Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,071
Hatimaye kila kitendawili cha hatma ya kisiasa ya Majaliwa katika nafasi ya waziri mkuu kimehitimishwa rasmi leo baada ya Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa 'masikitiko' makubwa kutangaza rasmi kuwa hatachukua tena fomu za kugombea ubunge wa jimbo la Ruangwa, na hivyo kufuta ndoto zote za kuendelea kuwa waziri mkuu au hata kuwa sehemu ya serikali ijayo ya CCM.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo huku akionekana usoni kama mtu aliyekosa furaha fulani. Binafsi ninadhani masikitiko hayo hayajatokana na kuachia kiti hicho cha ubunge bali fedheha aliyoipata au atakayoipa kwa huo uamuzi wake sasa kwa kuwa wiki moja iliyopita tu, akiwa bungeni akitoa hotuba yake ya mwisho bungeni kwa furaha, kujiamini, bashasha na shangwe kuu alitangaza rasmi kuwa angechukua tena fomu za CCM ili kugombea ubunge wa Ruangwa kwa kipindi kingine.
Wadadisi wengi wanajua na kusema, kwa kipindi kirefu mnoo tangu kuingia kwa Rais Samia, Mheshimiwa Majaliwa alikuwa kwenye shinikizwa kubwa la kutakiwa kuachia kiti cha uwaziri mkuu, lakini kimtindo akakaza, na maafikiano yakawa ni kutua taratibu kwa kuhitimisha safari yake mwisho wa awamu hii na baada hapo apumzike kisiasa.
Soma Pia: Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge
Sasa hili tukio la wiki iliyopita la Mheshimiwa Majaliwa kutangaza kugombea tena Ubunge (ikiwa na maana anautaka tena uwaziri Mkuu) lilitushtua wengine, lakini hili tukio la leo la kutangaziwa tena kuwa hata gombea limetushtua zaidi wengi.
Swali kuu:
Je, Mheshimiwa waziri mkuu Kassim Majaliwa hakujua kuwa hatakiwi tena kugombea au alikuwa anatikisa kiberiti kuona kama kimejaa?