Pistorius apatikana na hatia ya mauaji

Pistorius apatikana na hatia ya mauaji

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
attachment.php


Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini imempata mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius na hatia ya mauaji.


Mahakama hiyo imekubali rufaa iliwasilishwa na upande wa mashtaka ikitaka Pistorius apatikane na hatia ya mauaji, ambayo adhabu yake ni kali zaidi kuliko ya kuua bila kukusudia.

Jaji Lorimer Leach amesema mwanariadha huyo anafaa kurejeshwa kwa jaji aliyemhukumu ili apokee adhabu ya kosa la mauaji.

Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 2013 baada ya kufyatua risasi kupitia mlango wa choo.

Amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani baada ya kukaa mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Awali, ilikuwa imeripotiwa kimakosa kwamba rufaa hiyo ilikuwa imetupwa na angeendelea kutumia kifungo cha kuua bila kukusudia.

Pistorius alifungwa jela miaka mitano mwaka 2014 baada ya kupatikana na kosa hilo la kuua bila kukusudia.

Chanzo:
BBC Swahili
 

Attachments

  • 141210083201_pistorius_court_promo_640x360_afp_nocredit.jpg
    141210083201_pistorius_court_promo_640x360_afp_nocredit.jpg
    12 KB · Views: 1,786
Huyu ni kweli aliua anafaa kwenda jera tu .risasi tatu zote hijui unarenga nini acha akae jera .kudus
 
Kwaheri Pistorius jela sio mwisho wa life ila kwasababu uliuwa nenda katimikie kifungo.
 
I would have been surprised if the appellate court couldn't have found merit in the appeal. It's clear that the guy had 'malice aforethought'. He had a conscious intent to cause death or grievous bodily harm to whoever was behind the door. 'Four bullets' was a clear predetermined actus.
 
Huyu bwana,ni kweli aliua makusudi coz ya wivu wa kimapenzi ,alishatambua demu wake anachepuka na mcheza mpira baada ya uchunguzi wa muda mrefu ilipowadia siku akajifanya anaenda fanya mazoezi kumbe amesha hack simu ya mpenziwe ,ndipo huyo mpenzi akawasiliana na huo mchepuko wake ili wakafanye yao fasta kabla kilema hajarudi ,jamaa hasira zikamzidi ndipo aliporudi ghafla wakati mpenzi wake anaoga kujiandaa kutoka na mchepuko wake.kilichofata mauaji
 
I would have been surprised if the appellate court couldn't have found merit in the appeal. It's clear that the guy had 'malice aforethought'. He had a conscious intent to cause death or grievous bodily harm to whoever was behind the door. Four bullets was a clear predetermined actus.

Duh! u shuld defend me once i have shot my wife dead for cheating on me
 
I would have been surprised if the appellate court couldn't have found merit in the appeal. It's clear that the guy had 'malice aforethought'. He had a conscious intent to cause death or grievous bodily harm to whoever was behind the door. Four bullets was a clear predetermined actus.

Uko law school? Umetema paragraph ya shule
 
Kama alimchoka mkewe angemuacha tu yanini kumuua? Afungwe tu.
 
Back
Top Bottom