Plata O Plomo: Ulimwengu wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja[ Pablo Escobar]

By KINGO SR:

Kingo inversion



Marafiki zake wa karibu walipenda kumuita El Patron(The Boss) au El Zar de la Cocaina(The Tsar of Cocaine) lakini alipozaliwa mnamo tarehe 1 Disemba 1949 wazazi wake walimuita Pablo Emilio Escobar Gaviria au kwa kifupi Pablo Escobar kama ulimwengu wote ulivyomtambua

Akiwa mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto saba ambapo baba yake alikuwa ni mkulima na mama yake alikuwa ni mwalimu wa chekechea...Pablo Escobar alikuwa ni mwenye kutamani mambo mazito na mwenye maono makubwa tangu angali mtoto

Akiwa bado mwenye umri wa makumi(teenage) Pablo mara kwa mara aliwaambia ndugu zake na marafiki zake kuwa anataka awe na utajiri wa kiasi cha pesa milioni moja za Colombia(COL$ 1 Mill) atakapofikisha umri wa miaka 22

Ndoto hizo zilimfanya ashindwe kumaliA chuo kikuu alipokuwa anasoma(Universidad Autonoma Latino Americana of Madellin) na kujiingiza katika biashara za halali na haramu na hatimaye aliacha masomo shuleni

Moja ya biashara zake haramu za kwanza kabisa akiwa kijana chini ya miaka 21 ilikuwa ni kutengeneza vyeti bandia vya stashahada vya chuo alichokuwa anasoma na kuwauzia watu waliohitaji kwa ajili ya kwenda kupata ajira.

Pamoja na biashara hiyo pia Pablo alijihusisha na kusambaza mizigo ya sigara zilizokuwa haziruhusiwi nchini Colombia (Marlboro), pia alifanya kazi kama mlinzi binafsi (bodyguard) pamoja na wizi wa magari.

Moja ya matukio muhimu ya ujana wa Pablo yaliyochangia kuamsha ari ndani yake na kumfanya atamani kuwa moja wa manguli wa biashara haramu lilikuwa ni tukio ambalo alipofikisha miaka 26 alifanikiwa kuweka benki (Cash Deposit) kiasi cha Peso Millioni 100 za Colombia (COL$ 100 Million).

Mafanikio haya yaliwasha taa ndani yake na kuamsha ari ya kutaka kuwa ‘Papa’ katika ‘Dunia’ ya siri ya ulimwengu wa biashara haramu.

Katika miaka ya 1970 mamlaka ya kupambana na matumizi mabaya ya madawa nchini marekani (US Drug Enforcement Agency) waliwahi kutangaza kuwa wamewekeza zaidi rasilimali zao kupambana na matumizi na uingizaji wa dawa aina ya Heroin nchini marekani na kwa maoni yao walisema kuwa wanadhani madawa aina ya Cocaine hayakuwa na uwezo wa kuleta uteja (addiction) au kufanya mtumiaji kuwa muhalifu tofauti na dawa aina ya Heroin.

Hivyo basi walielekeza nguvu zao zote na rasilimali kupambana na biashara ya usafirishaji wa Heroin kama kipaumbele cha kazi zao.
Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa upande wao. Kwani kijana Pablo aliona mwanya huu na udhaifu huu upande wa DEA au pengine tusema kwamba Pablo alifahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa mihadarati kuliko DEA.

Kitu kikubwa ambacho Pablo alikiona na watu wakiwemo DEA hawakukiona ilikuwa ni uwezekano (potential) ya kuifanya Cocaine kuwa moja ya madawa yenye soko zaidi Amerika ya Kaskazini.

Katika kipindi hiki kulikuwa na watumiaji wachache sana wa Cocaine nchini marekani lakini Pablo aliona fursa ya kuifanya mihadarati hiyo kuwa moja ya madawa yenye kuhitajika sana nchini marekani na ulimwenguni kiujumla.

