Plan C: Baada ya mazungumzo ya Chadema na JK. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Plan C: Baada ya mazungumzo ya Chadema na JK.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sakafu, Nov 24, 2011.

 1. s

  sakafu Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mazungumzo baina ya JK na CDM yamepangwa kufanyika wiki ijayo kati ya jumatano hadi Ijumaa. JK anaweza kuhahirisha ku-assent muswada huo baada ya kukutana na CDM, baadaye NCCR, CUF na CCM. Maazimio ya NEC kuhusu kukutana na vyama vyote umekubaliwa na JK. Tayari, Salva ameagizwa kutoa mwaliko tamko kwa umma kwa chama chochote kinachotaka kukutana na JK kabla muswada haujawa assented.

  Hata hivyo, licha ya hoja hizo, JK atasaini muswada huo kwa sababu anaogopa kuingia katika mgogoro wa wazi na wabunge wa CCM walioupitisha kwa kishindo.

  NINI PLAN B KWA CDM:
  Katika Kikao cha Kamati Kuu ya CDM kilichoketi Dar es Salaam - Viongozi wa CDM walisema kuwa JK akikataa - Plan B itakuwa ni maandamano yasiyokuwa na ukomo kupinga muswada huo kuwa sheria. Msimamo huo tayari umeungwa mkono na Mbowe na Dr. Slaa.

  NINI PLAN B KWA CCM:
  Katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoketi Dodoma- wajumbe waliona hatari ya CDM pekee yao kukutana na JK, badala yake iwe ni kwa vyama vyote vya kisiasa angalau vyenye uwakilishi Bungeni ili kupunguza nguvu za hoja za CDM.

  NINI PLAN B KWA JUKWAA LA KATIBA:
  Miongoni mwa hofu kubwa sana kwa CCM ni Jukwaa la Katiba na CDM. katika kikao cha CC - CCM, wameitaka vyombo vya usalama kutoruhusu maandamano yoyote ya wanaharakati au CDM. Hayo yalibainishwa wazi na Mkama. Tayari jana jeshi la Polisi limeyazuia maandamano hayo kwa hoja ya fujo na ghasia kutokea.

  NINI PLAN C: tunasubiria.
   
 2. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uchambuzi makini.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  PLAN C: KUFANYA MAANDAMANO NCHI NZIMA KILA MKOA, KILA WILAYA NA KILA KIJIJI/ KATA KUWE NA MAANDAMANO askari hawatatosha kutuzuia na PLAN D: KUWAPIGA NA KUWATEKA ASKARI WOTE WATAKAOTUINGILIA KWENYE MAANDAMANO. Plan e:...
   
 4. S

  STIDE JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Plan B ya chadema ndio funga kazi!! Hakutakuwepo na haja ya plan C.
  Ila cdm wasihusishe wanaharakati maana tiyari wameonyesha uoga!!
   
 5. P

  Paul J Senior Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahasante kwa kutujuza.
  Ukisikia watu wanataka kuandamana, si kwamba watu hao ni wajinga bali huwa kuna kitu kinakuwa hakijakaa sawa. Kuzuia maandamano bila kuweka sawa kile kisichokuwa sawa ni sawa na kukuza tatizo maana ipo siku tu maandamano yatakuwa hayawezi kuzuilika kwa sababu na gharama yoyote ile. Ifikie point watawala waukubali ukweli taifa lisonge mbele. Tulipofikia hata Jukawa la KATIBA au CHADEMA au wanaharakati vikafutika chini ya uso wa tanzania bado kizazi kilichopo kitaandamana tu hata kama hawana kiongozi (kumbukeni yaliyotokea Mbeya). Misingi ya usawa, utu na heshima ya kijana wa tanzania na hasa masikini vimepotea kabisa na chanzo kiko wazi kuwa ni utawala mbovu usiojali maslahi ya watu wake na taifa kiujumla. Haya mambo hayawezi kupatiwa suluhu na serikali ya ccm au ccm yenyewe maana walipofikia ni bora liende tu hatutegemei jipya kwa wale wote ambao mentors wao ni akina Msekwa, Marcela, Mukama, Makamba au JK! Kwa sasa watu wataandama si kwa kuwa wanaipenda chadema au jukwaa la katiba au unaharakati bali hali halisi ya maisha ya watanzania tuliowengi na jinsi nchi inavyoendeshwa vinawalazimu wengi kuona maandamano ndiyo suluhu sahii ya serikali isiyoweza kutatua matatizo ya watu wake hasa ya umasikini,ujinga maradhi na gapi kati ya walionacho na wasiokuwa nacho.
   
 6. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Hii nimeipenda,
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndg yangu Angel, naomba usome bango vizuri na uelewe kabla ya kutoa maoni yako.
  Plan B ya CDM ilikuwa kuandamana kama JK angekataa ombi lao.
  Hoja, kama Jk amekubali kukutana nao lakini akakataa pendekezo lao, nini kitafuata?
   
Loading...