Baada ya tume iliyoundwa na mh. Raisi kukamilisha kazi yake, ndio matatizo ya mikopo yameongezeka mara kadhaa. Wanafunzi wanaendesha maisha yao kwa kutegemea mikopo wamezidi kutengwa kutoka kwa wanafunzi wanaotoka familia bora wasiotegemea mikopo, ambao huwa darasani wenzao wanapozunguka na njaa wakifuatilia mikopo. Labda tushauri mihula ya masomo ya haya makundi mawili iwe tofauti, wa mikopo wasome wakati HESLB inakuwa na fedha!? Mvumilivu hula mbivu, mtafikia malengo yenu. Poleni st John, UDOM, Tumaini-Iringa kwani mmekwenda sikukuu hata majina ya mikopo hayajafika na muda ukiwa umepita, poleni na wengine wote.