Kutokana na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu, Pablo aligundua kuwa zao la Coca linalimwa nchini Bolivia ambalo linatumika kutengeneza Cocaine ni bora zaidi kuliko Coca inayolimwa nchini kwake Colombia. •
Hivyo basi Pablo akadhamiria kuwa kama anaingia kwenye biashara hii ya kusafirisha Cocaine ni lazima mihadarati yake iwe tofauti na bora zaidi kuliko Cocaine nyingine watu waliyozoea kutumia. Akadhamiria kufanya Cocaine yake iwe daraja la kwanza ili kuvutia watumiaji na kufanya soko likue kwa haraka.

Kama sehemu ya mkakati wake wa kuingia rasmi kwenye biashara ya kusafirisha mihadarati aina ya Cocaine, mwaka 1975 kijana Pablo alisafiri mpaka nchini Bolivia kukutana na Roberto Suaréz Goméz ambaye marafiki zake walipenda kumuita El Padrino (The Godfather) kiongozi wa Genge lililoitwa La Corparacíon (The Corporation). •
Suaréz alikuwa ndiye mtu pekee anayeendesha na kuratibu uzalishaji wa zao la Coca katika nchi ya Bolivia na Peru. Kipindi hiki Suaréz tayari alikuwa na mtandao mkubwa katika America ya kusini na alikuwa na jina kubwa, ushawishi na nguvu ya kijeshi hivyo haikuwa kazi rahisi kwa kijana Pablo kumshawishi Suaréz akubali kufanya naye biashara.

Huyu bwana Suaréz alikuwa na nguvu kiasi kwamba alikuwa na jeshi lake binafsi la anga (Air force) na wanajeshi wa miguu 1,500 ambao walipatiwa mafunzo nchini libya.

Pablo alitumia uwezo wake wa kujieleza na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu kumshawishi Suaréz na kumueleza kuhusu mkakati wake wa kuiteka biashara ya mihadarati ya Cocaine nchini marekani na akamdadavulia jinsi ambavyo yeye Suaréz atapata utajiri wa kupindukia kama atakubali kufanya nae biashara.

Pia Pablo alimpa wazo Suaréz kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini (Suaréz alikuwa amefanikiwa kumpenyeza Mdogo wake serikalini na kuwa Waziri wa mambo ya ndani) ahakikishe wanakutana na kiongozi wa Cuba Fidel Castro ili wamuombe kuwa mshirika wao katika mambo kadhaa.

Suala hili lilifanikiwa kwani Pablo na Suaréz walipata fursa adhimu na wakakutana na Fidel Castro na ombi lao kubwa kwake lilikuwa ni kuwaruhusu kupitisha mizigo yao nchini kwake Cuba na nchi za jirani pasipo bugudha. Pia walimuomba aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanja vya ndege vya Cuba na kujaza mafuta pale inapobidi kufanya hivyo.

Castro akawakubalia kwa masharti mawili, moja ni kwamba atakuwa anawachaji mamilioni ya dola za marekani kwa huduma hizo na pili mihadarati hiyo isiuzwe ndani ya Amerika ya Kusini bali isafirishwe na kuuzwa Marekani ambapo Fidel Castro alisisitiza kuwa atafurahi akiona vijana wa Mabepari wakiharibika na mihadarati.

Masharti yote mawili haya yakakubaliwa na Pablo na Suaréz kisha wakarejea Bolivia. Baada ya kufanya mazungumzo juu ya namna watakavyo fanya biashara hatimae Pablo na Suaréz walifikia muafaka na kwa mzigo wake wa kwanza alioununua nchini Bolivia kutoka kwa Suaréz ulikuwa ni kilo 14 za unga gafi za Cocaine

Baada ya unga gafi kufikishwa nchini Colombia kwenye mji wa Medellín, Pablo alikuwa ameandaa jengo maalum la ghorofa mbili ambalo alilitengeneza kuwa maabara maalumu ambapo Cocaine gafi kutoka Bolivia ilichanganywa na maligafi nyingine na kuboreshwa zaidi kikemia na hatimaye kupata Cocaine daraja la kwanza aliyoihitaji tayari kusafirishwa nchini Marekani kwa ‘walaji’.

Baada ya Cocaine kutoka kwa Pablo kuingia kwenye soko la Marekani uhitaji na biashara ya mihadarati ya Cocaine ilipaa kwa kasi ya ajabu na Pablo Escobar akaanzisha rasmi genge lake la biashara ya mihadarati na akaliita Medellíne Cartel.

Pablo akatengeneza mtandao madhubuti wa wasambazaji wa mihadarati yake katika miji ya Florida na California pamoja na majimbo mengine ya Marekani.

Pia akabuni njia mpya ya kupitisha mihadarati kupitia Bahamasi katika kisiwa cha Norman’s Cay takribani kilomita 350 kusini mashariki mwa pwani ya Florida.
Ili kufanikisha zaidi azma yake Pablo Escobar alinunua nusu ya ardhi ya kisiwa cha Norman’s Cay na nusu nyingine ikanunuliwa na swahiba wake wa kimarekani aliyeitwa Robert Vesco ambaye pia alikuwa ndiye anashughulikia masuala yake ya kibenki na uhasibu..

Katika Kisiwa hiki Pablo alitengeneza uwanja wa ndege, bandari, hoteli, nyumba za kuishi pamoja na ghala kubwa la jokofu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mizigo ya Cocaine kabla ya kuisafirisha kwenda marekani. Kwa kifupi hapa ndipo kilikuwa kitovu cha kibiashara cha Genge lake la Medellíne Cartel.

Pablo Escobar alikuwa amepania haswa kuliteka soko la Cocaine Amerika ya Kaskazini na hii ilijidhihirisha kutokana na juhudi zake alizozifanya kibiashara ili mda wote awe hatua kadhaa mbele tofauti na washindani wenzake kibiashara.

Ili kufanikisha usafirishaji wa mizigo yake kwa ufasaha na uhakika Pablo alinunua ndege za mizigo 15 za ukubwa wa kati na helikopta 6. Pia alinunua Nyambizi ndogo mbili (submarines) kwa ajili ya kusafirisha mizigo mikubwa ya mihadarati.
Hadi kufikia mwaka 1985 Pablo alikuwa anasafirisha takribani tani 70 mpaka 80 za Cocaine kwa mwezi na alikuwa ameshikilia asilimia 80 (80%) ya soko la mihadarati la Marekani.

Na katika kipindi hiki Genge lake la Medellíne Cartel lilikuwa linaingiza kipato cha cha Dola Milioni 70 kwa siku (Shilingi Bilioni 140 za Kitanzania) na mapato yao kwa mwaka mzima yalifikia Dola Bilioni 21.9. (Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania).


Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)
Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.

Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).

Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.
****
Katika miaka ya 1990 utajiri wake binafsi ulifikia kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 30 ambazo ni sawa na Dola Bilioni 54 kwa hesabu za sasa (Shilingi Trilioni 110 za kitanzania)
Ni katika kipindi hiki ambacho Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba 5 tajiri zaidi ulimwenguni na muhalifu tajiri zaidi katika historia ya Ulimwengu.

Kutokana na nguvu na ushawishi alionao, Pablo aliteuliwa na serikali kama mjumbe wa baraza la wawakilishi la Colombia (Chamber of Representatives of Colombia) kupitia chama cha Kiliberali Cha Colombia (Colombia Liberal Party).

Moja ya majukumu muhimu aliyoyafanya akiwa kama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kilikuwa ni kwenda kuiwakilisha Serikali ya Colombia katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mpya wa Uhispania Bw. Felipe González mwaka 1982 ambapo Pablo alitumia nafasi hii ya Safari ya kiserikali nchini Uhispania kuanzisha tawi jipya la Genge lake la Medellíne Cartel katika nchi ya Uhispania.

HACIENDA NÁPOLES: Pepo Juu ya Uso wa Dunia
Kutokana na utajiri uliopitiliza wa Pablo Escobar alithubutu kutengeneza makazi ya kuishi ambayo namna pekee ya kuyaelezea ni kana kwamba alijitengenezea ‘pepo’ akiwa duniani.

Katika mji mdogo wa Puerto Triunfo, takribani kilomita 150 kutoka katika mji wa Medellín, Pablo alinunua eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 20 na kujenga makazi yake na familia yake na akayaita makazi haya Hacienda Nápoles (Naples Estate).
Licha ya majengo ya kifahari ya kuishi yeye na familia yake pia makazi haya yaliwekwa anasa lukuki zisizomothirika.

