"POLE sana RAIS wangu KIKWETE" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"POLE sana RAIS wangu KIKWETE"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magwero, Apr 15, 2012.

 1. M

  Magwero JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Zamani nikiwa mtoto mdogo,nikiwa bado mwanafunzi wa shule ya msingi Mabatini..
  Babangu alinipatia magazeti mara kwa mara, nipate kuyasoma na yeye akinisikiliza..
  Leo nikiwa mtu mzima nagundua dhamira ya babangu kwangu, kwamba niwe nafahamu kusoma kwa fasaha na haraka zaidi na kunijengea tabia ya kupenda kusoma..
  Sitaki Amini kama alifanya hivyo ili kusikia sauti ya mtoto wake wa pekee na aliyempenda zaidi..
  Sitaki Amini hvyo kwa kuwa mara kadha wa kadha alinikosoa na kunifundisha namna ya kutamka maneno ambayo sikuweza kufanya hivyo kwa kipindi kile..!!sasa
  Nikiwa nataka achana na habari za marehemu Babangu na GAZETI alizokuwa akinipa nizisome..
  Kuna swala moja ambalo leo limenisukuma kuandika kurasa hii...
  Ni lile swala la "BARUA YA WAZI KWA ....,..."katika magazeti ya kipindi kile..siku hizi sio sana..
  barua hzi zilikuwa zinawezwa elekezwa kwa Taasisi au kwa mamlaka fulani au kwa kikundi cha watu au hata mtu mmoja...
  Zilikuwa zikiandikwa kwenye kurasa za MAGAZETI,hata kama waandishi hawa walikuwa wanajua anwani za watu hawa,au taasisi husika..
  Sijajua kwa nini waliamua kufanya hivyo..

  Sasa leo,, Mim ninajua kuwa Raisi wangu Jakaya ni moja ya watu Makini na Wenye uwezo mkubwa wa kupembua na Kuchambua Mambo..!!
  Ndiyo..,ndivyo alivyo rais wangu,, na Jamii Forum ndiyo mahala watu wote wenye sifa kama nilizozitaja kwa rais wangu wanapatikana hapo..!
  Hvyo sina shaka Rais Kikwete ni mchangiaji mkubwa wa mada mbali mbali zinazowekwa Jamvini..

  Hivyo na mimi nikaona ni vema kuchukua fulsa hii kumwandikia Rais wangu mpendwa JK, barua hii ya wazi ..!!

  "Mheshimiwa Rais , kabla ya pole zilizonifanya kukuandikia barua hii,, kwanza nikupe PONGEZI kwa kulipeleka taifa letu kwenye hatua ya kihistoria ya Mchakato wa Uandishi wa KATIBA mpya..!!hakika hakuna hatakae sahau jambo hili gumu ulilolikubali litukie katika utawala wako..
  Najua ya kwamba Taifa letu, ni lazima lingefikia hatua ya kuandika Katiba mpya mtukufu..
  Lakini wewe Utakumbukwa milele kwa kuruhusu mchakato katika utawala wako..
  HONGERA SANA..

  Mkuu,ukiwa unasoma Barua hii,usisahau kuwa lengo la Barua hii ni kukupa POLE..

  Ndiyo, POLE...!!
  Hakuna hasiyefahamu ni mgumu namna gani mchakato wa uteuzi wa wajumbe wa ukusanyaji wa maoni juu ya KATIBA MPYA..!Pole sana mpendwa wangu JK..

  Ila Rais nikupe POLE tena,na labda zaidi ya POLE Kwa kuingiliwa madaraka yako au KUSHURUTISWA KIFIKRA na watu flani flani au kikundi cha watu flani au watu wa sehemu flani au kanuni na taratibu flani kufanya mambo ambayo hayakuwa matakwa yako,,eti labda kwa nia ya kulinda kitu flani..
  Kwa hili nakupa POLE SANA Rais wangu..

  Sitaki Amini kama uamuzi wa kuteua Watu 15 kutoka Bara na wengine 15 kutoka Tanzania visiwani(kuunda tume ya kukusanya maoni) ni Uwamuzi uliofanywa na Rais wangu JK mwenyewe..!!
  Kuna namna hapa,, hata rais mwenyewe unajua...
  Haya siyo maamuzi yako mkuu,,kuna mambo flani,flani yamekusukuma mkuu..
  Ila Pole SANA kwa hili..
  Mimi nakumbuka sana na sidhani hata kama miezi miwili imepita tangu uteue MABALOZI ...!
  Nakumbuka mabalozi waliotokea Tanz Bara walikuwa wengi zaidi ya wale Ulioteua kutokea mkoa wa Zanz na Unguja..

  Nakumbuka,,kelele Zilisikika tokea mikoa hii miwili ya Tanzania kuwa haikutendewa haki kabisa kulinganisha na ile sehemu nyingine ya Jamuhuri yetu..

  Eti ni kweli kuwa leo umeamua kuweka nusu kwa nusu ya idadi ya watu katika ukusanyaji wa maoni ya katiba..kati ya mikoa 2 ya jamuhuri na 26 ya jamuhuri hyo ,hyo..!
  Ndiyo mana nasema utakuwa umeshindikizwa..
  Mim Rais wangu ni mchumi na ndiyo maana nina uhakika anajua hisabati..
  Hvyo hasingeweza kufanya uamuzi kama huu isipokuwa ameshindikizwa kifikra...
  Nakupa pole tena na kukuomba usikubali tena kufanya maamuzi ya Kitaifa kwa kuogopa eti kundi flani litasemaje au upande flani utalichukuliaje swala hili..
  Wako mtiifu..
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  aha ha ah kweli umempa kikwete pole uliyoitoa moyoni kabisa shinikizo hilo kama amelipokea basi ameonyesha ni jinsi gani alivyo dhaifu hana msimamo nami nampa pole raisi wangu kikwete
   
 3. z

  ziwapohazipo Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mtoa mada ulipoandika thread hii kama ni mvulana nawasiwasi na jinsia yako huenda ukawa boflo au chakula cha watu kwani kule kwetu neno magwero maana yake ni ushuzi wa ****** na kama ni msichina unatumia mfumo dume kustarehesha wenzio, kama hujui waulize wenye kazi zao rais hashurutishwi na mtu ni maamuzi na muono wake na hasa kwa kuwa inaijua katiba ya jamuhuri ya muungano vizuri wewe huielewi kwani hio fani yako kama kushurutishwa rais angefikiria kitu kimoja tu kuengeza idadi ya watumishi kutoka kule visiwani kwenye nafasi za kibalozi na taasisi zenye sura ya muungano na muhimu zaidi ni mgawano wa mapato ya muungano hizi ndizo kero kubwa za muungano katika hayo ratio ya visiwani haifiki hata asilimia 10 sasa wewe unaongea nn kwenye hili halafu ujuwe znz sie mkoa ni nchi kamili yenye bendera yake, serikali yake wimbo wake wa taifa na maamuzi yake kama ni mkoa basi tanganyika iko wapi serikali yenu uko wapi wimbo wenu wa taifa yuko wapi rais wenu fikiria kwanza kabla ya kusema nyambafuuu mmoja ujinga na umimi umekujaa tafuta historia zanzibar umekulea wewe waulize waasisi nani alietaka muungano kati ya nyerere na karume nyerere aliona mbali sana kuhusu visiwa vile akaona njia pekee ni kula rasilimali zake kupitia muungano na kupunguza nguvu alijua kama muungano ungekuwa wa serikali tatu asingeweza kufanya yale waliyoyapanga kufanya kama kweli watanzania tunataka kuprove nani alikuwa anamuonea mweziwe kwenye muungano tuweke serikali 3 halafu sote tuweke ushiriki sawa kwenye shirikisho la muungano kwa kigezo cha idadi ya watu au vyenginevyo uwone madudu yatakavyoibuka
   
 4. Entuntumuki

  Entuntumuki Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gracias!
   
 5. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hebu jamani let's be a bit serious, kuna sababu yoyote ya kutumtukana mtu kiasi hiki? eti kisa anafikiri tofauti na wewe! isitoshe mambo ya jinsia yanakujaje kwenye mada hii? watu kama wewe ndio mnaambiwa na makonda wa daladala 'hasira za nyumbani kwako usituletee hapa' siku njema kaka/dada.
   
 6. M

  Magwero JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  We mpemba/muunguja umeongea kwa Hasira sana...!
  POLE na wewe, kwani naona imefikia hatua hata wew Kijana Swafi kutoa lugha za matusi na uzalilishaji.. Hakika Umekereka,, ila sijui Asili ya Kero yako..
  1/Mim kumpa Pole Rais wangu au
  2/kuita Zanzibar na Unguja kama mikoa au
  3/.... ?

