Sikwangalasyene
Member
- Jul 3, 2018
- 76
- 130
Tukubali au tukatae, hakuna mafanikio ambayo serikali inaweza kujinasibu kuwa yamefikiwa. Mafanikio hayawezi kuwa kujenga barabara tu, barabara hujengwa daima (Since independence barabara zinajengwa) kununua ndege, kujenga barabara ili hali hali za wakulima zinatia simanzi. Masoko ya mazao ya wakulima yamevurugwa, wafanyakazi hawakopesheki kwa kuwa hawajaongezewa mishahara kwa miaka mitatu mfululizo hivyo kutokidhi vigezo vya makato, biashara zimevurugwa, kodi inakusanywa kwa vitisho, biashara kama enzi za ukoloni, hakuna uwazi kwenye manunuzi (Ndege zimenunuliwa pasipo kufuata taratibu), kuna double standard kwenye kuwajibisha watumishi (Upendeleo), vyombo vya habari havipo huru tena, wananchi wamenyimwa haki ya mijadala ya wazi, serikali haipo radhi kukosolewa, kila mwenye mamlaka ana kauli ya mwisho (Wakuu wa Wilaya na Mikoa wamekuwa kero), upotoshaji kwenye hali ya uchumi wa nchi ni mkubwa, 1.5 trillion hazina maelezo (Kuna wizi na ufisadi mkubwa kuwahi kutokea), polisi wanafanya kazi za CCM na si kwa maslahi ya wananchi, usalama wa viongozi ni kipaumbele na si usalama wa nchi. Hata kama wapo wanaounga mkono utawala huu, lakini ukweli utabaki pale pale na ni muhimu Mh. Rais atambue kuwa wakati haudanganyi (Every thing is and will be put open soon).
Mh. Rais naiona kesho yako ukiwa pekee yako kwani wanokuzunguka wanachumia matumbo BUT for real umeharibu. Takasa mikono yako kabla hakujacha usipotoshwe na Malaika wa NURU. Ninaamini Mungu anaongea na wewe lakini unapuuza! Yoshua 3:10 " Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu ..........................". Mh. Rais, Mungu wa Watanzania ndiye Mungu wa kweli But Nina shaka na Mungu wako, hasa unayemuomba kutekeleza unayoyafanya!
I stand to be corrected! But that is!