Poland wamedungua Drones za Urusi zilizoingia kwenye anga yake kimakosa.
Hawa jamaa huu ujasiri wa kumvimbia Russia wanatoa wapi?
View attachment 3468965
Polish huwa ni watu wabishi, hata Soviet Union walipata shida Papa alipochaguliwa John Paul II raia wa Poland, mchakamchaka waliupata maana walizoea kuonea Wakristo na ndio sababu walimpiga risasi bahati nzuri alipona.
Poland ilipigana na Ukraine mwaka 1918 ikashinda, mwaka 1919 ikachokozwa na USSR ya Vladimir Lenin ambayo iliiteka Ukraine kuiunganisha kwenye Soviet Union. Poland ikawafuata kuanzia Kiev ikaenda mpaka Belarus ikawapiga Warusi. Kasome Miracle on the Vistula ambapo dunia ilidhani Poland watapigwa kumbe wapi.
Wakasaini mkataba wa kutambua mpaka ambao Poland walitaka ingawa pia hawakuwa wanataka USSR ikue iunganishe Belarus na Ukraine (waliona changamoto za baadae).
Mwaka 1939 Hitler aliivamia Austria peke yake, Ufaransa peke yake, Belgium peke yake ila kwa Poland aliomba msaada wa USSR nusu Ujerumani ikaivamia na nusu USSR ikaivamia. Ila ingekuwa ni Poland avamiwe na USSR peke yake au Nazi Germany peke yake wangepotezewa sana muda ingawa wangeshinda. Wasovieti walipoteka nusu yao wakawinda kila anayevaa miwani (that time almost kila anayevaa miwani alisoma sana maana walikuwa wanasoma kwenye low light usiku wanapata madhara ya macho, kwahiyo kafika chuo), wakaua wanajeshi, maofisa usalama na watumishi wa umma. Katyn Massacre Wasovieti waliua Wapolish over 20,000. Baadhi walitoroka mmojawapo ni Marian Rejewski aliyegundua njia ya ku-decode Enigma machine vita ile. Mwingine ni General Stanislaw Sosabowski aliongoza majeshi ya Poland yaliyofanikiwa kutoroka kupigana kutokea Uingereza kukomboa nchi yao, alishiriki Operation Market Garden.
Turudi 1939, upande wa Ujerumani walianza kuvamia Danzig kamji ka pwani kanakojitegemea kiutawala sio mamlaka kamili ya Poland ila hiyo vita Polish walivyoivaa utadhani umevamiwa mji mkuu. Ilizuka battle of Westerplatte, Ujerumani ilikuja na ndege 60, melivita mbili na wanajeshi zaidi ya 3,000 ikatumia wiki kupigana na wanajeshi chini ya 300 wa Poland wasio na ndege wala melivita na hawana supply.
Kila wakitumia kitu kinapungua idadi, kila anayejeruhiwa au kufa anapunguza idadi ya wapiganaji, huwezi enda hospitali, huwezi letewa chakula wala dawa, walijichimbia wiki nzima wanapigana na hapo command kutoka makao makuu imekatika wanapigana kichwakichwa.
Na hapo walipigana na ile Ujerumani ya mwanzoni kabisa ambayo ina kila kitu na ina jeshi bora zaidi duniani.
Poland sio watu wazembe vitani hata kidogo, alafu hawatishiwi. Na miaka hii ya 2020s wana massive rearmament wanaunda silaha, kununua kutoka South Korea na Marekani na washirika wengine. Na wameongeza idadi ya active troops kwa sasa ndio nchi ya NATO inayotumia GDP kubwa jeshini.
Sababu kwanini wako hivi? Kipindi ni wanyonge walionewa kila jirani alikuwa mkorofi wakaipoteza Fisrt Polish Republic. Poland mwaka 1025 walikuwa na Ufalme na jina lao hili, baada ya hapo uvamizi, kuungana, kutengana vilifuata.