Kwa kauli aliyotoa Pinda jana bungeni, inatosha kabisa pasi na shaka kukosa vigezo vya kugombea nafasi ya juu kabisa ya kuongoza nchi hii.
Nasema hivyo kwa sababu ameonekana wazi wazi kutoka kuzima jambo hili kwa maslahi binafsi ama yeye mwenyewe au kulinda kundi la watu waalifu na wezi.
Kwa nchi yenye watu makini swali ni moja tu, kama kwa nafasi yake kwa waziri mkuu na matarajio yake ya urais ameweza kudiriki kufanya vile je akipewa nafasi hiyo kubwa ataficha maovu mangapi na wakati huo atakuwa na rungu la kufanya hivyo?
Pinda umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati kweli? Natamani ungejua sisi wananchi tunakuonaje huku kitaa.
Hakika umekosa sifa, umekosa upako, umekosa weledi na zaidi umekosa wofu ya Mungu!
Pinda umejitoa mwenyewe katika kinyang'angiro cha urais.
Pinda sasa hata ubunge si halali yako kwani ukifika bungeni unaweza kukosa nafasi ya uwaziri na si hekima kwa mtu aliyekuwa waziri mkuu!
Pinda jana ilikuwa tarehe 20/11/2014 hutasahau tarehe hii!
Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali Andrew Chenge alipewa dola milioni 1 za ESCROW sawa na bilioni 2 kasoro za kitanzania imefahamika.-
Chenge ambae alikua mwanasheria mkuu wa serikali wakati mkataba wa IPTL unasainiwa miaka ya 1990 amekiri kupokea kiasi hicho cha pesa kutoka kwa mwanahisa wa IPTL Rugemalila ambae alikua na hisa 30%. Chenge ambae ni mbunge wa Bariadi amekiri kupokea pesa hizo akidai kuwa ni malipo ya kazi ya ushauri aliyoifanya kwa Rugemalila. Hata hivyo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa mkataba wowote baina ya mwanahisa huyo na Chenge. Mwanasheria aliyekuwa anaishauri na kuiwakilisha IPTL kwa ujumla akiwemo mwanahisa Rugemalila ni Dr. Ringo Tenga ambae alilipwa pesa zake.-
Chenge ambae ni mtu wa karibu sana na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ndiye mtu anayetajwa kuwa chaguo la nafasi ya waziri mkuu ikiwa Lowassa atakua Rais wa Tanzania. Hii ni kutokana na urafiki na mchango mkubwa wa mali na maarifa anaoutoa Chenge katika kusaidia harakati za Lowassa.-
Andrew Chenge ndiye mwalimu wa mwanasheria mkuu wa sasa Jaji Frederick Werema. Wakati Chenge akiwa Mwanasheria mkuu wa Serikali, Jaji Werema alikua afisa wa sheria wa serikali "State Attorney".
Haijajulikana kama malipo hayo ni ya Chenge mwenyewe au ni nani aliye nyuma ya Andrew Chenge. Aidha Haijajulikana kama Chenge hakuwa mchoraji mkuu wa namna gani uporaji huu ufanyike ikizingatia kuwa kashfa nyingi zilizotokea miaka ya karibuni zilitokea yeye akiwa mwanasheria mkuu wa serikali. Hizi ni kama ununuzi wa Rada na Buzwagi.