Pole mheshimiwa lakini...

alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
5,709
12,226
Kwanza napenda kukupa pole mheshimiwa TUNDU LISSU kwa magumu unayopitia,na nakuombea kwa mungu upone haraka na kurejea kwenye majukumu ya kulijenga Taifa.

Lakini nimekuwa nikipata na shaka kupitia kauli zako ukiwa hospitali kuashiria bado una ari ya kuendeleza mapambano.. uncle yaliyokupata makubwa mnoo,sababu ya yote hayo ni siasa . hili liko wazi.

Nadhani huu si muda muafaka wa kuwa na muhemuko wa kutamka hili na lile,nadhani ungenyamaza kusubiri afya yako ikae sawa,chukua muda mrefu kidogo kupotea,baada ya hapo uitishe mkutano wa waandishi kujivua nyadhifa zote za kisiasa na kitaaluma kwa masilahi ya afya na familia yako. Achana na habari sijui ya kutetea watanzania,kila mtu apambane na hali yake.

Mungu amekuepusha na kifo ili ujifunze kitu.unlce watu wanakushabikia tu lakini hawakupendi, bwawa la siasa sasa hivi limeingia luba ,huwezi ogelea ukawa salama, yule mzee yuko frontline hana masihara.imagine wangekumwaga ubongo pale dodoma,aunt na wapwa zangu wangeumia zaidi,

Mbona yule muhenga aliachana na siasa anajilia papuchi huko mashariki ya mbali ,nchi hii si salama kwa watu kama wewe kwa sasa,nahofia wale watu watarudi tena usipokubali matokeo,kwasababu huwezi jua kama wamepanga kukuacha au kukumalizia,wamekuharibu sana uncle na marisasi mie roho inaniuma sana mjomba.

Mbona babu mabadiliko yuko kimya? Unadhani hana akili?,au unataka uitwe shujaaa? Mambo hayo waachie wahenga kina mkwawa na isike na milambo.mjomba watu wanakupamba wàkati we unaumia,acha hizo mambo.

Ukifa na lako halipo.yupo wapi mzee wa kasi na viwango? Amekwenda..tumemsahau,mateso na kumbukumbu hubaki kwa waliompenda sio hawa mashabiki wa siasa, vp shangazi yuko tayari uende kwa ajiri ya watanzania utakaowaacha wakifurahi na familia zao huku wanao wakiwa wapweke?

Kila la kheri mjomba mungu akupe wepesi!
 
Atulie au asitulie.......siku yake kama haijafika, hakuna wa kumuua. Kukaa kimya sio jibu la yeye kuachwa na watesi wake.
 
Nelson Mandela (RIP) naye alipewa ushauri kama unaompa kaka wa Taifa letu. Kama Madiba angekunali Afrika ya Kusini huenda mpaka sasa ingekuwa gizani. Alikataa, South Africa ikapona.

Lissu tinakuombea sana upone urudi uwanjani, mapambano bado yanaendelea nyie endeleeni kuweweseka.
 
Back
Top Bottom