Pinda: Wanaopinga kodi ya simu hawana jema

Tatizo hasa ni matokeo ya kodi tunazolipa!..Tumeshalipa sana kodi na matokeo hatuoni! Na hata kdg kinachofanyika pesa yake inakua imekopwa! SASA pesa za kodi tunampeleka wapi?
 
Dah! nani alimpa hili jina la mtoto wa mkulima? huyu ni mtoto wa Fisadi no, ni FISADI.
 
mi siku zote nawaambia ccm imezeeka,haina mawazo mapya,tujaribu kuitupia cdm hapo magogoni tuione nayo itafanya nini,watz tusibaki kulalamika tu ikifika 2015 ukipewa wali nyama na tshirt unalegea aaaah siwapend ccm
 
hahahaaa...ni sawa na kupanga kwa kila shule za msingi kutumia sofa badala ya madawati wakati madawati yenyewe hatuyawezi...Serikali imetupiga changa la macho hapo.
 

Kauli moja wataitoa wapi hawa akina Pinda, Makamba na Nape? Utatu huu usio mtakatatifu haujui unatetea nini, unakosoa nini ama unawakilisha nini...yaani ni mzabwamzabwa tu alijisemea Marijani Rajabu.

Dawa yao ni kuendelea kuwabinya mbinyo wa kisiasa. Mnyika lazima awatoe kamasi hawa. Tena siku zao za kutawala kwa hila zinahesababika
 

I hate this dude with a passion :A S-fire1:
 
Hypocricy to acquire public sympathy. Siwakachuke zile zinazozagaa zagaa bila kazi hadi deep green na kagoda wakajitwalia. Nchi hii, kila kukicha maudhi mapya, so sick and tired, na hatulipi liwalo na liwe.
 
Punda,makombo na nepi eee! Nimewachukia wanyama kama punda, sili makombo na nimekua sivai nepi.
 
Hivi kwanini hii serikali kila kiongozi anakuja na kauli yake!? Hawa mbona wanakuwa kama kambale? Au serikali inapoteza maana ya kuwa serikali? Rais anasema hili, waziri anasema tofauti, katibu wa ccm anasema tofauti kuhusu suala lile lile.
Nimeamini kwamba ujenzi wa mnara wa Babeli umeanza.
 
Hii nafasi ya Waziri mkuu baada ya kujiuzulu Lowassa hata ingeachwa wazi hakuna madhara yoyote ambayo yangetokea. Huyu aliyepewa nafasi hiyo ni hasara tupu hana uwezo wowote!
 

Kweli huyu jamaa hovyo sana. Angekuwa na akili angechagua kufunga domo lake labda angesahaulika. Walivyokuwa wajinga eti wametenga bilioni moja kwaajili ya mazishi ya viongozi watakaokufa mwaka huu na shilingi milioni 18 kwa ajili ya wajumbe wa tume ya katiba watakaopata ukimwi(Akina Warioba!) Hii nchi inaweza kwenda bila waziri mkuu! Huyu ni kimeo cha karne!
 
wananchi wanapokataa mpango fulani wa serikali,basi viongozi ni lazima wasugue vichwa kwelikweli

Kweli lakini sio hawa tulio nao! Katika mikosi mikubwa iliyoipata nchi hii ni pamoja na kuwa na viongozi kama Pinda na bosi wake!
 
Watu waliochoka wanatakiwa wapumzike la sivyo wataendelea kusababisha majanga kwa wa Tanzania! Viongozi waliojilimbikiizia mali za ufisadi, wanaoongozwa na ushabiki wa kichama na ubinafsi wanaianganiza Tanzania! Wananchi tuamke....
 
huyu mzee nilikua namuheshimu lakini anazidi kujiaibisha kila siku anashindwa elewa hii ni kama KODI YA KICHWA na usije na excuse ya kupeleka umememe vijijini wala wapi izo excuse ni za kizaman!!! tafuten pesa kwa vyanzo vingine kwa ajili ya kupeleka huo umeme vijijini kama kwenye madini, utalii, kilimo, uvuvi nk tuna kila kitu mnashindwaje kupata pesa!!!
 
Huyu mzee kachoka. anataka kutudanganya eti hela hiyo itatumika kwa ajili ya umeme vijijini. mbona hela zinazoibwa na kufanyiwa ufisadi ikiwa ni pamoja na matumizi ya ovyo serikalini ameshindwa kuyadhibiti miaka yote! Hivi ni kodi ngapi tunakatwa kila kukicha lakini mashuleni shida, hosipitali shida, miundombinu mibovu and not sustainable.. Laana iwashukie wote wasio wahurumia wananchi wanaoteseka Tanzania. Hizi ni hila za ccm kujinufaisha wachache kwa kuwaumiza wengine...
 
Pindaaaaaaaaaaaaa ivi kwenu kule Kilando Namanyere kuna mtu ana uwezo wa kulipa iyo BUKU?
Alafu makusanyo ya sasa yanatumikaje mpaka mnataka kutuambia kuwa mnataka na izo za simu
Obama alikuja na bit la Power Africa limeishia wapi?
Sikubaliani na suala la hii kodi to me ni namna ya kujitafutia ulaji tuu.
Kuweni a HURUMA juu ya wapiga kura wenu
 
ni kweli watozwe tu serikali haina hela tumechoka kuomba sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…