Jana pale Kigogo Sambusa wananchi wamekataa kuokolewa na kikosi cha Zimamoto baada ya nyumba zao kuzungukwa na maji wakidai hawataki kuacha vitu vyao ndani ya nyumba
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo jingine wakiambiawa msijenge mabendeni hawakubali yakiwapata mafuriko wanalalama hakuna msaada wakati walikwishaambiwa au kujenga kiholela ili majanga ya moto yakitekea basi zimamoto wawezekufika kwa haraka lakini hawakubali.Nasikitika kuona Tanzania kutokuwa na idara imara ya kuokoa maisha ya watu. Ndugu mmoja kaniambia kaokolewa na majirani kwenye mafuriko Dar cha ajabu hakuna kikosi cha zimamoto watu idara yetote y serikali imeenda kumsaidia kumwangalia wala nini. Sasa tujiulize hizi idara zinafanya kazi gani. Ni kwamba hazijapewa pesa, hatuna vifaa au ni kwamba wana kila kitu lakini hawajui kazi yao. Serikali wamekuwa wakaguzi tu lakini sio waokoaji. Tatizo lingine kila mapungufu tulionayo kuna watu watatetea badala ya kulalamika. Zile namba zilizofunguliwa za ukipa tatizo unapita zinafanya kazi gani?
Nadhani kuna tatizo la kukariri pia. Siku hizi mvua zikinyesha Dar popote pale panaweza kufurika, mfano makutano Nssf, Kijitonyama, Mbezi-chini n.k.Tatizo jingine wakiambiawa msijenge mabendeni hawakubali yakiwapata mafuriko wanalalama hakuna msaada wakati walikwishaambiwa au kujenga kiholela ili majanga ya moto yakitekea basi zimamoto wawezekufika kwa haraka lakini hawakubali.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani huyu baba yangu mdogo imebidi anipigie simu USA kuoma pesa kapoteza kila kitu na anasema majirani ndiyo waokoaji hakuna serikali wala nini
Mimi nafikiri hakuna ubunifu kuna JKT, kuna asikari kibao pale Lugalo wanashinda kupalilia bustani pale siku nzima wakati wananchi wanaowalipa wako kwenye mafuriko, magari ya jeshi yame park na kutengenezwa kwa kuchakaa mengi bila kutumika, tunafumdisha ukakamavu JKT kwanini yakitokea majanga wasiletwe hata kwa muda mbona korosho walienda kubeba wataahidwa kubeba watoto
Wakati watanzania wengine wako kwenye mafuriko watu wengi wanajali zaidi siasa wakati hawa ni walipa kodi
Huyu mtu anapaswa kumshukru mheshimiwa rais wa awamu ya tano kwa juhudi zake maana amewapa majirani zake roho nzuri na moyo wa upe do otherwise alikuwa asombweNasikitika kuona Tanzania kutokuwa na idara imara ya kuokoa maisha ya watu.
Ndugu mmoja kaniambia kaokolewa na majirani kwenye mafuriko Dar cha ajabu hakuna kikosi cha zimamoto wala watu kutoka idara yoyote ya serikali imeenda kumsaidia kumuangalia wala nini.
Sasa tujiulize hizi idara zinafanya kazi gani. Ni kwamba hazijapewa pesa, hatuna vifaa au ni kwamba wana kila kitu lakini hawajui kazi yao?
Serikali wamekuwa wakaguzi tu lakini sio waokoaji. Tatizo lingine kila mapungufu tulionayo kuna watu watatetea badala ya kulalamika.
Zile namba zilizofunguliwa za ukipata tatizo unapiga zinafanya kazi gani?
Uko sahihi,huu ujenzi maeneo hatarishi kama mabondeni au karibu na mikondo ya maji bila kusahau ujenzi holela bila kufuata utaratibu unakwamisha uokoaji.Wataendelea kulaumu na kufa pia kama hawataki kutoka sehemu hatarishi,kila siku serikali inasisitiza watu wahame ila hawataki sa serikali ifanyaje?
NB: Wanaweza kuendelea kuishi maana hata serikali yenyewe imejenga kituo Jangwani wakati wanajua hapafai.
macson