Wana JF,
Napenda kutoa pole kwa Mzee wetu Kinana Katibu Mkuu wa CCM kwa yale yaliyomkuta leo hapo bungeni. Ni ukweli usio fichika kuwa hata yeye alikuwa anachosubri ni suala la muda tu ili maovu yake yaweke hadharani kama alivyofanya Mh. Mch Msigwa leo. Biashara unayofanya Mzee sijui ni nani alikushauri urudi katika ulingo wa siasa kwa muda huu pole sana. Lakini kama uliamua kwa mapezi yako na si kwa kushauriwa na mtu yeyeote basi poa kubali matokeo. Kwa hali ya siasa hapa nchini kwa sasa bila shaka kabla hujachukua uamuzi wa kuingia kwanza jichunguze mwenyewe kabla ya kuchunguzwa otherwise matokeo yake ndo hayo.
Siasa za TZ zimefikia wakati si tena Kidumu chama cha Mapinduzi au CCM oyeee!. Wananchi wa sasa si wale wa kipindi kile mlikuwa mnafanya mnavyotaka na mambo yanakuwa shwari. CDM wanahitaji kuingia Magogoni na kila dalili zinaonekana kwa hali ya Siasa inavyokwenda sasa hivi. Kwa mfano kila chaguzi zinazofanika sasa hivi CCM imekuwa inashindwa tena kwa mbali na ni hukohuko vijijini ambako niyi kwa fikra zenu huko ndo kwenye mtaji wenu. CCM mlitegemea suala la kuwaita CDM magaidi ingeweza kuwasaidia japo kwa kupunguza kasi kubwa ya cdm kwa sasa lakn matokeo yake CDM ndo inazidi kupendwa kila kukicha.
Kwa sasa Mzee hakuna sehemu ya nchi hii utakwenda na kusimaa watu wakuelewe na kila utakapoomba wananchi wakuulize maswali UJANGILI ndo litakuwa la kwanza na hautakuwa na majibu sahihi. Na hali ilivyo kwa sasa ccm wakijaribu tu kukutoa katika nafasi hiyo ujue wamehalalisha UJANGILI wako na CCM haitakuwa salama tena. Ukiendelea na nafasi yako kwa kulazimisha ndo CCM haitasimaa mahali popote na kusikilizwa.
Nina mengi Mzee wangu lakini pole sana na hizi ndo siasa halisi. CCM mlizoeza simple politics sasa wanzenu wanafanya complicated politics. Mukama aliko anashukru kikombe hiki kilimpita na sasa anakula kuku japo si saaaana
Wasalam, Mzee Kinana.