Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

si ajabu rais anataka waanze kufanya uchunguzi kama kawaida watasema wanaunda kamati. kweli kuna haja ya mambo yote yaongozwe na katiba ya nchi si mtu moja.


Atakuwa kaambiwa atulize mambo ikiwezekana ajaribu kuchakachua akili za wabunge bajeti ipite.

kwa vyovyote atakuwa amemwambia kuwa hata yeye anahusika.

nchi hii hatuna head of state....



Anaposema mapya ni dhahiri sasa ni tofauti na lile lake la kumfukuza mara moja, na anaenda mbali zaidi kusema wanalifanyia kazi ina maana linahitaji muda si kam alivyosema kuwa kama ni yeye alikuwa ni kutamka tu! Mara moja. Swali linalobaki gizani ni mapya yapi hayo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi?

Kama ingelikuwa ni kumchunguza ni lazima wangemsimamisha kazi mara moja ili uchunguzi uanze, hivyo nachelea kusema kuwa wana mchunguza! Kama ni kujuwa wahusika wote hili wachukuliwe hatua kwa pamoja nadhani pia hisinge zuia yeye kusimamishwa kazi na kuchukuliwa maelezo na katika maelezo yake ndipo uchunguzi wa mwanzo unge baini njia ya kutambuwa walio nyuma yake.

Hivyo basi ni dhahiri wanatafuta jinsi ya kuchakachuwa hili jambo! au wanataka kummaliza aondoke na ushahidi wote? sidhani au wanataka kumuamisha haraka hili kumuepusha na janga ya kuzee kichaa, maana nimemuona kama mzee vile akifukuzwa leo Penshen ya Katibu Mkuu ambayo ndugu yake na Swahiba wake alikuwa anamtafutia hataipata! kwahiyo nadhani wanataka awe katibu Mkuu Mstafuu kama kawaida ya CCM badala ya Mtuhumiwa! This is fine watakuwa wamemsaidia sana, ila wajuwe kila upuuza watakaofanya katika hili jambo litakuwa Milestone ya kuikaanga CCM, waamue ama kuisaidia Chama au Mpuuzi mmoja!

Labda wanataka kubadili baraza la mawaziri kwahiyo kampa kazi ya kuunda jipya akija walifanyie kazi na kulitangaza? Hili litakuwa wazo zuri sana, lakini watapata wapi watu maana Wabunge wa CCM ni wale wale. Myt: wote hovyo wote Posho na Rushwa, wazo zuri lakini siyo feasible; Pole sana Kikwete, haya ni madhara ya kuchakachuwa wagombea ubunge majimboni, itabidi CCM kama si sikio la kufa ijifunze kuanzia hapa maana najuwa ni kazi ngumu sana kupata watu safi wenyewe uwezo wa kuongoza wizara zote zilizopo kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM waliopo sasa, kazi ngumu sana labda waunganishe baadhi ya wizara.

Pinda tunasubiri, Muhimu waandishi wa habari warudi wamuulize tusubiri hadi lini?
 
Watanzania tumeliwa kekundu!!!!! haha ha ha ha ha ha ha ha n.k......
 
Hata kama Ngeleja na Naibu wake walikuwa hawajui kilichotokea, wao watabidi kuwajibika kisiasa . Hatuwezi kukubali usemi kuwa alikuwa hawajui. Mwinyi na wenzake Kina Kisumo walijiuzulu kwa makosa ambayo wao (kiukweli) walikuwa hawajui.
Hivi itakuaje maelekezo yanatolewa kuwa ukisha deposit wa inform DAP. Inaonyesha kuwa admin ya wizara ilikuwa wanafahamu mpango huu.
21 CEO chini ya wizara yake , hata mmoja asimuulize??
 
Hayo mambo yanatendeka miaka yote, safari hii kuna watu wamekosa mgao. Mama Shelukindo analijua hilo sana kwa sababu mme wake alikuwa ni M/kiti wa kamati hiyo miaka 5 iliyopita; naye alikuwa anapata mgao kupitia mr. wake. Leo hii mr. wake hayupo mjengoni kwa hiyo mgao haumfikii ndo maana akalipuka!
 

Unaweza kufa kwa kihoro kama sio BP ukijua vipaumbele vyake!! nchi yetu inatia aibu ukianza na kiongozi wa Juu hadi wa mwisho wao kila jambo ni kanyaga twende hakuna jambo lenye umihimu kwao wala kipaumbele zaidi ya nafsi zao inakera sana but dawa yako iko jikoni inachemka ikiwiva tu watakiona cha moto!!
 


kwa kujua kwako kuwa huu upuuzi ulikuwa unatendeka miaka yote, ukaminya; utakuwa mmoja wao au uwajibike kwa kunyamazia uovu.

Amandla.
 
Swali zito hili. Kinahitajika chombo zaidi ya rais kuamua hili.
Katiba.
Pamoja na matobo yake.
Walau itumike basi.
 
wala sitashangaa, ukiona Jairo na Waziri wake wakaendelea tu kuifisadi nchi yetu, na wala hakuna la kufanyiwa! Hawako peke yao.............
 
maagizo mapya ina maana ni yale yanayoenda kinyume na mpango uliokuwepo wa kumfukuza kazi Jairo.
 
Kuomtoa kafara Jairo mwenyewe ni kosa maana kwa ufahamu wangu mdogo sana katibu mkuu hawezi chukua maamuzi mazito kama hayo bila ya mabosi zake kujua pamoja na hazina kwa maana hiyo basi Ngeleja,Malima na Mkulo wapo kwenye channel moja 50milioni kwa kila wizara 21 zilizo chini ya wizara ya nishati sio hela ndogo jamani!! hatakama wao wataona ni ndogo vipi wakaguzi wetu wanapopita kukakua watasema zimetumika kwa matumizi yapi Chai ama Soda za wageni???

Hii chaneli ni ndefu tusiiangalie kijuu juu tu tujaribu kuangalia kwa mapana zaidi tukiamua kuchunguza ndani zaidi waweza kuta hata CAG naye yumo kwenye mkumbo maana hii nchi imeoza, na pengine hata wizara nyingine wanatumia mkumbo huo huo wa kina Jairo kupitisha bajeti zao.

Sitoshangaa kumsikia JK akimkingia kifua Jairo mbali yakuwa ni maswaiba bali ni kuficha aibu ya kuumbua wengi kwa maana nyingine Jairo nikama kidagaa tu baharini kuna MIJISAMAKI mikubwa iko pembeni inasikilizia kinachoendelea.
 
Wana msemo wao siku hizi eti kelele za mbu haimzuii mtu kulala
 
Acheni kumsumbua JK wangu bado anakula bata kwa Madiba, Yaani akose utamu wa pilau la Sauz kisa wabongo?

Kwanza mimi ninavyomuelewa atasema angalieni msifanye uamuzi utakaowanufaisha wapinzani
 
HABARI ZA KUAMINIKA

JAIRO AMEJIUZURU WADHIFA WAKE .................

mchana huu.....
 
Mi nilijua tu hapa tutapigiwa danadana alaf linapita, Jairo ataendelea kuwas katibu mkuu, si unajua tena mabo ya Magamba, kila kitu utasikia uchunguzi unafanywa, uchunguzi wa nn wakat jambo liko waz? mi nahis huu mchezo mtoto wa mkulima alikuwa haujui ndo maana akataka amfukuze yy lakin mkubwa wake inawezekana ndo alimwambia Jairo afanye mambo ndo maana akamwambia PM asimfukuze
 
Hivi Rais anaposafiri hakuna anayekaimu? Au hamuamini daktari mwenzie!??? Any way, inawezekana mtoto wa mkulima aliingia kichwa kichwa hakujua kwamba katika sakata hili na mzee mzima anahusika. Hapa ndipo tunapomkumbuka Lowassa.
 



na HABARI ZA UHAKIKA TAYARI AMEACHIA NGAZI MCHANA HUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…