Plan A: Dunia kupoteza watu millioni 91.5 ndani ya masaa 5

Plan A: Dunia kupoteza watu millioni 91.5 ndani ya masaa 5

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,311
Reaction score
12,202
Wataalam wa masuala ya Sayansi na Usalama toka Chuo cha Princeton (Princeton's Program on Science and Global Security) wamefanya utafiti wao kutokana na mvutano unaoendelea hivi sasa duniani wa masuala ya ulinzi na usalama.

Katika utafiti wao (simulation) wamekuja na mpango wanauita "Plan A", mpango ambao unaonyesha ni jinsi gani bomu moja kutoka Russia linavyoweza leta madhara kwa dunia nzima ndani ya muda mfupi.

Katika simulation yao wameonyesha mfano Russia akiamua kupiga "nuclear warning shot" kwenda kwa washirika wa US-NATO pale watakapomua kumvamia basi vita itaenda sababisha watu millioni 91.5 kupoteza maisha ndani ya masaa 5.

PHASE 1:

NATO watakapo jaribu mvamia Russia basi atawajibu kwa kuwatumia mabomu 300 ili kupunguza Wanajeshi, Ndege, Vifaru na Kambi maalum za NATO zinazomvamia. NATO nao watajaribu jibu kwa kutuma mabomu 180 kwenda Russia kwa kutumia Ndege ili kumpunguza nguvu Russia.

vUtk9ktTURBXy82YWU5ZTk0Ni1jOTg5LTQ2ZmItYTI2Zi01YmMwOGU2NTgwZjAucG5nkZUCzQHgAMLDgqEwAaExAQ.jpeg

Mpaka hapa imekadiriwa watu Millioni 2.6 watakuwa majeruhi au wamepoteza maisha.​

PHASE 2:

Pale NATO watakapojaribu kulipiza kwa Russia, basi Russia atawajibu kwa kuilipua na kuiangamiza Ulaya ambao nao kwa pamoja watajibu wakitumia Nyambizi na msaada wa Marekani kwa kumlipua na mabomu zaidi ya 600.

9Mnk9ktTURBXy9jNzZlNDNlNC1hMTcyLTQ1M2UtYWE3NC00YjFlM2M5NGM2NDMucG5nkZUCzQHgAMLDgqEwAaExAQ.jpeg

Kufikia hapa watu Millioni 3.4 wataangamia ndani ya dakika 45.​

PHASE 3:

Katika hatua ya mwisho ya vita Russia na NATO watalenga miji mikubwa 30 yenye watu wengi na kuipiga kwa mabomu 5-10 kulingana na ukubwa wa mji wa adui.
Hatua hii ya mwisho itaangamiza watu millioni 85.3. Huku vita nzima ikiwa imeacha vifo vya watu millioni 34.1 na majeruhi millioni 57.4 au kwa hesabu ya jumla watu millioni 91.3 watakufa, potea au jeruhiwa kwenye vita ambayo haitachukua masaa 5.

-LWk9kuTURBXy9iMmMzMjY1Mi01MzFlLTRhN2YtOTczZC03OTgzMzUzM2U2NWYuanBlZ5GVAs0B4ADDw4GhMQE.jpeg
Vita hii itaiathiri dunia nzima kwa miaka mingi ijayo. Kutokana na 'radioactive fallout' ambazo imeonyesha itasababisha anga la dunia kupoa kwa ghafla, Njaa kubwa itatokea, Wakimbizi watakuwa wengi sana, Wizi na Vurugu zitatokea duniani.

Video:

Business Insider
 
kwani hapa ule usemi wa "ndugu wakigombana shika jembe ukalime"hauapply[emoji16][emoji16]

maana nahisi nitakuwa na kazi nyingi za kufanya.
 
Mpango wa kupatikana kwa Anti-Ballistic Missile System ya kueleweka utakapokamilika, hizo silaha zitatumika tu na zitakuwa 'za kawaida'. Hii bado ni ndoto yenye vikwazo vingi vinavyosababisha ichelewe kutimia.

Bahati mbaya ni kuwa juhudi hizi za kupatikana kwa Defence System ya haya makombora zinakwamishwa kutokana na kwamba silaha hizi zinazidi kuwekewa uwezo mkubwa wa kutoweza kuzuilika (Interception).

Ila nisiwavunje moyo wale wanaosubiria Teknolojia hii ya kukabiliana na Makombora haya ambayo ni 'magumu' kuwa Intercepted kwamba hatua zimefikia mahala pazuri na juhudi bado zinaendelea.
 
ABM ni kazi kuizuia, hakuna mfumo unaoweza zuia hii kitu badala yake inapunguza maumivu ya kipigo kwa kudetermine critical points na kuzidefend!.
 
Wapigane tu tumechoka kusubiri vita ya tatu
Afrika mtakosa mafuta.. Nchi itaingia gizani ndani ya siku mbili mpaka tatu. Huduma za muhimu zitasitishwa. Pesa itapoteza thamani ndani ya muda mfupi.

Vurugu, wizi, mauaji, vitatamalaki.

Hapo mtamuita mpinga kristo aje haraka aitawale dunia kwa kutumia vibaraka na majeshi.
 
Hizi story tu za kupitisha muda. USA na Russia hawatapigana kamwe. Wote wanajua hamna wa kumshinda mwenzake sasa ya nn kupigana?
Unavyosema “kamwe” unamaanisha nini . Umetumia vigezo gani vya kihistoria au vya kihisia
 
USA/NATO VS RUSSIA HII VITA UTASUBIRI SANA HAITAKAA ITOKEE KAMWE
wenye akili zao wanafanya simulation kuangalia faida na hasara, kwa mtogole tunaaminishana HAITOKAA ITOKEE!..
 
Hizi story tu za kupitisha muda. USA na Russia hawatapigana kamwe. Wote wanajua hamna wa kumshinda mwenzake sasa ya nn kupigana?
Wazungu vita ya kwanza na ya pili ya dunia ili wagarimu sana maisha yao mpaka leo kuna makovu makubwa. Wazungu hawataki tena kusikia mambo ya vita kwenye ardhi yao. Watapigana mikwara kwenye media tu lakini hutasikia vita ulaya kamwe
 
USA hajawahi kuonja full scale war yeye anafanya expedition tu, so mtoe kwenye watu waoga wa vita. Israel muda wote anawaza kutafuta chimbo apigane vita naye si wa kumuweka kundi la watafuta amani ya mezani!.
Kule North Korea muda wowote anataka achemshe mapipa yake Washington DC, Russia mwenyewe amekaa nje ndani sera zake zinaadvocate kila mtu akae kwake sasa anavyoona anafatwa mpaka Ukraine muda wote amekaa kwenye kill switch!..
Its not leo wala kesho but WW3 itaenda tokea kuibalance upya dunia!.
 
Kuna mtu akiiona hii atasema hawa mabeberu waanza tuuze mahindi yetu. Kwa ujumla ukiangalia ramani africa tutakuwa kimbilio lao
 
Kuna mtu akiiona hii atasema hawa mabeberu waanza tuuze mahindi yetu. Kwa ujumla ukiangalia ramani africa tutakuwa kimbilio lao
Hapo ni makadirio ya masaa 5 baada ya hapo kinachofata sasa ni proxy war kwa watakaokuwa wamebakia!.
Africa na Asia tutatakiwa chagua upande wa kupigana iwe kwa kupenda au kutopenda!.
 
Back
Top Bottom