Pole sana mama yote ni maisha

Pole sana mama yote ni maisha

fizo talent

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
2,256
Reaction score
3,890
Habari wakuu,

Nijielekeze ktk hiki kisa moja kwa moja maana mambo ni mengi halafu muda ni mchache

Baba baada ya kufiwa na mkewe alikaa alone kwa muda wa miaka miwili hapo tayari alikuwa na watoto watatu na mimi nikiwemo. Baada ya kipindi hicho cha miaka miwili akampata mama mwingine kipindi hicho watoto wote watatu bado tupo home ila mzee hakumuoa na waliishi pamoja kwa muda wa miaka minne.

Kwa kipindi chote wakati yule bi mkubwa yupo home hatujawahi kuona manyanyaso wala kutengwa wala kujikweza kwake na maisha yalikuwa safi tu japo mpaka wakati huo hakubahatika kupata mtoto.

Baada ya kipindi cha miaka miwili mzee siku hiyo alimuita kaka ambae ni wa kwanza kuzaliwa wakati huo alikuwa ameingia kwenye ndoa kama miezi minne hivi na kumwambia;najua uliishi vizuri na mama yako kabla hujaoa na mpaka sasa una familia yako ila mahusiano yapo vizuri kwako pamoja na wadogo zako ambao bado wapo nyumbani(hapa kaka alinisimulia baadae)ila mzee alimwambia kaka yeye hana furaha na anataka kumuacha mama aendelee na maisha yake kwa kuwa amekataa vitu viwili,cha kwanza hataki afunge ndoa nae na cha pili hataki kumzalia mtoto.

Kaka alishtuka sana na kwa jinsi mama alivyo mstaarabu,mpole,akamuuliza sababu ni ipi mpaka hataki hayo mambo muhimu kabisa kwake,mzee alijibu kwa uchungu hayataki hayo kwa kuwa yeye baba ni mweusi na alimwambia hayupo tayari kuolewa nae wala kumzalia mtoto sababu inaweza ikatokea akazaa mtoto ambae atafuata rangi ya baba ambae ni mweusi kwao itakuwa kama mkosi maana ktk ukoo wao hakuna ngozi nyeusi.

Kaka alistaajabu sana hata alivyokuja kunisimulia mimi sikuamini kwa jinsi mama alivyo kimatendo na tabia pia.Ila kaka alimshauri baba ampe muda waendelee kuwa pamoja huwenda akabadili maamuzi,baba akamskiliza kaka na akampa muda lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote baada ya miaka miwili mbele wakaachana sababu kuu ikiwa ni hiyo japo kaka alifanya uchunguzi wake wa kumdadisi mama na kweli akathibitisha madai ya baba ni kweli na alimwambia baba hana mamlaka ya kuingilia mapenzi yake japo amemshirikisha kwa kuwa ni mtoto ila maamuzi yoyote atakayochukua yeye yupo tayari kuyapokea na atatuelewesha sisi wadogo zake.

Baba alichukua maamuzi ya kuachana na yule mama.

Baada ya miaka minne toka walipoachana na yule mwanamke na baba kuoa mwanamke mwingine na kujipatia watoto wawili,yule mwanamke alipata jamaa mmoja ambae ni mwarabu pure na kuolewa nae,na toka alivyoolewa ana miaka ipatayo miaka mitatu tulikutana nae ktk hii sikukuu ya Eid iliyopita akiwa ktk mazingira mabaya na amekongoroka vibaya mno akiwa amebeba mtoto mdogo mgongoni.

Hakuna aliyeamini kama ni yeye ila kiuhalisia alikuwa ndie yeye baada ya salam za hapa na pale ndipo akamuuliza kilichomsibu hapo familiy yote tupo,tupo akasimulia huku akilia

Baada ya kuachana na mzee miaka kadhaa mbele ndipo akaja kumpata huyo mwarabu ambae alifunga nae ndoa,ila kilichotokea baada ya yeye kujifungua alizaa mtoto mweusi tii kitu ambacho huyo mumewe hakuwa tayari kukikubali na kusema sio mtoto wake na akamwambia kaleta mkosi ktk ukoo wao hakuna mweusi hivyo akampe baba yake na sio yeye na talaka ikafuatia.

Baba hakua na msaada mwingine na ikizingatiwa sasa hivi ana mke mwingine alichofanya ni kuzama kwenye wallet na kumpa kiasi cha elf hamsini na habari ikaishia pale pale.
 
Mpe pole sana mama yetu, mwambie wahenga walisema "Usitukane mamba kabla hujavuka mto"
 
kwahyo bi mkubwa wako alichepuka au ?
kiuhalisia na "genetic laws" alitakiwa azaliwe mtoto chotara
 
Bika shaka hawa watakua ni wale ndugu zetu waumini wa dini ileee maana wao wanawake hata wakiachika hawawezi kukituliza lazima watafute wakuaoa tena kwa mara ingine...
 
Mtoa mada kama una vijisenti kidogo msaidie huyo mama yenu ambaye aliwalea wakati wadogo na Mungu atakulipa sana. Malezi, mafunzo na uangalizi alioufanya pindi mkiwa wadogo ni makubwa sana kuliko hata ada ya Chuo kikuu na yeye aliyafanya bure tu. Ukikua utanielewa
 
Back
Top Bottom