Pinda vs Lowassa vs Sumaye - Ufanisi katika kuongoza sekta ya Elimu iliyo chini ya TAMISEMI

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Naomba kutoa masikitiko yangu makubwa sana juu ya Mh. Pinda kushindwa kumsaidia Rais kwenye suala la Elimu.

Ni muhimu kwanza kuweka wazi kwamba shule za msingi na sekondari ziko chini ya TAMISEMI, wizara iliyochini ya Waziri Mkuu. Hivyo majukumu ya mambo ya shule za Msingi na Sekondari yako kwa ujumla wake chini ya Waziri Mkuu.

Sasa naomba tujikumbushe.

Sumaye:
- Alibuni, akasimamia kwa ukaribu wa hali ya juu tatizo la madawati kwenye shule za msingi na sekondari, bila msaada mkubwa wa Rais Mkapa. Na wale wanaokumbuka alifanikiwa sana,

LOWASSA
- Alibuni, akasimamia ujenzi wa shule za kata a.k.a shule za Lowassa bila msaada wa karibu sana wa Rais. Haya ndio matokeo makubwa ambayo CCM inayaringia kupita matokeo mengine yote.

PINDA
- Rais wake, boss wake amebuni na kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa maabara za shule za sekondari. Kwa maana nyingine msaidizi wa Rais badala ya kumsaidia Rais yeye ndiye sasa mwenye kusaidiwa na Rais.

Ninasikitishwa kama Raia wa Tanzania kuwa na waziri mkuu kama huyu... Mimi sio mwanasiasa hivyo isijechukuliwa ni kampeni... ni ukweli tu,

Mwenye maoni tofauti na haya karibu.
Pasco Ritz
 
wewe hujui lowasa alikuwa moja kwa moja waziri wa tamisemi sumayi alikuwa kama waziri tamisemi ikiwa chini yake mawaziri walikuwa manaibu kwa miaka 5 miaka 5ya mwisho wake kulikuwa na waziri kamili na pinda alikuwa naibu waziri tamisemi wakati kabla ya kumaliza kwa mkapa pinda akawa waziri kimili wa tamisemi jibu lipo moja kwa moja kazi hiyo pinda ndio mzoefu tamisemi kipindi hiki cha awamu ya nne kuna waziri wa tamisemi na manaibu wawili na mpaka sasa wamedhibiti wizi wa mitihani
 
  • Mbona kipindi hiki Rais anamfanyia kazi yeye?
  • Mimi nadhani ni kweli ana uzoefu wa kufanya kazi taratibu na kwa ulegelege,
  • Pinda can not think big projects... lazima vitu vidogo vidogo.
 
Back
Top Bottom