Ndani ya makazi haya kulikuwa na Uwanja wa ndege binafsi (private airport), bustani maalumu ya sanamu za kuchonga na kufinyanga (Sculpture Park), kulikuwa na sehemu maalumu ya kuhifadhi magari ya kifahari na pikipiki za kifahari kwa ajili ya kutazama tu (collection), kulikuwa na uwanja wa mbio za magari magogo (kart racing track), kulikuwa na uwanja wa mapigano ya ng’ombe (Bullring), na pia ndani ya makazi haya kulikuwa na mbuga ya wanyama ya kutengeneza (Zoo) ambapo Pablo alikusanya aina mbali mbali za wanyama kutoka kila kona ya dunia na kuwaweka humo...

PLATA O PLOMO
Moja ya vitu muhimu vya kihalifu alivyovifanya Pablo na kufanikiwa kuibuka kama kinara wa uhalifu Amerika ya kusini ilikuwa ni kutekeleza sera yake aliyoianzisha yeye mwenyewe ili kuidhibiti serikali na vyombo vya ulinzi ambapo sera hii aliita “Plata o Plomo” (silver of lead (fedha au risasi)). Akiwa na maana kwamba kama wewe ni mtu wa serikali na ikitokea mmesigana basi atakupa fedha (rushwa) kama ukikataa kupokea fedha basi anakupiga risasi.

Sera hii ilimfanya Pablo aogopwe na watendaji wa serikali pamoja na vyombo vya usalama na ikapelekea wengi kukubali ‘Plata’ (silver (fedha)) wakihofia kupoteza maisha endapo wangekataa fedha kutoka kwa Pablo.
Hii ilimsaidia Pablo Escobar kuwa na vibaraka wengi katika serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Lakini sera hii iligharimu maisha ya watu wengi sana wale ambao walikataa kupokea fedha kutoka kwa Pablo na mojawapo ya matukio mawili yanayokumbukwa sana ya utekelezaji wa sera ya ‘Plata o Plomo’ ni haya:-

Mosi; Uvamizi wa Mahakama Kuu ya Colombia 1985.
Mwaka 1985 baada ya mabishano ya muda mrefu bungeni kuhusu vifungu vya kikatiba vinavyokataza raia wa nchi ya Colombia kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni akiwa kama muhalifu hatimae serikali ikafungua kesi ya kikatiba mahakama kuu ya Colombia ikitaka ruhusu ya kukabidhi baadhi ya wahalifu kwa serikali ya Marekani ikitokea wakikamatwa.
Suala hili lilikuwa linamlenga moja kwa moja Pablo Escobar kwani serikali ya Colombia ilikuwa inapewa shinikizo kubwa na Marekani kuwa wafanye marekebisho ya katiba ili iruhusu raia wa nchi hiyo ambaye ni muhalifu kukabidhiwa kwa nchi ya kigeni. Haya yalikuwa ni maandalizi endapo ikitokea Pablo Escobar akikamatwa.
Pablo akajitahidi kwa juhudi zake zote kuhonga serikalini na hata kutoa onyo kuwa mabadiliko hayo ya kikatiba yasifanyike lakini serikali iliendelea na mchakato kutokana na shinikizo walikuwa wanapata kutoka kwa marekani.


Inajulikana kwamba Pablo mara kwa mara alikuwa akiapa mbele za watu wake wa karibu kuwa kamwe hatokubali kufungwa katika nchi ya marekani na alikuwa na msemo anaoupenda kuusema kwamba “ni heri kuwa kaburini Colombia kuliko kuwa hai kwenye gereza la Marekani”.

Baada ya juhudi zake zote za kuionya serikali kutobadili katiba kushindikana hatimaye Pablo akakodi kikundi cha wapiganaji wa msituni kilichoitwa M-19 ili wasaidie kumaliza tatizo lake.

Siku ya Novemba 6, 1985 majaji 25 wa mahakama kuu walikuwa katika vikao vya mwisho kujadili na hatimae waweze kuridhia mabadiliko hayo ya katiba lakini kabla ya kumaliza vikao vyao na kuridhia mabadiliko hayo walivamiwa na wapiganaji wa kikundi cha M-19.

