Pinda: Serikali inakabiliwa na hali mbaya kifedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Serikali inakabiliwa na hali mbaya kifedha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Apr 14, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Serikali inakabiliwa na hali mbaya kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo, serikali imeziagiza wizara na taasisi zake kufunga mkanda na kuhakikisha wanabana matumizi ili angalau fedha zilizopo ziweze kumaliza mwaka huu wa fedha wa 2011/2012.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo bungeni jana wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge. Pinda alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, aliyetaka kujua serikali inafanaya nini kupunguza makali ya maisha kwa watanzania hasa kutokana na kupanda kwa kiwango cha mfumuko wa bei.

  Mohamed alihoji kama serikali imefilisika kwa kuwa Wizara na idara zake zote zimekuwa zikilalamikia ukata. Mbunge huyo alisema hali ya maisha ya Watanzania inazidi kuwa mbaya kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu, lakini serikali haionyeshi jitihada za makusudi kukabiliana na hali hiyo. Katika majibu yake, Pinda alikiri kuwa hali ya maisha imepanda, lakini si kwa Watanzania tu kwani hata nchi zinazoizunguka nchi hali ni hivyo hivyo.

  "Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe, tubane matumizi kwelikweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida, kweli mfumuko wa bei unapanda sana ingawa tumejitahidi kutafuta kila mbinu, lakini haitusaidii," alisema Pinda na kuongeza: "Tumejitahidi kuondoa ushuru wa sukari inayotoka nje, lakini bado haitoshi, mafuta nayo yanapanda bei kila siku hivyo tunaomba wafanyabiashara waisaidie serikali wawe waaminifu wasipandishe bei bila sababu."

  Hata hivyo, Pinda alisema kuwa serikali haijafilisika. "Pamoja na hayo serikali haijafilisika kwani ingekuwa hivyo wewe usingekuwa hapa bungeni?" alihoji.


  CHANZO: NIPASHE

  Mijadala ya awali:

   
 2. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Huku ndio kukumbuka shuka.., wakati mtu umeshaamka upo bafuni unaoga... :(

  Nadhani hapo inaitajika taulo na sio shuka..., To put it bluntly all that got us in this situation needs to be sacked
   
 3. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni wakati wa kujaribu mbinu za kuweka miundombinu mpaka vijijini mazao yaje mijini kwa urahisi, kubana matumizi (kuanzia kupunguza posho zao na kupiga mashangingi yao mnada, kupunguza baraza la mawaziri, kuhakikisha wawekezaji wanalipa kodi ya kutosha, kutumia mali asili zetu kwa manufaa ya wananchi, na bila kusahau kufufua viwanda vyetu nchini walivyoviua na kuongeza viwanda ili tusitegemee products toka nje ya nchi).

  Je wameshajaribu kufanya hayo?
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Hilo jibu la waziri ni jibu la kipumbavu kabisa!

  Angechanganua makisio ya mapato na mapato halisi kwa miezi kumi iliyopita.

  Halafu atuambie matumizi ya mapato, na ukasi unaotukumba ni wa kiasi gani na wizara zote zipunguze matumizi kwa asilimia ngapi.
  Huyo mbunge wa CUF aliridhika na hilo jibu kweli?... yaani hamna swali la nyongeza?

  That was too shallow!
   
 5. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi mnatumia mifumo hipi kichama kuwapa nafasi za juu watu kama hawa. So far nimekutana na watu wanaoniambia Mh.Pinda yupo Ikulu muda mrefu (to me it doesn't mean he is a qualified decision maker nor a useful spokes person), majibu yake ya pumba pumba kuanzia sakata la mgomo wa madaktari, issue ya Jairo, posho za wabunge and many more says it all.

  Na alivyo pimbi yeye huwa hanafikiria in terms of the higher echelon kwenye majibu ya bajeti or social issues. Ukweli wenyewe tuna safari ndefu sana ya kutafuta accountability and democracy, especially kuwafanya hawa jamaa wajue wajibu wao vilivyo or else may be its just me and my views of how responsibility should be, are outdated or do not fit the Tanzanian society. Lakini kama siasa inatumika Pinda ni pumba tupu na majibu yake.
   
 6. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Mwambie Pinda ahold chq ya Ml 10 waliyotaka kutoa kwa familia ya Kanumba it might help.
   
 7. Robati

  Robati JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hii serikali ya Tanzania inakatisha tamaa sana
   
 8. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Pinda ni janga la kidunia. Nachelea kusema ni aibu kumsimamisha katika jukwaa moja na mwenzie Raila Odinga kwani mwenzie yuko deep sana na ana mtazamo wa kimaendeleo.

