Pole sana ndugu yangu, ni mitihani tu ya maisha ila ina mwisho wake. Kwanza napenda kukwambia usisikilize ya watu, kila binadam ana uelewa wake na mapungufu yake, kwahiyo usivunjike moyo unapokatishwa tamaa, wewe songa mbele tu. Km ulivosema ajira ngumu, mi sioni tabu ukianza hiyo kazi kama unaipata maana pia ina ugumu wake, sina uwelewa mkubwa kuhusu mshahara lakini nafahamu ni mdogo sana, na wengi wanaofanya hizo kazi hawategemei mshahara bali wanategemea kazi na madili wanayopata huko wanapoenda kulinda, utakuta mtu ana gari yake anataka umuoshee anakupa elfu mbili, mwingine kakutuma dukani chenchi imebaki kakupa, mambo kama hayo.
Nashindwa kukushauri zaidi kutokana sifahamu elimu yako ni ngazi ipi, naomba unijuze tafadhali angalau nipate mwanga naweza nikawa na ushauri na pengine ikakusaidia.
Kingine kama umesoma na kazi hauna, hata kama una degree ya kwanza, nakushauri ni bora zaidi hata ukaomba kazi kama mhudumu kwenye kampuni, wale wanaoandaa chai kwa mabosi, wanaofuta futa vumbi, ni rahisi pale ukimzoea boss ukimpa cv yako hata yeye atasema kwl unahitaji kazi maana umetokea chini sn, atakuona kwl una nia, kuliko kwnye ulinzi kufikia malengo kidogo ni ngumu zaidi ila inawezekana.
Samahani kwa kukuchosha na message yng ndefu. Asante