Wapiganaji hawa walivamia na kuteka mahakama kuu kwa muda wa siku mbili na zaidi ya nusu ya majaji waliuwawa na waliosalia walichukuliwa mateka.

Majaji hawa waliochukuliwa mateka walikuja kutumiaka kama sharti muhimu la kuibana serikali waache kurekebisha katiba ili waweze kuachiwa. Baada ya serikali kukubali kuacha kubadili katiba hasa kipengele cha kukabidhi wahalifu kwa nchi ya kigeni, majaji wote waliotekwa wakaachiwa.

Pili; Mauaji Mgombea Urais Luis Carlos Galán
Tukio la pili linalokumbukwa sana la utekelezaji wa sera ya ‘Plata o Plomo’ lilikuwa ni mauaji ya mgombea Urais wa Colombia aliyeitwa Luis Carlos Galán.

Galán alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni nchi nzima na alikuwa anatarajiwa kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa urais wa Colombia wa mwaka 1990.
Moja ya sera kubwa aliyokuwa anaihubiri kila kona ya nchi ilikuwa ni kupambaa na Magenge ya Mihadarati hasa hasa akililenga Genge la Medellíne Cartel na kiongozi wake Pablo Escobar.

Pabloalimtumia barua kadhaa ambazo ziliwekwa nje ya nyumba yake kwenye kisanduku cha barua akimuonya na kumtaka aachane na sera hiyo ya kumsakama yeye pamoja na washirika wake wa Medellíne Cartel lakini Bwana Galán alionekana dhahiri amezamilia kutekeleza sera hiyo endapo angechaguliwa kuwa rais wa Colombia.

Akiwa katika kampeni Bwana Galán alifanikiwa kufika kwenye mji wa Madellín ambapo Pablo alikuwa na ushawishi mkubwa na wapo wananchi waliojaribu kumuua Galán kwa kumrushia guruneti la kutupa kwa roketi (Rocket Propelled grenade) lakini kwa bahati nzuri Bwana Galán akisalimika.

Baada ya hapo Pablo akakodi wadunguaji maalumu kufatilia nyendo za Galán na akawapa amri ya kumpiga risasi mara tu wakipata upenyo wa kufanya hivyo.
Wiki kadhaa baadae akiwa kwenye kampeni katika mji wa Saocho Kiranga alipokwenda kuhutubia wafuasi wake wapatao 10,000 waliokusanyika wakisubiri kumsikia na mara baada ya kuwasili na kupanda jukwaani kuhutubia kabla hajatoa hata salamu kwa wafuasi wake alidunguliwa na risasi na kupoteza maisha papo hapo.

Tukio hili lilizua taharuki nchi nzima na imekuwa skendali yenye utata mpaka leo hii nchini Colombia kwani kuna tetesi kuwa viongozi wa serikali, polisi, pamoja na mashushushu walishirikiana na Pablo Escobar kutekeleza mauaji haya.

Licha ya Pablo kuonekana kama adui namba moja nchini marekani na baadhi wa watendaji wa serikali ya Colombia hali ili kuwa tofauti kwa raia masikini wa Colombia ambao wengi wao walimuona kama shujaa wao na katika mji aliozaliwa na kushi wa Medellín anaonekana zaidi ya shujaa kwani mpaka leo hii wanamuona kama ni aina fulani hivi ya masihi walipewa.

Hii inatokana na umahiri wa Pablo Escobar katika mahusiano na jamii iliyokuwa inamzunguka.
Pablo alikuwa ni mtu mwenye kusaidia masikini nchini Colombia pengine kuliko hata serikali yenyewe.

Pablo alijitolea kweli kweli katika kuboresha huduma za jamii kama vile kujenga mahospitali, shule, nyumba za wazee, nyumba za kuishi kwa ajili ya masikini na akawekeza fedha nyungi kujenga miundo mbinu ya Kanisa Katoliki na nyumba za kuabudia.

Pia Pablo alijenga vya kuendeleza watoto katika mpira wa miguu, alifadhili klabu mbali mbali za wakubwa za mpira wa miguu na alijenga viwanja vya kisasa kabisa vya mpira na michezo mingine.
Ilifikia hatua mpaka Pablo alikuwa anawapa fedha taslimu wananchi wa Madellíne ili waweze kujikimu kimaisha.