  Swala la kumpa Rais wangu Pole kama limekura basi wewe si Muungwana na Una Roho mbaya...(ili ntakusaidia kwa maombi)

  Kama UMEKERWA kwa kuwa nimeiita sehemu ya Tanzania yani Zanzibar na Unguja ni mikoa(hapa ntakupa Pole na Elimu kidogo)..
  Sikia kijana wangu, Tunaposema Tanzania katika macho ya Kimataifa basi lazima utambue kuwa Muungano wetu, wa eti nchi 2 unavunjika na kubakiwa na nchi 1 yenye mikoa mingi ikiwemo iyo unayodhania ni nchi ndani ya Muungano(zanzibar)..
  Hvyo basi lazima kuanzia leo na wew uwe Balozi mzuri kwa watu walio Pumbavu kama ulivyokuwa wewe kabla ya Elimu hii..
  KUWA hakuna NCHI inaYOitwa ZANZ au TANG 2napozungumza Juu Ya TANZANIA..

  Bali sehemu zote hizi mbili,zinazounda Jamuhuri yetu huwa kama mikoa...
  Hvyo uwelewe kuwa ninaposema Zanzibari ni mkoa na kuwa na maana sawa sawa na kusema Kigoma,Mtwara nk(ndani ya Tanganyika)..
  Hvyo Rais wangu kuteua watu 15 kutoka mikoa miwili ya Tanzania(unguja na Pemba) na kuiacha mikoa mingine zaidi ya 28 kuwa na uwakilishi wa watu 15...
  Hapa ndo natilia shaka langu kuwa Rais aliyafanya haya kuepusha kelele za watu wa mikoa ile uku akiwaacha watu wamikoa mingine wakiumia kwa ufinyu wa uwakilishi..
  Ninafurahi kwa kuwa unatikisa kichwa "juu chini,na chini juu" ishara nzuri kuwa unaelewa..
  Lamwisho sijui umri wako,,ningejua labda ningekufunza mengi juu ya Maisha..
  Jawabu la Upole utuliza gadhabu na neno la uchokozi uchochea hasira...
  Jaribu kuwa muungwana kijana,,matusi na lugha za kuzalilisha kila mtu anayo anayo(ila si busara kuyatumia)
  kuhusu jina la Magwero inaweza kuwa na maana hyo uko wete/chakechake ila uku kwetu inamaana sawa na neno "Produgal Son"
  kwani haujawahi sikia mtu anaiwa NANI...!!mbona kwenu ni swali na kwao ni Jina..
  Ntafurahi kukuona tena hapa
   
 7. z

  ziwapohazipo Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu nilikuelewa sana lkn usiupotoshwe umma kwa ufahamu wako mdogo rudi kwenye katiba yetu ile ya muungano wapi palipoandikwa kuwa unguja na pemba ni miongoni kwa mikoa ya tanzania iheshimu ile nchi kama unavyojiheshimu wewe iliyokufa ni tanganyika na sio zanzibar na kuhusu umri wangu nafikiria naweza kuwa baba ako au kaka ako wa mwanzo ndugu yangu au mwanangu tunapojadili utaifa tuwe na heshima una kila sababu ya kumpogeza rais wetu makini wa jamuhuri wa muungano lkn kwenye hili nafsi itakusuta hukumpogeza bali umemkejeli na tatizo lako hutaki kujua mambo rudi kwenye historia na kama kati ya wali watanzania wachache wanaofikiri kuwa na degree moja ni kuelimika basi ningekuomba ukarudi darasani huenda ikakusaidia na jifunze kutembea uone mambo, la mwisho nakushukuru kwa kuelewa kuwa ulifanya kosa huwezi kuita zanzibar ni mkoa na kama zanzibar ni mkoa basi na tanzania bara ni mkoa kwani tanganyika imekufa zamani sasa tatizo nn mkoa wa znz umetoa wajumbe 17 na tanganyika 17 najua hii hesabu huijui wajumbe 2 kila upande wameunda secretariet mwenyekiti bara makamo znz katibu znz naibu bara . Wewe nimekujibu mmoja unasema nimekutukana jee wewe uliwajumuisha wazanzibar wote nani katukana zaid karibu ndugu yangu mwanangu kwenye visiwa vya karafuu muulizeni pinda kuna hela zilitoka huko mbali na kuingia znz yy na wajinga fulani wa BOT wakaanza chokochoko walijibiwa nn rais kikwete
   
 8. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  SASA WEWE NDO HUELEWI.NIMERUDIA KUSOMA MARA MBILI HABARI YAKO HAKUNA HOJA ULIYOJENGA,form two bwna
   
 9. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Lugha ya matusi haisaidii kujenga hoja ndugu yangu, hata kama ulikuwa unahoja nzito ukishaweka matusi tu huwa haivutii.
  Jitahidi siku nyingine kuepuka lugha za matusi utaeleweka tu
   
Loading...