Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Naomba nieleze jambo moja. Hii ni taarifa ya Mwaka ya Kamati ya POAC. Ukiona hapo utaona ni mwaka wa fedha unaoishia June 30,2009! Taarifa ya CAG inayoishia june 2010 inawasilishwa Bungeni siku ya jumanne na baada ya hapo ndio Kamati zitapewa na Spika ili kushughulikia.
Kwa hiyo katika Taarifa hii hutakuta taarifa ya CAG maana imeshatoka na unaweza kuipata katika tovuti ya national audit office. POAC inatoa taarifa ya kazi kufuatia taarifa ya mwaka 2009.
Kazi ya kamati ni kuhoji na kutoa maelekezo, maagizo na mapendekezo kufuatia taarifa ya CAG. Kwa wale wanaotaka CAG report inayoendana na taarifa ya POAC waende kwenye tovuti ya CAG.
Kila la kheri
Ahsante Mzee
Ila naomba kama una muda unijibu swali hapo juu, kuwa 'kwa kukagua mashirika kwa kutegemea ripoti ya 2009, haimaanishi kuwa taarifa yenu inakuwa too outdated?