Plastic wrapping katika vituo vya SGR

Plastic wrapping katika vituo vya SGR

Ngurumbizi

Member
Joined
Aug 8, 2011
Posts
97
Reaction score
114
Kwa:
Mkurugenzi Mkuu
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
S.L.P 63154
Dar es Salaam, Tanzania

Yah: Ombi la Ufafanuzi Kuhusu Matumizi ya Plastic Wrapping kwa Mizigo ya Abiria wa SGR

Ndugu Mkurugenzi,

Napenda kuwasilisha taarifa na lalamiko kuhusu mwenendo unaoendelea kwenye vituo vya reli ya kisasa (SGR), ambapo abiria hulazimishwa kufunga mizigo yao kwa kutumia plastiki (plastic wrapping) kabla ya kuruhusiwa kupanda treni.

Taratibu hizi zimekuwa zikitekelezwa na wahudumu wasiobainishwa wazi kama ni wa TRC au watoa huduma binafsi, na mara zote huambatana na malipo kwa abiria. Hali hii imeibua maswali kwa umma, hasa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ina marufuku rasmi dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki kwa mujibu wa Kanuni za GN No. 291 ya mwaka 2022, zinazosimamiwa na NEMC.

Zaidi ya hayo, ipo hali ya mkanganyiko wa wazi: abiria wanaowasili katika viwanja vya ndege vya kimataifa hapa nchini huonywa kuondoa wrapping ya plastiki kabla ya kutoka uwanja wa ndege, kwa mujibu wa kanuni hizo za mazingira. Swali linajitokeza:

Kwa nini wrapping hiyo inakataliwa kwenye uwanja wa ndege kama ni hatari kwa mazingira, lakini ikiruhusiwa au kulazimishwa kwenye vituo vya SGR ndani ya nchi?

Naomba kufahamu yafuatayo:

1. Ni taratibu au Sheria gani imetumika kuhalalisha matumizi ya plastic wrapping kwenye vituo vya SGR?

2. Iwapo hakuna,
je NEMC inaweza kuchukua hatua dhidi ya utaratibu huu usio rafiki kwa mazingira?

3. Kuna sababu ipi ya msingi inayosababisha utofauti huu wa utekelezaji wa sheria kati ya viwanja vya ndege na vituo vya reli?

Naamini kuwa Baraza lenu lina nafasi muhimu ya kuhakikisha utekelezaji wa sheria za mazingira unafuatwa kikamilifu katika taasisi zote za umma na binafsi.

Natumaini barua hii itapokelewa na kufanyiwa kazi ipasavyo.

Wako katika utunzaji wa mazingira,
Dudumizi Ngurumbizi
 
Pamoja ya kwamba una hoja nzuri lakini plastic wrapping ni worldwide practice. Airports zote hufanya hivyo lakini sio lazima ni pale mtu binafsi akitaka kufanya hivyo ili kuzuia bag lake lisichubuke au kuchafuka then atalipia huduma hiyo na yale malipo huwa kama comensation kwa ajili ya kutumia plastic.

Jambo la ajabu ni kama hao SGR wanakulazimisha kufanya hivyo hapo watakuwa wanakosea. Ile haipaswi kuwa biashara bali hudma ambayo malipo yake huwa makubwa kiasi kwa sababu ya compensation ya matumizi ya plastic na pesa ile ilipaswa ipelekwe kwenye mfuko wa mazingira not otherwise
 
Binafsi mara zote nimepanda SGR sijawahi kukumbana na balaa la kulazimishwa ku wrap mizigo yangu..

Sijawahi hata kuona Mtu akimlazimisha Mtu afanye wrapping mule Stesheni..

Kwa uelewa wangu Mdogo, watu Kwa ridhaa Yao wenyewe huomba Huduma ya Plastic wrapping Kwa ajili ya usalama wa vitu vyao vya thamani walivyoweka kwenye mabegi ambayo yatafanyiwa check in (ambayo hawatabeba mkononi)..
 
Binafsi mara zote nimepanda SGR sijawahi kukumbana na balaa la kulazimishwa ku wrap mizigo yangu..

Sijawahi hata kuona Mtu akimlazimisha Mtu afanye wrapping mule Stesheni..

Kwa uelewa wangu Mdogo, watu Kwa ridhaa Yao wenyewe huomba Huduma ya Plastic wrapping Kwa ajili ya usalama wa vitu vyao vya thamani walivyoweka kwenye mabegi ambayo yatafanyiwa check in (ambayo hawatabeba mkononi)..
ukibeba magimbi au samaki wabichi lazima usije kuchafua treni yetu
 
Back
Top Bottom