Pinda kushitakiwa kwa kauli zake tata "wapigwe"

Huko ni kudilisika kimawazo. Huyu Pinda si ndiye mliyekuwa mnamwita mpole mdhaifu. Halafu kumbukeni kuwa kauli ile katoa ndani ya ukumbi wa Bunge ambao una kinga kisheria. Vinginevyo waache wauze tu sura na wao wajipatie kipato
Hilo la kauli kuitolea bungeni..
sijui kinga ya woteva..
watajibu mahakamani.
Cha muhimu Pinda kafikishwa mahakamani kwa kauli zake za kikatili, kiuaji...
hata mahakama ikitupia hilo shitaka., rekodi haitatupwa.
 
mbona mi ni chadema lakin ni mnyaturu,vp zito,wenje,sugu,msigwa,slaa, n.k usichangie post kiukabila.

na safari pia ni mchaga,
na baregu
na marando,
na watanzania wooooote ni wachaga.
Hujaelewa tafsiri yake ya "wachaga".
 
na safari pia ni mchaga,
na baregu
na marando,
na watanzania wooooote ni wachaga.
Hujaelewa tafsiri yake ya "wachaga".

Watanzania walio wengi siyo wachaga. Na ndiyo maana Mrema hakuingia magogoni. Na ndiyo maana pia mbowe na chama chake binafsi kipo kwenye upinzani. Na ndiyo maana kitaendelea kuwa chama cha upinzani. Mpaka pale watanzania watakaporidhika kwamba ni chama cha kitaifa. Na hii ni baada ya uongozi wa chama na wagombea wake kuweza kuchaguliwa na wanachama badala ya kuteuliwa na freeman mboye.
 
Ujiulize mwenyewe kwamba mtumiwa anapigwa au anafikishwa kwenye vyombo vya sheria? Yeye Pinda aliposema "wapigwe, tumechoka sasa". wamechoka yeye na nani, na kwa sababu gani? Fuatilia mada humu jamvini, kwamba JWTZ yawateka watu wanne waliokuwa wanashangilia mjadala wa juzi - ITV ambapo JWTZ walitumumiwa kwa kuwafanyia watu vitendo vya kinyama. Kwa hiyo anayeshangilia apigwe tu?

Ukumbuke kauli za Pinda zenye maelekeo ya serikali kujichukulia sheria siyo kitu cha mara ya kwanza. Hata wakati wa mauaji ya albino alisema wauaji wa albino wauawe badala ya kusema washtakiwe. Kama hukumu ndiyo itakayosema wanyongwe hadi kufa ni sawa lakini siyo kiongozi (ambaye siyo hakimu) hana mamlaka ya kusema wauwe.
Usikwepe kujibu swali ambalo unajua jibu lake.
Anayetazamiwa KUPIGWA ni yule mleta fujo, muandamanaji ovyo, asiyetii amri halali, na hata mdharau mamlaka.
Kama wewe umo katika kundi hilo subiri kisago , maana kwa uhakika kitakujia.
Usijiingize ndani ya kundi la kondoo ilhali wajifahamu kuwa wewe ni chui mrarua amani nchini.
Pengine uelewe vile vile kuwa HAKUNA sheria itakayokupa kinga wakati unararuriwa ukifanya vitendo vilivyo kinyume na ustaarabu wa amani ya nchi.
 
Usikwepe kujibu swali ambalo unajua jibu lake.
Anayetazamiwa KUPIGWA ni yule mleta fujo, muandamanaji ovyo, asiyetii amri halali, na hata mdharau mamlaka.
Kama wewe umo katika kundi hilo subiri kisago , maana kwa uhakika kitakujia.
Usijiingize ndani ya kundi la kondoo ilhali wajifahamu kuwa wewe ni chui mrarua amani nchini.
Pengine uelewe vile vile kuwa HAKUNA sheria itakayokupa kinga wakati unararuriwa ukifanya vitendo vilivyo kinyume na ustaarabu wa amani ya nchi.

Mkuu, hata kule shuleni walimu hawachapi wanafunzi watiifu isipokuwa watukutu. hivyo kama wakiandamana ilhali maandamano hayo hayana kibali cha polisi, kupigwa kwao ni haki yao maana hata wakipelekwa mahakamani wanaachiwa tu. si unajua mahakama zetu zilivyo dhaifu kwa sasa hususan katika kesi za wanasiasa?
 
nawaza kweli kama hawa jama watafanikiwa?. mana mweshimiwa anajua kwa nini amesema na na hisi anajua kivipi atashinda. ngoja tuone hili gemu litaishiaje.
 
ni lazima tujiulize kiongozi kama pinda kutoa kauli za kuvunja haki za binadamu?????????????????hapa kuna mambo mawili 1. hana chembe ya damu ya mtanzania 2. hakulelewa na wazazi hivyo hana malezi ya kuelekezwa kujali binadamu wenzake.
 
Pinda hana msimamo na ameokuwa akitoa kauli zisizo na mwelekeo na tata kijamii.kauli zake za piga ua vunja na hata zile za wanaoua albino nao wauliwe
 
Kuna haja gani ya kushtakiwa wakati yeye ni muuaji na kaagiza kupiga hadi kuua? Si afungwe tu? Tumechoshwa na ubabe wa waccm na magamba yao pinda wakati umemwishia kiutawala ndo mana kila kchwapo anakosea anaropoka sana PIA IKUMBUKWE KUWA LWAKATARE ALISHTAKIWA KWA KOSA LA KUPANGA KUTENDA TENDO OVU,JE INAKUWAJE KWA ANAYEAGIZA KUTEKELEAZA TENDO OVU?KUPANGA vs KUAGIZA
 
Back
Top Bottom