Platnum Credit wanidhulumu

Platnum Credit wanidhulumu

Hahaaa never ever mkuu. Wale jamaa ni wezi sana. Bank zote za aina yao siwezi kopa. Platnum, Maboto, sijui faidika, nufaika wote hao ni wezi wakubwa
Kweli kabisa wale ni majambazi

Ova
 
Hahaaa never ever mkuu. Wale jamaa ni wezi sana. Bank zote za aina yao siwezi kopa. Platnum, Maboto, sijui faidika, nufaika wote hao ni wezi wakubwa

Hizi takataka wanawaumiza sana ndugu zetu na waalimu wakiwemo!
 
kuna hatua uliruka wakati unataka kuclear deni lako ndio maana umepata changamoto nenda makao makuu yao mtafute mtu anaitwa juliasi atakusaidia niliwahi kuwa na changamoto kama hiyo yako iliisha lakini
 
Wakuu salaam.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Ilikuwa mwezi wa nne mwaka huu nilipata dharura ya kifedha; ni shida ya haraka ya fedha so nikaona niende kwa hawa jamaa wanajiita Platnum Credit. Wao wanatoa mkopo ndani ya muda mfupi sana ila riba yao ni kali sana. So mi nikawaambia nahitaji mkopo ( ni kama laki sita hivi) ila baada ya miezi mitatu nitalipa hela yenu yote ili nisitishe makato kwenye salary yangu.

Hawa jamaa wana riba kubwa sana yaani fikiria hiyo laki sita niliyokopa inatakiwa nilipe milioni tatu kwa muda wa miaka nane. So tukakubaliana baada ya miezi mitatu nitakuja ku clear deni ili kuachana ni hizo riba( coz ukilipa saizi unalipa ile ile uliyokopa).

Sasa tangu mwezi wa tisa nawadai wanipe balance ya deni langu ili niwalipe, hawataki; mbele ya kutimiza mashati yao waliyonipa like kuandika barua ya kuomba kusitisha deni na kulipia elfu kumi lkn mpaka leo jamaa hawataki kunipa balance yangu.

Mpaka nimekata tamaa jamaa ni kama hawataki kuwaachia watu waliokopa kwao. Sasa nimekuja kwenu kuomba ushauri na mwongozo nifanye nini ili nipate balance yangu niwalipe nimalizane nao, kuna muda nawaza niende polisi maybe nitapata msaada. Lakini kabla ya kufanya yote hayo naombeni ushauri wenu nipite njia gani ili niweze kufanikiwa. Maana naona kwa njia ya amani imeshindikana. KARIBUNI SANA.
Hiyo laki 6 ni bora ungekopa kwa mtu
 
Nenda kwa afisa Utumishi wako wataandikiwa barua waje na wewe uwe na vielelezo vyote baada ya hapo ni mahakamani watalipa hela yote walio kukata ila kama uli top kesi nyingine hiyo
Naunga hoja
 
Kazi ya benki kuu ni Nini hizo tasis za mafisadi zinaachiwa ziwaibie wananchi kwa mikataba ya kilaghai

Nani wa kuigusa mfano bayport wakati wamiliki wana vinasaba na wastaafu wa magogoni!
 
BOT Kuna kitengo cha malalamiko dhidi ya taasisi za kifedha. Ila Hao Jamaal ni matapeli mno
 
Kwa platinum sishauri akakope. Nilikopa 3m nikaja kurudisha 6m. Yaani kwa kifupi ni matapeli wakubwa
 
Back
Top Bottom