Pole sana Rais Magufuli kwa msiba wa Balozi John Kijazi

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Nimemwona Rais Magufuli kwenye ibada ya kumuaga marehemu John Kijazi.

Bila shaka yoyote, kwa mwonekano tu, Rais Magufuli ni mwenye majonzi makuu na huzuni moyoni iliyochanganyika na fikra nyingi.

Tumemlaumu na tumemsema sana Rais kuhusiana na ugonjwa huu wa corona ambao mpaka sasa kwa uhakika umeondoa na unaendelea kuondoa ndugu zetu wengi. Mimi ni miongoni mwa waliopoteza ndugu na marafiki.

Ugonjwa huu ni janga maana japo tunajua kila mmoja atakufa, na kwamba vifo vimekuwepo nyakati zote, lakini vifo vinavyotokana na corona ni vya pekee maana tunakosa kuwaaga na kuwaliia wapendwa wetu kwa namna ya uhuru ambao tungependa kuwa nao. Mama yangu alipofariki kwa maradhi tofauti, nilimuaga kwa kumshika mkono, nilimlilia kwa uhuru wote, ile ilinipa faraja mpaka leo lakini ndugu zangu waliofariki kwa corona, sikuweza hata kuyakaribia majeneza yao.

Leo mke wa Kijazi hajaweza hata kumwona mumewe akiwa kwenye safari yake ya mwisho, Rais Magufuli hajaweza kuuona mwili wa rafiki na msaidizi wake mkuu kwa uwazi.

Rais Magufuli, huenda kwa yale tuyasemayo yamekuumiza, nawe hatua ulizozichukua juu ya ugonjwa huu umetukwaza, basi wakati huu wa msiba wa John Kijazi, tuyasahau yote, tuungane kama Taifa, tushirikishane, tushauriane, na tuchukue hatua kwa pamoja kupambana na ugonjwa huu, tunaweza tusifanikiwe kwa 100% lakini umoja wetu utatupatia faraja kuu.

Rais tuongoze katika mapambano haya, na wala usiamini kuwa ni wewe tu ndiyo mwenye jibu la corona, umoja wetu na ushirikishwaji wa kila moja ndiyo mafanikio yetu. Lakini pia tukubali nchi yetu ni sehemu ya familia kubwa ya Dunia, tushirikiane na wenzetu, tusijitenge nao bali tuchangie kwenye juhudi za Dunia.

Mateso ya ugonjwa huu, vifo, na kukosekana maelewano miongoni mwetu juu ya hatua za kuchukua, kutazidisha simanzi kwa wagonjwa na wanaopoteza wapendwa wao. Rais unganisha Taifa. Hakuna ushindi katika vita vyovyote katika utengano.

Mungu mkuu uliye asili ya hekima, tujalie hekima, utupe mwanga, na utufunulie hata yale yaliyofichika ili hatua tunazozichukua zitupeleke kwenye ushindi. Pamoja nasi, uwajalie viongozi wote wa Duniani ili washikamane katika kupambana dhidi ya maradhi haya.

Maradhi haya siyo ya kwanza, yamepita magonjwa mengi, lakini Dunia iliyashinda. Ni umoja ndio uliofanya tuyashinde.

Lakini misiba hii inayotokea itukumbushe kurudi kwenye ubinadamu, yaani tujue kuwa sisi ni wanadamu, hakuna aliye binadamu zaidi. Dhuluma, hadaa na hila huzaa laana. Sisemi vifo hivi ni laana maana Dunia nzima watu wanakufa kwa corona, lakini misiba hii utukumbushe ubinadamu wetu.

Uchaguzi wa mwaka jana bado umeligawa Taifa kutokana na dhuluma, hadaa na hila. Tujutie ushetani ule, tuombe hekima ya Mungu ili Taifa letu liendelee kupokea baraka za Mungu. Tufuate maelekezo ya wanasayansi, tumwombe Mungu aweke baraka kwenye hizo jitihada. Lakini tusisahau, Mungu hasikilizi maombi ya mwenye dhambi. Uovu ule uzaao laana uliofanyika 2020 lazima tuutubie ili tupokee neema za Mungu.
 

Attachments

  • VID-20210219-WA0011.mp4
    18.7 MB
Acha kumpangia mh. Rais cha kufanya. Alishasema wazi kuwa hapangiwi na ukimpangia ndiyo unaharibu zaidi.

Tuheshimu msimamo wa rais kuhusu kutotaka kumpangia cha kufanya
 
Umeanza vizuri mwisho umeharibu hoja yako,suala la corona na uchaguzi ni wapi na wapi?, kwa nini binadamu kweye kila tatizo lazima mpate wa kulaumu?!, km umekili kuna ndugu zako corona imewala,je nani wa kulaumiwa? Wewe au magufuli?!, kwenye familia yako wewe ni rais na mkuu wa familia,ulifeli wapi?!,
 
Usione ukadhani ,fitina titi la paka halifai kwa mtindi - Medani za Andanenga Sauti ya Kiza.
 
Story yako ndeefu km nini, naomba tu nieleze, vp magu alivaa barakoa wakati wa kumuaga??

Ajue kuwa huu ugonjwa hautaki hasira, hasiufananishe na kitendo cha kutuibia kura zetu sisi watu dhaifu, hii kitu haijui mtukufu wala mtakatifu, inachapa hata raisi,

nadhan nkurunzinza alikua vizuri pia alikuwa mtu wa mazoezi lkn Mr covid hakuyajua hayo aliliwa tu kichwa chake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom