The golden
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 1,383
- 2,586
Niliposikia ile hukumu ya kifo kule Bukoba nilishituka kidogo, ila nikajipa mda wa kutosha kutafakari.
Mwalimu aliyekuwa anafundisha watoto leo amehukumiwa kifo. Masikitiko. Kazi ya ualimu imeharibu hatima ya maisha yake.
Kinachonisikitisha si hukumu hii ya kifo aliyohukumiwa , bali nasikitika kwa nini mwalimu alishindwa kuzuia hisia zake za hasira akaamua kutoa adhabu mbaya ambayo ilipelekea umauti wa yule mtoto mdogo.
Binadamu tumeubwa na hasira ,chuki ,na upendo pia. Hatuwezi kuzikataa hisia hizi. Jambo la msingi ni kujua kuzitumia hisia hizi na kuzitawala pia. Tusiruhusu hasira zikatawala maamuzi yetu maana athali zake ni mbaya mno.
Nina uhakika Mwalimu hakukusudia kumuua huyu mtoto . Tatizo ninaloliona kwa huyu mwalimu ni kuwa alishindwa kuzuia hasira zake na matokea yake ni hayo.
Tatizo hili la kushindwa kutawala hasira haliko kwa walimu peke yao ,hata wale tuliowapa kazi ya kulinda usalama wetu wana tatizo hili. Naomba niwakumbushe wote linapokuja swala la sheria wewe mwenyewe binafsi utawajibika. Wale waliokutuma ukapige watu hutawaona siku ya hukumu yako. Badilikeni .
Tatizo hili ni la kitabia. Watu weusi tuna hulka ya kunyanyasana ,kuoneana na kutesana. Na hii inaonekana katika nyanja nyingi za maisha yetu ,Leo sitafafanua sana.
FUNZO
Kila tukio huacha funzo. Walimu na wale wanaolinda usalama lazima wawe makini sana. Dawa ya kuepuka matatizo kama haya ni kufuata sheria za nchi tu. Someni sheria inasemaje kuhusu viboko . Toeni adhabu kwa mjibu wa sheria.
NB ; Pole tena mwalimu, bado iko nafasi ya kukata rufaa.
Sent using Jamii Forums mobile app