Mambo haya yote yalifanya wananchi wampende na kufumbia macho uhalifu wote aliokuwa anaufanya.
Kwa mfano katika mji wa Madellín ilifikia hatua kana kwamba wananchi wote walikuwa ni walinzi wake binafsi kwani walikuwa wakimtonya kila walipoona polisi wageni wakiingia hata kwa siri kwenye mji huo. Au wakati mwingine walikuwa wakitoa taarifa za uongo au kukataa kusema chochote pindi wakiulizwa na vyombo vya ulinzi kuhusu nyendo za Pablo.

Hii ilimfanya Pablo azidi kujizatiti na kuongeza mahaba kwa wakazi wa Medellín na raia wa Colombia kwa ujumla.

VITA KUU YA KWANZA YA MAGENGE YA MIHADARATI.

Kuna msemo wanasema ‘adui wa adui yako ni rafiki yako’! Swali: je, inakuwaje pale adui wa adui yako akitishia maslahi yako??
Adui wa Adui yako (Kikao cha Kwanza)
Hapo baadae nitaeleza kwa kifupi kuhusu kuibuka kwa genge lingine ambalo nalo lilishamiri katika biashara ya Cocaine lililoitwa Cali Cartel hivyo kufanya kuwe na uwepo wa magenge mawili yanayoshindana kibiashara yaani Medellín Cartel chini ya Pablo Escobar na Cali Cartel.
Licha ya ushindani wao wa kibiashara mwaka 1983 iliwabidi washirikiane kwa sababu za msingi kabisa.

kuliibuka kikundi cha wahuni waliokuwa wanateka watu na kudai fedha kutoka kwa ndugu ili wawaachie. Baada ya kuteka ndugu kadhaa wa viongozi wa serikali wahuni hawa wakaanza kuteka ndugu wa mabosi wa Cartels na kudai pesa.
Moja ya watu muhimu waliowateka alikuwa ni Marta Nieves Ochoa dada wa moja ya mabosi wa Cali Cartel na watekaji walikuwa wanataka wapewe dila milioni 10 ili wamuachie.

Hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya mabosi wa Cali Cartel na Medellín Cartel kukutana ili kuweka mkakati maalumu ambao utapeleka ujumbe kwa wahuni na watekaji wote kuwa familia za mabosi wa Magenge ya mihadarati ni mwiko kuzigusa.

Katika kikao hiki cha kwanza Medellín Cartel na Cali Cartel waliunda kikosi kazi maalumu walichokiita Muerte a Secuestradores (Death to kidnappers (Kifo kwa Watekaji)) au kama kilivyojulikana kwa kifupi MAS.
Kila Genge lilichangia fedha, vifaa (silaha), na askari kwa ajili ya kikosi kazi cha MAS.

Kesho yake baada ya kikundi hiki kuundwa ndege ilipita juu ya uwanja wa mpira wa miguu kuliko kuwa na mechi kubwa ikifanyika na kumwaga vipeperushi kuhusu kutangaza zawadi nono kwa yeyeto atakayetoa taarifa kuhusu kufahamu lolote juu ya wahuni wanaoteka watu na kushinikiza wapewe hela. •
Jioni ya siku hiyo taarifa muhimu kutoka kwa wananchi zikaanza kuletwa na kikosi kazi cha MAS mara moja kikaanza kukamata wahuni wa vikundi vya utekaji na kuwatesa huku wakiwarekodi na kuwatumia wenzao wanaoshikilia dada wa bosi wa Cali Cartel.

Ndani ya siku tatu Marta Naives dada wa bosi wa Cali Cartel aliachiwa akiwa salama salimini na huo ndio ukawa mwisho wa magenge ya wahuni kuteka wanafamilia wa mabosi wa magenge ya mihadarati.

Kama ni rafiki yako, anaweza kuwa mshirika wako: Kikao cha Pili
Licha ya ushindani wa kibiashara kuendelea kuwepo kati ya Medellin Cartel ya Pablo Escobar na Cali Cartel lakini kufanikiwa kwa mkakati wa MAS kuliwapa moyo kuwa yako maeneo mengine mengi wanayoweza kufanya kwa kushirikiana na yakawa na faida kwa pande zote mbili.

