Sina hakika kama wabunge wote wa CDM (ukiondoa Shibuda) wanazipinga hizi posho, lakini kama ni kweli kwa umoja wao wanazipinga nawapongeza na waendelee kuzipinga. kutokana na uwingi wa wa wabunge wa CCM ni wazi pingamizi hili litashindwa na wabunge wataendelea kupokea posho kama kawaida labda kwa wale watakaoamua kususa kama Mh. Zitto alivyofanya huko nyuma.
Mtazamo wangu ni kwamba, kama pingamizi hili halitasikilizwa, na hatimaye posho kupitishwa, na kama kweli wabunge wa CDM kwa ujumla wao (47)hawazitaki hizi posho (kitu ambacho siamini) nawashauri wazichukue na wazifungulie account huko CDM makao makuu na zipangiwe shughuli za maendeleo kwenye majimbo yanayowakilishwa na CDM pamoja na maeneo mengine yanayohitaji kujiimarisha kisiasa.
Sisi wananchi kwenye majimbo yenu tuna shida nyingi sana, hatuna maji, hatuna zahanati, watoto hawana madawati, wengine hawana vyoo, hawana madarasa ya kutosha, pelekeni hizo pesa kwenye maeneo hayo nasi tutawaona kweli mlizikataa posho lakini mkazirudisha kwetu kwa njia nyingine. (nimejaribu kuzipigia hesabu ni karibu milioni tisini kwa kikao cha siku kumi kwa wabunge 48 wa CDM).
Mkizisusa, hao majambazi kamwe hawatazipeleka kwenye mfuko wa maendeleo kama mnavyotaka, watazitafuna mchana kweupe.