Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 7,170
- 8,622
Bodi ya Ithibati ya waandishi wa habari haikuona Majaliwa akishangiliwa?
---
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Tanzania ( Jounalist Accreditation Board) imempa muda wa masaa 24 Mwandishi wa habari Mwandamizi Paschal Mayala kuthibitisha kauli yake aliyoitoa kwenye kipindi cha JAMBO ASUBUHI kinachorushwa na Jambo Television kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba alichukizwa na kitendo cha waombolezaji waliokuwa kwenye ibada ya mazishi ya Marehemu Kadrinali Pengo kuwashangilia viongozi wakuu wastaafu akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, Dkt.Philip Mpango, Jaji Joseph Warioba na Mizengo Pinda huku yeye (Mwigulu) akikosa kushangiliwa msibani hapo.
Pia soma
Dar es Salaam, 03 Machi, 2026
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za Habari na Kanuni zake, ilifanya kikao cha majadiliano na Mtangazaji WILBERFORCE NGOTO pamoja na Mchambuzi wa masuala ya kisiasa PASCAL MAYALLA, wote wakiwa Waandishi wa Habari Wenye Ithibati, kufuatia maudhui yaliyotolewa katika kipindi cha Jambo Asubuhi kinachorushwa na Jambo TV.
Kikao hicho kililenga kujadili kipande cha taarifa chenye kichwa: "Mwigulu hakufurahia akina Majaliwa kushangiliwa msibani", kilichosambazwa mtandaoni. Baada ya majadiliano ya kina, Bodi ilibaini kuwa maudhui hayo yalikuwa na upungufu wa kimaadili, yakihusisha hitimisho lisilothibitishwa na kichwa cha habari chenye taswira ya shambulio binafsi bila kuwa na vielelezo vya kuthibitisha muktadha halisi wa madai yaliyotolewa.
Wahusika walikiri makosa, kuomba radhi na kuahidi kuimarisha umakini na weledi katika vipindi vijavyo. Kwa kuzingatia utayari wao wa kurekebisha makosa, Bodi imewapa ONYO na kuwataka kuzingatia maadili, nidhamu na misingi ya taaluma.
Bodi inasisitiza kuwa lengo lake si kuminya uhuru wa habari, bali kulinda hadhi ya taaluma na kuimarisha uwajibikaji. Ikumbukwe kuwa uhuru wa kukosoa unatambuliwa katika Kifungu cha 52(2) cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, hata hivyo uhuru huo unapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia ukweli, uthibitisho wa taarifa, staha na kuepuka mashambulizi binafsi.
IMETOLEWAΑ ΝΑ: -
Patrick Kipangula
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB)

- Paschal Mayalla: Mwigulu Nchemba hakufurahia Majaliwa, Warioba na Pinda kushangiliwa kwenye mazishi ya Kardinali Pengo
- Dkt Nchimbi: Kuna raha yake kupigiwa vigelegele Vs Dkt. Mwigulu: wanalinganisha makofi, sijaletwa kwa ajili ya kupendwa
- Maoni ya Pascal Mayala kuhusu Mwigulu yawaamsha TCRA, Jambo TV yalimwa barua ya onyo kali, kuwa chini ya uangalizi kwa Miezi 6
BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAANDISHI WA HABARI MAYALLA NA NGOTO WAONYWA UKIUKWAJI MAADILI