Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Nimerudi!
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimeona clip ya video ikimuonesha Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowasa akimtaka Rais kupeleka chakula cha msaada kwa waathirika waliokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha kwa zaidi ya wiki mbili mfululizo. Hata hivyo, Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli ameshatoa msimamo wake kuhusu hili suala la misaada. Rais hakuahidi wala kupeleka chakula tulipokumbwa na Ukame. Na sasa hawezi kufanya hivyo tulipokumbwa na mafuriko.
Akijitutumua baada ya Rais kutoa msimamo wa kutopeleka chakula cha msaada, Edward Lowasa akiwa mbele ya madhabahu ya kanisa la KKKT Bukoba Mjini Jumapili ya tarehe 15 Januari 2017, alisema kuwa CHADEMA watapeleka chakula cha msaada kwa waathirika wa ukame ili kuonesha kuwa Mr President is wrong.
Wananchi wa Bukoba wangali na matumaini ya kupata chakula cha msaada toka kwa CHADEMA kutokana na ukame, mafuriko hayooo yawakumba. Lowasa anajitokeza tena kwenye media safari hii akishindwa kutoa ahadi ya kuwapelekea chakula kutokana na aibu aliyopata kwa kushindwa kutimiza ahadi ya awali. Hapa ndipo ninapoona tofauti ya Rais Magufuli na Edward Lowasa. Watanzania hatujajuta kumchagua Magufuli. Ukisikia anaahidi basi anatenda. Kama hana uwezo ama dhamira ya kutenda haahidi.
Lowasa ni bingwa wa kuahidi lakini ni Ziro katika kutenda.