Sehemu ya kwanza ambayo waliona inaweza kuwa na faida kwa pande zote mbili ilikuwa ni Cali Cartel kukubali Pablo Escobar aweze kupitisha fedha zake haramu katika benki ya First InterAmericans Bank ambayo ilikuwa inamilikiwa na maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel. Hii ilikuwa na faida kwa kubwa kwa Pablo kwani ilikuwa ni njia rahisi na salama kwake kuweza kusafisha fedha zake haramu lakini pia ilikuwa na faida upande wa wamiliki wa benki maswahiba wa mabosi wa Cali Cartel kwani nao wangepata faida kwa kutoa huduma hiyo kwa Pablo kutokana mabilioni ya dola ya dola ambayo atakuwa anayapitisha kwenye benki yao.

Sehemu ya pili waliyokubaliana kushirikiana ilikuwa ni namna ya kuratibu bei ya Cocaine mtaani, kuratibu viwango vya ubora wa uzalishaji na njia salama za kusafirisha mizigo.

Ushindani mkubwa wa kibiashara kati ya magenge haya mawili unaweza kuwa sababu kubwa ya wao kuingia vitani lakini hii iliepushwa kutokana na vikao vya makubaliano walivyokaa awalinkuhusu kugawana soko.

Sababu kubwa zaidi na ya msingi iliyochochea vita hii ilikuwa ni Pablo kuamua kuacha kuheshimu makubaliano akiyoingia na Cali Cartel kutokana na genge hili kujihusisha na vitendo ambavyo Pablo alivipinga kwa nguvu zote.

Haijulikani ni kichaa gani kiliwapata viongozi wa ngazi za juu wa Cali Cartel lakini ilipofika miaka ya kati kati ya 1980 Cali Carteli wakaanza kujihusisha na imani zenye utata za “Kusafisha Kizazi/jamii” (Social Cleansing). Cali Cartel walisimamia mauaji ya mamia ya watu kwenye mji wa Cali pasipo sababu ya msingi wakidai kuwa watu hao wanaichafua Cali.

Mauaji yao yaliwalenga walemavu, machangudoa, watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, watoto wa mitaani, na watu wasio kuwa na makazi.
Baada ya kuwaua waliwaandika maandishi kifuania “Cali limpia, Cali linda” (Clean Cali, beautiful Cali (Cali nadhifu, Cali inayopendeza)

Vitendo hivi vilimkera Pablo na ikampa sababu ya kutokuheshimu makubaliano yake na Cali Cartel kuhusu kugawana soko na akaamuru watu wake wafanye biashara nchini marekani katika mji wowote ule wanaojisikia.

To be continue..........
IMG-20181101-WA0026.jpeg
 
Jamaa alikuwa boya tu angekuwa chini ya RC wa dar asingetamba ivi
Pablo Escobar sio MO DEWJ au YUSUF MANJI wewe kichwa, RC DAB ange kimbia nchi mwenyewe au tungeulizana raia, kama TUNA SAFIRISHA kwenda KOLOMIJE au tunapeleka mzigo KINONDONI.

Huyo jamaa alikua akiendesha jeshi zima, bunge na serikali ya ma mafia walioshindikana, sembuse huyo unaemtaja? Na aliwatoa jasho la makalio CIA miaka kenda!!!
 
Kama naiona Narcos hv,
Moja ya vitu vya muhimu sana alivowah fanya Pablo ni kuinvest kwa watu wa nchi yake , Pablo alijenga makanisa akawajengea maskini nyumba za kuishi na kutoa msaada kwa maskin. Hii kitu iliwapa tabu DEA kumkamata Pablo maana wananchi walikua wanampenda sana Pablo.na hawakua tayar kutoa taarifa zake...
 
Kuna Series moja inaitwa Kingpin inarlezea wahalifu nguli Duniani waliyowahi kutokea.
moja ya mtu wanaomuelezea ni Pablo ila maelezo yao na yako kidogo yanatogautiana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom