Please Kikwete, just resign

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Uliutaka urais na ukaupata.

Hakuna heshima nyingine tena utakayoipata zaidi ya hii uliyoipata ya kuwa rais wa taifa letu. Nakusihi kama kweli unaipenda nchi yetu achia madaraka ili mwingine nae ajaribu. Bwana mkubwa, ukiendelea kwa mtindo wako wa uongozi ulio nao hata vitukuu vyako vitaona aibu kuhusishwa na wewe. Fanya uamuzi wa kishujaa na taifa zima litakusifu.

JIUZULU NA JENGA MAZINGIRA YA KUACHIA MADARAKA KWA HESHIMA
 
Sioni kama unamtendea haki Rais wetu. ni lazima utoe sababu madhubuti na ushahidi ili hoja yako isionekane kama ni fitina na majungu tu. Sioni sababu ya kujiuzulu kwake labda tujuze zaidi kwa hoja sio fitina fitina tu
 
Hakuna fitina wala majungu hapa. Ukweli unaonekana kwa kila mtu anaetaka kuuona Hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha. Kikwete nchi imemshinda, hana uwezo wa kuongoza na hii si siri hata kidogo.
 
Mtoboasiri, nini maana ya uongozi?. Ni rahisi sana kuandika, kusema na kulalamika, lakini kile kiti si mchezo ndugu yangu. Kuongoza watu zaidi ya millioni 40 si kazi ndogo hata kidogo?. Tungetoa mawazo nini kifanyike pale tunapoona kumefanyika makosa ingesaidia zaidi kuliko kutoa kashfa. Tuna uhuru wa kusema ama kuandika mawazo yetu hasa katika kipindi hiki cha JK. Ni vyema kutumia nafasi hii vizuri.
 
Sioni kama unamtendea haki Rais wetu. ni lazima utoe sababu madhubuti na ushahidi ili hoja yako isionekane kama ni fitina na majungu tu. Sioni sababu ya kujiuzulu kwake labda tujuze zaidi kwa hoja sio fitina fitina tu
Acha ujinga wewe, ina maana huu upupu wote ambao unafanywa na serikali wewe huoni mpaka useme kwamba atoe maelezo,unalala na giza na ufisadi wa mabilioni unafanyika hilo huoni???au maelezo gani unataka upewe???
 
Kidatu ndugu yangu, Kikwete kama mtu sina shida nae na wala simchukii hata kidogo.

Umekiri mwenyewe kuwa kuongoza watu million 40 si kazi ndogo. Kwa maana hiyo unahitajika umakini. Lakini Kikwete amethibitisha kuwa si kiongozi makini hata kidogo. Hebu jiulize, vitu vidogo vidogo kama kupunguza tu matumizi yasiyo na tija kutokana ukubwa wa baraza la mawaziri, magari ya kifahari na posho hawezi kuamua ataweza kufanya maamuzi gani yanayoashiria ubunifu? Basi angalau aanze na hayo ambayo ni rahisi, anaona ugumu gani?
 
Nchi inaongozwa na watu wasiosoma ndio maana inakuwa haina mbele wala nyuma......Mkuu wa kaya sasa hivi anachojua ni kusafiri tu kuhudhuria mambo yasiyomuhusu na ku waste time for nothing.
 
Considering Dr. H. Mwinyi and Bill Ngereja haven't resigned, I hope we are not squeezing a stone to get milk!
 
Sioni kama unamtendea haki Rais wetu. ni lazima utoe sababu madhubuti na ushahidi ili hoja yako isionekane kama ni fitina na majungu tu. Sioni sababu ya kujiuzulu kwake labda tujuze zaidi kwa hoja sio fitina fitina tu
Ni ushahidi gani usioujua unataka upewe kuwa rais ameshindwa kazi.
 
Mtoboasiri, nini maana ya uongozi?. Ni rahisi sana kuandika, kusema na kulalamika, lakini kile kiti si mchezo ndugu yangu. Kuongoza watu zaidi ya millioni 40 si kazi ndogo hata kidogo?. Tungetoa mawazo nini kifanyike pale tunapoona kumefanyika makosa ingesaidia zaidi kuliko kutoa kashfa. Tuna uhuru wa kusema ama kuandika mawazo yetu hasa katika kipindi hiki cha JK. Ni vyema kutumia nafasi hii vizuri.
Unataka tumwambie nini kifanyike kwani wakati anakimbilia ikulu hakujua mwanzo anakwenda kufanya nini.
 
Kama kwa kweli aliomba nafasi ya kutuongoza tukampa hiyo nafasi lakini uongozi wenyewe ndo huu wa kutupeleka gizani na kutuweka rehani kwenye mikono ya mafisadi, basi ni afadhali aachie ngazi.
 
Uliutaka urais na ukaupata
Hakuna heshima nyingine tena utakayoipata zaidi ya hii uliyoipata ya kuwa rais wa taifa letu. Nakusihi kama kweli unaipenda nchi yetu achia madaraka ili mwingine nae ajaribu. Bwana mkubwa, ukiendelea kwa mtindo wako wa uongozi ulio nao hata vitukuu vyako vitaona auburn kuhusishwa na wewe. Fanya uamuzi wa kishujaa na taifa zima litakusifu. JIUZULU NA JENGA MAZINGIRA YA KUACHIA MADARAKA KWA HESHIMA
ajiuzuru ushike wewe nchi? acha upumbavu kijana. hii ndio faida ya kuingia JF baada ya bia za harusi.
 
ajiuzuru ushike wewe nchi? acha upumbavu kijana. hii ndio faida ya kuingia JF baada ya bia za harusi.

Hivi unakijua ukisemacho au unakurupuka tu?
soma vizuri maelezo yake kijana...amesema anae weza inaweza kua hata wewe tutakupa tukiamini utaweza sawa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom