Platnum Credit wanidhulumu

Abie

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
261
474
Wakuu salaam.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Ilikuwa mwezi wa nne mwaka huu nilipata dharura ya kifedha; ni shida ya haraka ya fedha so nikaona niende kwa hawa jamaa wanajiita Platnum Credit. Wao wanatoa mkopo ndani ya muda mfupi sana ila riba yao ni kali sana. So mi nikawaambia nahitaji mkopo ( ni kama laki sita hivi) ila baada ya miezi mitatu nitalipa hela yenu yote ili nisitishe makato kwenye salary yangu.

Hawa jamaa wana riba kubwa sana yaani fikiria hiyo laki sita niliyokopa inatakiwa nilipe milioni tatu kwa muda wa miaka nane. So tukakubaliana baada ya miezi mitatu nitakuja ku clear deni ili kuachana ni hizo riba( coz ukilipa saizi unalipa ile ile uliyokopa).

Sasa tangu mwezi wa tisa nawadai wanipe balance ya deni langu ili niwalipe, hawataki; mbele ya kutimiza mashati yao waliyonipa like kuandika barua ya kuomba kusitisha deni na kulipia elfu kumi lkn mpaka leo jamaa hawataki kunipa balance yangu.

Mpaka nimekata tamaa jamaa ni kama hawataki kuwaachia watu waliokopa kwao. Sasa nimekuja kwenu kuomba ushauri na mwongozo nifanye nini ili nipate balance yangu niwalipe nimalizane nao, kuna muda nawaza niende polisi maybe nitapata msaada. Lakini kabla ya kufanya yote hayo naombeni ushauri wenu nipite njia gani ili niweze kufanikiwa. Maana naona kwa njia ya amani imeshindikana. KARIBUNI SANA.
 
Hizi kampuni ni za kuogopa sana zina magumashi mengi ila watu wanashindwa kuzikwepa kwa kuwa wanatoa mkopo kwa muda mfupi sana bila milolongo mingi.

Tatizo linakuja kwenye mifumo ya ulipaji mikopo riba kubwa sana na ukitaka umalize deni haraka ili upunguze hawataki.

Hizi kampuni kwa sasa zinaitwa NYONYA DAMU....
 
Wakuu salaam. Niende moja kwa moja kwenye mada. Ilikuwa mwezi wa nne mwaka huu nilipata dharura ya kifedha; ni shida ya haraka ya fedha so nikaona niende kwa hawa jamaa wanajiita Platnum Credit...
Wapeleke TAKUKURU

Wanakupa chapu

Sio Hizi vikampuni za mikopo .

Hata Mabank makubwa nao wanamambo Yaoo

Hawakubali kumpoteza Mteja hivi ivi
 
Kuna thread kama hii nadhani ya 2018 hapo. Jamaa alienda akawatembezea ngumi za kutosha, kesi ikaisha pale pale. Ukienda Polisi utaishia kuwapa Polisi pesa Kisha watakwambia hawahusiki na mambo ya madai.

Ushauri wangu, nenda kapige mkwara mzito saaaaana sana, yaani kafanye valangati la Maana.

Bayport walimsumbua Sister Aisee, Ofisi zao zilikua pale Moroca jirani na jengo la Airtel sasa, tulikusanyana wanaume kama watano na Dada tuko nae hahahaha Ile issue waliifuta ghafla.
 
Nenda kwa afisa Utumishi wako wataandikiwa barua waje Na ww uwe na vielelezo vyote baada ya hapo ni mahakaman watalipa hela yote walio kukata ila kama uli top kesi nyingine hiyo
Mkuu Ni mbaya sana kukimbilia kucoment bila kusoma na kuelewa hoja,hebu soma hoja kwa umakini then ulinganishe na ulichoandika hapa
 
Back
Top Bottom