele.

Huwezi kuwa mkulima ukatae kutayarisha shamba! Au ukatae kulima udai mwenzako aliyelima atakutambua!
 

Rungutira

Member
Dec 11, 2018
49
125
Sijasoma Mpaka Mwisho lakini bandiko lako seems umeandika rubbish... Hauna lolote la kuwashawishi watanzania kuhusu hii idea yako... Uchaguzi /uchafuzi uliomalizika umeangukia njia yako unayohita numba mbili whether you like or not....Endelea kujifariji...
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
92,511
2,000
Huyo mleta mada ni sawa na kina Jinga lao na kina Magonjwa Mtambuka
Sijasoma Mpaka Mwisho lakini bandiko lako seems umeandika rubbish... Hauna lolote la kuwashawishi watanzania kuhusu hii idea yako... Uchaguzi /uchafuzi uliomalizika umeangukia njia yako unayohita numba mbili whether you like or not....Endelea kujifariji...
 

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,731
2,000
Mwanzoni umejenga hoja vizuri lakini umeishia kuwalaumu wapinzani as though hawana support katika nchi, hilo si kweli! Nakubaliana na wewe njia ya kistaarabu ya kuingia madarakani ulimwenguni kote ni sanduku la kura, lakini jiulize toka tupate uhuru njia hii ya kistaarabu imekuwa ikitumika, hata sisi tuliozaliwa ndani ya mfumo wa chama kimoja tuliikuta na watu walikuwa wanashindana kweli kweli kwa hoja, jiulize hii hatua ya kistaarabu tuliyokuwa tumefikia kwa nini awamu hii inaonekana ni mbaya mpaka zinatumika mbinu za ovyo ovyo mpaka tunaonekana wajima? Huu ni udhaifu wa uongozi wa amu hii ambao unaamini demokrasia ni adui wa maendeleo!! huu ni mtazamo wa ovyo kutokea katika karne hii.

Nikukumbushe kwamba wapinzani wakikosa mahali pa kupumulia kwa kuwa mmeziba kila sehemu kitakachofuata ni kama kujifungia na paka chumba kimoja na huku ikimchapa fimbo - atakurarua!! mpe nafasi ya kukimbia, maana yangu ni hivi kutatokea vitendo vya maasi na terrorism. It might not be today but i can guarantee you we are heading to ditches and i would not like this to be the legacy of our generation. Kama umenote ushindi wa 99.9% mbona haushangiliwi mtaani? tafsiri yake ni kwamba you have grabbed power by force and therefore you don't have legitimacy and that is why you are losing confidence.
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
8,807
2,000
Pole kwani pole pole umeanza kukolea propaganda za kitoto za H Polepole. Uchaguzi UPI unaousema wapinzani wangeshiriki? Huu huu uliyoibwa na wenzenu kabla hata ya kuanza?

Kwa taarifa yako, Tanganyika ilikuwa ni Trusteeship haikuwa colony la Uingerezà kama Kenya au Zimbabwe. Tanganyika Ilikuwa chini ya UN, suala la uhuru lilikuwa sehemu ya mipango, baada ya vita kuu ya kwanza. Tatizo pekee ilikuwa ni uhuru uwe lini. Vita haikuhitajika hapa.

Nyerere kwa bahati aliweza kulijuwa hili vizuri. Na pia ndio maana Waingereza hawakuishupalia sana nchi hii.

Waweza kujisomea kidogo na kujibidiisha kidogo kuchambua ili ikusaidie kuachana na propaganda za wanaolazimisha kuonekana wanapendwa. Pole sana.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
6,469
2,000
Wewe Mleta mada, ina maana figisu zoote ulizozishuhudia ili wapinzani wasisogelee hata hilo sanduku la kura huzioni?. Au umejitia upofu na uchambuzi wako huo uchwara uliobiased?

Ina maana wewe hukumbuki chaguzi za marudio za wabunge zilivyoendeshwa?

Ina maana umesahau juzi tu hapa 96% ya wagombea wa Chadema walienguluwa bila haki na 97% ya wagombea wa ACT waliondolewa bila haki?

Unajifanya hujui yatokeayo kwenye chaguzi za Zanzibar, mfano uchaguzi wa 2015?

Kiufupi, CCM wanaogopa sanduku la kura na wapinzani wamekuwa wakigain nguvu kwenye sanduku la kura kwa hiyo CCM na serikali yake wamekuwa wakivuruga michakato hiyo.

Mleta mada unaonekana una akili, lakini kwa sababu unapenda uonekane uko sahihi basi una twist narrative yako ionekane ndiyo reality wakati reality unaijua.

Na reality ni hii, IWAPO KUNA CHAGUZI ZILIZO FAIR NCHINI, CCM ITALOSE BIG TIME. Hili wanalijua na ndo maana wanaharibu process za uchaguzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom