Pole mwalimu ila hili si tatizo la walimu tu na wengine wapo

Pole mwalimu ila hili si tatizo la walimu tu na wengine wapo

Hivi hizo hasia za kiwango hicho zilitokana na nini? Kwani hiyo pochi "iliyoibiwa" ilikuwa yake? Mimi hadi nahisi huyo mwalimu aliyepoteza pochi alikuwa mpenzi wake ndio maana alikuwa na hasira hivyo.
Halafu walimu wote waliokuwepo siku ya tukio ni punguani. Walipoona mwenzao anamuadhibu mtoto kupitiliza kwa nini wasimzuie? Wangetumia hata nguvu kumnyang'anya fimbo na vitu vingine ambavyo alikuwa anatumia kumsulubu mtoto. Tatizo walifanya eti "kumheshimu" mwenzao na matokeo ndio hayo.
Halafu pochi iliyopatikana eti ndio wanaagiza bagia na juisi apewe mtoto, hivi maiti huwa zinakula na kunywa?
Umeongea point sana mkuu . Hata Mimi nilishangaa hizo hasira zilikuwa za nini!!!!

Hivi kweli mtu mzima unaweza kumpiga mtoto kama nyoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na mwalimu yule kufanya jambo kwa hasira bado hii adhabu ya kifo haifai.This is a very rude and capital punishment which won't bring back/exhume our beloved son.Wanaharakati wa haki za binadamu bado wanapaswa kuipinga kwa hoja kali zenye nguvu iondoshwe vitabuni.
 
Namkumbuka Academic teacher aliyenifundisha sekondari alikuwa anazungumza mara kwa mara tena pasi kuficha "Ualimu ni Utumwa".

Kazi ya ualimu ni wito,mwalimu amefundishwa chuoni kuwa ni MLEZI(kama mzazi) sasa majukumu ya mzazi kwa mtoto ni nini?.

Sawa mwalimu amekosea kwa kutojizuia na mihemko yake,lakini pia mwanafunzi nae amekosea.

Kazi ya ualimu ni utumwa:
-mshahara mdogo hakuna motisha/posho yoyote.
-mazingira ya kazi mabovu
-Bado tena wazazi na wanafunzi wanawadharau walimu kwa ujumla wake.
-Licha ya dharau bado tena mtu una mhukumu kifo ukijua ana stress kama zote.

KAZI GANI HII?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaposema mwanafunzi ana makosa, haujafuatilia mwenemdo mzima wa kadhia hiyo.

Ni wapi alipokosa huyo mwanafunzi?

Ukiliangalia tukio lenyewe ni kama shetani aliwasimamia kuanzia huyo mwalimu wa kike aliposahau pochi lake kwa bodaboda.

Siungi mkono kwa adhabu zote, yaani alivyoadhibu huyo mwalimu hadi kusababisha kifo na adhabu ya kifo iliyotolewa kwa huyo mwalimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mwalimu akikata rufaa hata shetani atamshangaa, mikono yake imetenda dhambi hapo alipo nafsi inamsuta ,hiyo hukumu ndio njia pekee ya kumpa amani. Akiipinga hiyo hukumu moyo wake hautapata amani milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanafunzi kakosea nini kama sio kumpokea mkoba na kuuweka kwenye office za walimu..

Mwl wa kike hakuona pochi yake iliyokua na simu, chaki, pen na urembo... moja kwa moja akamtuhumu mtoto aliyempokea kua kaiba pochi

Kumbe mwl aliisahau kwenye boda boda ile iliyo mleta shule...

Basi vikaanza viboko mtoto akakataa kwamba hajachukua... Akakaguliwa Bado mtoto hawakumkuta nayo...

Akakabidhiwa shababi mmoja mwl wa nidhamu afanye uchunguzi basi alimchapa viboko, viboko vikaisha.. akachukua kuni walizokua wameziandaa kuwapikia chakula watoto wanao fanya mtihani wa darasa la saba...

Mtoto akapigwa kichwani, kifuani baadae akazimia.. lakini bado mwl akaendelea kumpiga akiwa kazimia.. akazinduka bado akala viboko.. mtoto alilia kwa uchunguzi sanaa mwisho akafa

Muda si muda mwenye boda boda akarudi shuleni hapo na kumpa mwl simu yake kwani ilikua inaita sanaa.. yeye alipanga amkabidhi anavyo rudi shule...

HAPO KOSA LA MWANAFUNZI NI LIPI KAMA SIO WEMA WAKE WA KUMPOKEA MWL?[emoji26][emoji26]

Sent using Jamii Forums mobile app
Inauma sana aisee
Kama ni mwanao kafanyiwa hivyo waweza kuvumilia kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom