Pinda na Mawaziri wanaonewa

kwanza hili la kujiuzulu tu mi nnawasiwasi itaeeenda wee afu watazoea nalo yaani mtu aatakuwa anavurugavuruga akijua mbina ntajiuzulu tu.....mi naona cha msingi hapa ifike mahali licha ya kujiuzulu....wawe wanafilisiwa mali zao zote na kutiwa ndani....full stop!!
 
Ni kweli chanzo cha matatizo ni uongozi mbaya wa kikwete, kulinda wezi, kutokemea uzembe, usimamizi mbovu wa maliasili nk. Lakini tunapaswa tuanzie mahali fulani, hawa mawaziri wanatumia za loophole zilizopo kwenye uongozi wa kikwete kutowajibika ipasavyo na kuendeleza ufisadi. Inabidi wafukuzwe ili kounyesha kwamba wananchi hatufurahii hapa walipotufikisha. Hii ni wakati tunajipanga nini kifanyike kuhusu kikwete, maana kwa kweli 2015 ni mbali, kwa hali tunayoendanayo tusipofanya maamuzi magumu tutafika chamoto tukiwa tumekiona, na atatuachia madeni ambayo kurecover itatuchukua muda.
 
yaani mtu mmoja tu? Asumbue vichwa? Tena asumbue serikali? Nao wanamwangalia tu kama hawabenefit? Na ikiwa hivyo kazi ya TISS ni nini tena?
 
Alisema Dr Slaa katika kampeni za uchaguzi mkuu 2010 kwamba, "Kumchagua Kikwete katika ucaguzi huu ni janga la Taifa."
Matatizo yote ya Tanzania yanasababishwa na Kikwete alias chaguo la mafisadi.
 
yaani mtu mmoja tu? Asumbue vichwa? Tena asumbue serikali? Nao wanamwangalia tu kama hawabenefit? Na ikiwa hivyo kazi ya TISS ni nini tena?

Tatizo ni mfumo wa kutowajibishana, ule mfumo wa utwa na utwana haujaondoka. Presda yuko juu ya kila kitu na sheria ni kivuli tu kwake.
 
Tujiulize, hivi kiranja mkuu anafanya nini na zile orodha kede alizonazo (Wahujumu uchumi, wafanya biashara ya madawa ya kulevya, watuhumiwa wa RADA, ........) kwa zaidi ya miaka 5???!!!!
Hizi si dalili za wazi kwamba yanamkwama kwa sababu anahusika???
Kweli nawaambieni, hata kurudi pale "mahali patakatifu" kwa mara ya pili, ni kutokana na ubovu wa katiba yetu, ujinga wa wananchi tuliowengi(ambao ndio mtaji mkubwa wa Chama Chawala) na ubinafsi na unafiki wa wasomi wa nchi yetu.
Kiranja mkuu na Chama chake ndiyo sumu na adui mkuu wa nchi yetu. TUAMKE!!!
Japo kuna ugumu kuwaondoa (hawatakubali kirahisi), lazima tufanye kazi bila kuchoka hadi tuwatoe!!
Wasipotolewewa, tutakufa sisi.
Kila siku watakuwa wanabadili mbinu na kutuletea maneno matamu yasiyo na tija.
Tukizubaa, watafuna zaidi, wanapata uwezo zaidi wa kyumbisha vyo vyetu vya haki kwa kutumia rushwa, vitisho na mabavu.
Moja ya sera zao maarufu ni kulindana.
Tumeshudia wasafi miongoni mwao, wakijaribu kusafisha mfumo na kukandamizwa hata kuhatarisha UHAI WAO! Sisi watanzania ni mashujaa, tusiogope kakundi ka WADHALIMU kanakojibandika sura ya serikali(a group of colluding rooters, in the dress of a government).
 
Kuna kigogo anayehusika na kuyumbisha nchi, hawa ni matawi tu. Sitegemei katika familia mtoto afanye kitu kinyume cha matakwa ya mkuu wa kaya. Yaliyompata Edward Lowasa ndiyo yanayowapata hawa sasa hivi. Kama Lowasa aliharibu nchi, je baada ya kuachia ngazi nini kinaendelea? Mbona mbaya zaidi kuliko wakati wa Lowasa katika ufujaji wa mali ya umma na usimamizi duni kabisa katika shughuli za serikali na mali ya umma?

Kuna mtu kaniambia Brazili kuna totoz si mchezo
 
Hakuna anayeonewa unafiki mtupu!! Mara ngapi Pinda "anavuliwa" nguo na bosi wake alafu anakaaa kushangaa???? Yanayompata yanasitahili na ameyatengeneza mwenyewe kama vipi aachie ngazi kwani nini? Kama kufa mtu anazaliwa siku moja na anakufa siku moja. Bora kufa shujaa,,,,ala!!!
 
Tujiulize, hivi kiranja mkuu anafanya nini na zile orodha kede alizonazo (Wahujumu uchumi, wafanya biashara ya madawa ya kulevya, watuhumiwa wa RADA, ........) kwa zaidi ya miaka 5???!!!!
Hizi si dalili za wazi kwamba yanamkwama kwa sababu anahusika???
Kweli nawaambieni, hata kurudi pale "mahali patakatifu" kwa mara ya pili, ni kutokana na ubovu wa katiba yetu, ujinga wa wananchi tuliowengi(ambao ndio mtaji mkubwa wa Chama Chawala) na ubinafsi na unafiki wa wasomi wa nchi yetu.
Kiranja mkuu na Chama chake ndiyo sumu na adui mkuu wa nchi yetu. TUAMKE!!!
Japo kuna ugumu kuwaondoa (hawatakubali kirahisi), lazima tufanye kazi bila kuchoka hadi tuwatoe!!
Wasipotolewewa, tutakufa sisi.
Kila siku watakuwa wanabadili mbinu na kutuletea maneno matamu yasiyo na tija.
Tukizubaa, watafuna zaidi, wanapata uwezo zaidi wa kyumbisha vyo vyetu vya haki kwa kutumia rushwa, vitisho na mabavu.
Moja ya sera zao maarufu ni kulindana.
Tumeshudia wasafi miongoni mwao, wakijaribu kusafisha mfumo na kukandamizwa hata kuhatarisha UHAI WAO! Sisi watanzania ni mashujaa, tusiogope kakundi ka WADHALIMU kanakojibandika sura ya serikali(a group of colluding rooters, in the dress of a government).

Wabunge wanahaha kila kukicha na kufunua uchafu unaotoka huko huko aliko mkuu halafu anaishia kunyamaza na kuwafumbia macho, sasa nani mwenye kulaumiwa?

Baada ya kufikiri sana nimeona Mtoto wa Mkulima amebeba lawama za Mkulu, nikikumbuka sakala la Jairo alishasema angekuwa yeye angetoa uamuzi pale pale, lakini kwa kuwa watu hao ni wa Mkulu. Na matokeo danadala lilotokea lilihitimishwa na tishio la Wabunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali ndipo aliporidhia kumweka kando ili uchunguzi ufanyike. Wote huu ni usanii wa Mkulu mwenyewe, hawa mawaziri ni victims. Hatuwezi kuwalaumu mno kwa vile wameachiwa wale watakavyo na wanakingiwa kifua na Ikulu. Wanatushangaa tunavyolalamika. Wachache tu wenye uchungu wamebaki na dhamiri yao safi kutojihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Alisema Dr Slaa katika kampeni za uchaguzi mkuu 2010 kwamba, "Kumchagua Kikwete katika ucaguzi huu ni janga la Taifa."
Matatizo yote ya Tanzania yanasababishwa na Kikwete alias chaguo la mafisadi.

Umenikumbusha na una kumbukumbu nzuri sana BAK, ukweli ndio umejidhihirisha sasa.
 
Kuna mtu kaniambia Brazili kuna totoz si mchezo

Hajakosea kukuambia hivyo, kwani kule kuna totoz za kichotara, chotara wa kizungu na chotala wa latin America, aka spanish chotara kama wala wa Cuba. Amini mwenye moyo mchache anateleza. Hata kama first lady yupo anaweza zungukwa maana mambo haya ni mipangilio ya kisayanzi na mbinu za kisanii.
 
Mie nilivyoambiwa hivyo, nkachukua akili za kuambiwa nikachanganya na zangu nkajua ndo zili zile safari za kutimiza ndoto za ujanani (fantancy)
 
""SIKUBALIANI MAWAZIRI KUJIUZULU TU! TWENDENI MBELE ZAIDI YA HAPO!!""

Ni Hatari kuamini kwamba kujiuzulu kwa mawaziri wa kIKWETE ni suluhisho kwa matatizo yanayotukabili watanzania.
Nilazima tulitafute na kutambua tatizo la msingi kisha tuchukuwe hatua sisi wenyewe. Tujiulize wamejiuzulu wangapi tangu huyu bwana kikwete achukue hii nchi. tulifaidikaje na kujiuzulu kwao? Tatizo la msingi ni Kikwete na hatunabudi sisi wenyewe kumuondoa kwani yeye ndiye aliye prove failure kwani uwezo wake ni mdogo ndio sababu akashindwa kuwachagua wasaidizi wake wazuri.
sitaki kuamini kwamba tanzannia hakuna watu wenye uwezo mzuri! kwa maana hiyo tuandamane tumtoe huyu asiye na uwezo tuliye mkabidhi dhamana kusimamia seria za nchii hii na hatiamaye ameshindwa.
Tukijitokeza vijana elfu moja kila wilaya ya Tanzania hii tukakutana Dar naamini atatuelewa kwasababu hataki kuwaelewa wabunge wetu twendeni wenyewe atatusikia atatuelewa na ataondoka na hatimae tutatafuta mwingine mwenye uwezo mzuri zaidi kuliko yeye na hao wa kwake.
TUJIRIDHISHE!, TUJIPANGE! TUCHUKUE HATUA KWA FAIDA YETU SISI NA KIZAZI CHETU KIJACHO!

Back
Top Bottom