  Tutamkumbuka sana DR Slaa, angekuwa presdaa asingetuwekea watu legelege kama hawa katika nafasi muhimu. We fikiria eti Pinda, Ngeleja na Werema ni sehemu ya baraza la mawaziri... Nchi hii ina laana au aliyetuloga alikufa.
   
 9. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunazidi kuongeza mawaziri wakuu wastaafu ambayo ni cost center.
  Siasa inapo oversmart uchumi ndiyo haya. Shughuli zote za maendeleo zitasimama ila pesa ya kuwalipa posho wabunge lazima zipatikane.
   
 10. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kinachotuumiza ni sisi wenyewe tunawaruhusu hawa watu kushika madaraka, jamani sio kila mwanaharakati, muongeaji, mtu maarufu , mfanyakazi wa serikali kwa muda mrefu anafaa kua kiongozi na mwanasiasa. Wengine kama mkuu wa kaya walipaswa kua watu wa propaganda, kujichekesha chekesha na kupiga vijembe. Kuna think tankers, wazee wa maamuzi magumu na utawajua tu hata kama hawana dini wana tabia safi kabisa sio wapayukaji, wakujirusha, mizaha ya kijinga jinga hata usela na maneno ya mtaani ni nadra kwao. Mfano John Mnyika, Vicent Nyerere, Deo Filukunjombe, Bashe.
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Matumizi yasiyo ya lazima ni yapi hayo na nani anayeamua kuwa matumizi fulani ni ya lazima na mengine siyo na kwa sababu zipi? Kwa mfano, matumizi kwa ajili ya vazi la taifa ni ya lazima?
   
 12. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  mkuu nakuunga mkono sana, tunaongozwa na majua, yeye anasema ivyo wakati kwa nafasi yake anatakiwa kutoa way forward, yani tunaongozwa na majua na ni majua wa kutupwa, hali zinazidi kuwa mbaya kila kukicha,
  lakini hali inapokuwa mbaya sana kiasi hiki ni dhahiri very soon solution is just around the corner, ngoja watuwekee katiba yetu vizuri then our voice will be held
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mh Zitto aliliona hili kale yule **** wa fedha alipinga
   
 14. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Zito Kabwe alishasema muda mrefu lakini walibisha na kukana sana... Mustafa Mkulo unakumbuka mlivyokana? Haya, kaneni na maneno ya pinda. Kweli mficha maladhi kifo humuumbua. Kukana ni kawaida yenu, mnakumbuka .... Zanzibar kujiunga na OIC, Loliondo kuuzwa vyote hivyo mlikana sana na mkalifungia lile gazeti (MOTOMOTO) lililotoa habari hizo. Lakini mwisho wa siku hayo yote yalionekana ni kweli....
   
 15. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sasa serikali yake inafanya nini kama jitihada zote walizofanya zimmekwama si waachie madaraka kwa wengine ili wajifunze! Rais mwenyewe ana digrii ya uchumi lkn hakuna lolote, waziri mkuu naye chaulizi, halafu posho kwa wabunge wameendelea kulipana zile nyongeza ila wamekubaliana yeyote asitoe siri awe magamba au upinzani. Nchi hiiiiiiii!!!
   
 16. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280

  Sidhani!
   
 17. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kobello unanishangaza kila siku! Kuna siku unachanganua mambo "viswano" ila wakati mwingine mhhh!
   
 18. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kutodhani kwako kunabadilisha hali halisi iliyopo na ambayo hata kichaa anaiona?
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Haijaanza leo, hii nchi imefirisika toka miaka miwili tu ya utawala wa Kikwete sema kwasasa tumefikia pabaya, na bado inasemekana ana hamu ya kuendelea mpaka amalizie kipindi chake alicho pewa na Usalama wa Taifa na Tume (Tusipoandamana ajiuzuru au jeshi lisipompindua)
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sie wengine na Zitto tulishasema technically serikali ilikuwa imefulia since March, 2011 . Jamaa wametubishia. Badala ya kuwaambia wizara wafunge mkanda ningeliwashauri wafanye yafuatayo:-
  a. Tunaona katika report ya CAG kuwa kunatokea upotevu wa fedha za serikali kwenye taasisi za serikali kila mwaka. Hizi pesa zinakisiwa kuwa kila mara zinakaribia kufikia Trillioni 1. Hizo ni pesa nyingi sana serikali inabidi kuamka na kulidhibiti hilo.

  b. Wapunguze matumizi yasiyo ya msingi semina, short course, vikao vya wakurugenzi vipungue. Mashangingi wauze kusave hela wanunue vitara, rav-4 kupunguza gharama.
   
Loading...