last man standing
Member
- Apr 3, 2012
- 79
- 13
Nilikuwa naactivate window 7, wakati wa kuirestart ndo tatizo limeanzia hapo, inawaka inazima, kuwaka kwake inaishia kwenye neno ACER then inazima, sijui ina matatizo gani wakuuu, plz naomba mawazo yenu.
Mkuu, key ni original au magumashi? ulikuwa ume-reinstall windows?
Yah, window nilikuwa tayari nimeinstall, na nimeitumia karibia mwezi mzima, leo ndo nikawa naiactivate, kwa kutumia ile software ya window 7 activator, na nimekuwa nikiitumia mara kwa mara haiajawahi kuleta matatizo, ni leo tu mkuu ndo imenibumia.
Ulitakiwa ui-activate siku ile ile ulipomaliza tu ku-install windows, mwezi mmoja baadaye itakuwa vigumu kwakuwa microsoft walishaweka mambo yao humo bila wewe kujuwa, kwahiyo hiyo windows 7 activator muda huu itasomeka kama kirusi kikali na pc kitu ambacho si kweli.
Piga windows upya na ui-activate hapo hapo, kisha kumbuka ku-turn off automatic updates (kumbuka ku-update antivirus kila mara).
yah, nilikuwa na idea hiyo hiyo, ila tatizo linakuja wapi? nimeweka cd ya window, stillinafanya vile vile, nakosa option ya kureboot ili niweze kuinstall, unaweza ukanisaidia alternative way ya kuinstall?
Hata baada ya kuinstall upya kwa kutumia CD?. Bado inajizima? cheki RAM au Processor, badili RAM nyingine uone(kama unayo ya akiba), je feni inatangulia kuzima kabla ya machine kujizima?
Okey, asante mkuu, ntakupa feedback ngoja nijaribu hizo options.