PM aagiza uwezeshaji watati wa michikichi

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
500
1550605822897.png

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Kilimo iwawezeshe watafiti katika kituo cha utafiti cha zao la michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, ili waongeze kasi ya uzalishaji wa mbegu bora za zao hilo

Alisema serikali imeamua kuongeza nguvu kwenye michikichi, hivyo Wizara ya Kilimo hainabudi kukiwezesha kituo hicho kwa lengo la kuzalisha mbegu bora zitakazosambazwa kwa wakulima. Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo jana alipotembelea kituo cha Kihinga kwa ajili ya kukagua shughuli za uzalishaji wa mbegu za michikichi, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. Alisema serikali imeamua kulifufua zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, ambapo kwa mwaka inatumia zaidi ya Sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.

“Wizara ya Kilimo iwawezeshe watu wa utafiti ili waendelee na shughuli hiyo kwa kasi, iwaongeze watumishi kituoni hapa na ongezeni nguvu kwenye zao la michikichi kama yalivyofanya mataifa mengine ya Costa Rica na Malaysia.”

nguvu ya uzalishaji wa mbegu bora, ili wafikie malengo aliwashauri washirikiane na taasisi binafsi zinazozalisha mbegu. Pia, Waziri Mkuu alisema Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga, kiendelee kutoa elimu na Wizara ya Kilimo ijenge majengo yake inayoyahitaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za utafiti. Mratibu wa Utafiti wa Kilimo kwa mikoa ya Tabora na Kigoma, Dk. Filson Kagimbo, alisema michikichi iliyopo sasa ina uwezo wa kuzalisha tani 1.6 ya mawese kwa hekta moja ambao kidogo na hauna tija.

Alisema mbegu wanazozizalisha zinalenga kumuongeza tija mkulima kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani nne kwa hekta, pia wanaendelea kuangalia vinasaba vya mbegu vilivyopo ili wazalishe mbegu bora zaidi. “Tutakusanya vinasaba vyote vya mbegu tulivyonavyo na kuvitathmini na kuona uwezo wake na ikibidi tutaagiza kutoka nje ya nchi ili kuboresha zaidi.” Miche ya michikichi inachukua muda wa miezi 18 kutoka hatua ya uchavushaji hadi kusambazwa kwa wakulima.

Baada ya kumaliza shughuli ya ukaguaji wa uzalishaji wa mbegu kituoni hapo, Majaliwa alikagua shamba la michikichi la Gereza la Kwitanga lenye ukubwa wa ekari 400 na kupanda mche kama ishara ya uzinduzi wa upandaji wa miche bora shambani hapo. Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu katika zao hilo na inategemea taasisi zake mbili za Jeshi la Magereza (Kwitanga) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT-Bulombora), ambazo zina mashamba makubwa ya michikichi.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliagiza elimu kuhusu kilimo cha michikichi kuanzia hatua za awali hadi uzalishaji wa mafuta itolewe mashuleni ili wanafunzi waanze kupata ulewa na ifikishwe hadi kwa wananchi.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
1,602
2,000
View attachment 1026805

Kilimo cha chikichi kinataka moyo wa kujitolea( uzalendo), huwezi linganisha na mtu anaepanda parachichi, miwa, kahawa, machungw nk.mpaka unapata mafuta mzunguko ni mkubw.Machingw mteja anakuja kuvuna shambani, chikichi unavuna mwenyew unakamua mafuta ndio mteja anakuja.Chikichi ni kilimo cha uzalendo. Mimi ni mzawa wa kigoma na nimefanya analytical study ya zao la chikichi ni 'shida'!, İwapo tutaamua kuwekeza kwa kiwango kikubw sana bila kuwepo viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali za chikichi na kutegemea mafuta tu as a byproduct bei itakuwa chini sana(chini ya 1000) ambapo sasa hivi ipo 1000 -1500 kwa lita. Hivyo suala si kuzalisha mawese kwa wingi suala ni viwanda vya product za mawese ikiwa mazulia, chakula cha kuku,urembo, engine fuel, food products kama chokoleti nk.Kwa kigoma mtu ukiwekeza katika ufugaji wa samaki itakulipa zaidi kuliko mawese kwa sasa!. Shime wanakigoma na watanzania tupande chikichi ila tutafute masoko wenyewe siku chikichi zinazaa Pm Majaliw atakuwa amestaafu.İkumbukwe chikichi inakubali kigoma, morogoro, Katavi, Pwani, Tabora(urambo), Mbeya na Tanga, tusikalili kigoma tu, tupanue kilimo nchi nzima.Vilevile Kigoma zinamea kokoa, Nazi korosho, kahawa, ndizi matunda nk tusikariri Kigoma ni ya chikichi tu tangu enzi za mababu hali hakuna tija yeyote katika zao hilo.Serikali kama imedhamilia kwelii ifanye kwa vitendo sio siasa.
Niishie hapa nikipata muda nitaleta my 'Analytical study' ya zao hili na jinsi gani tunaweza liboresha hasa wazaw wa kigoma.
 
DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,577

Hiyo analytical study mbona hujaileta. Je Kwa Eka moja wastani mtu anaweza kuvuna kiasi gani. Leta analytical study watu wajifunze kuanzia kupanda mpaka kuvuna
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom