kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,255
- 16,185
Sikuwahi kufikiria wala kudhani kuwa kamati ya maadili akiwemo rais Kikwete ingewaona Membe, January, Asha Migiro, Magufuli na Amina walioingia 5 bora ya CCM katika kinyang'anyilo cha kumsaka mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM ni wasafi, wachapakazi, waadilifu na waaminifu kwa taifa letu kuwazidi hata Pinda, Bilali, Sitta, Wasira, Mwakyembe, Jaji Ramadhani na Mwingulu wasaidizi na washauri wakubwa wa rais.
Binafsi niliogopa sana kuona nchi inaongozwa na watu wasioaminika kiasi hiki, lakini niliogopa zaidi kuona rais anasaidiwa na watu asiowaamini kwa kiasi hiki. Kisiki cha watendaji wake wakuu hawa kingekuwa CC, NEC na mkutano mkuu na sio kwenye ngazi ya awali ya kamati ya maadili ambayo na rais ni mjumbe wake na mdau muhimu.
Kama wasaidizi wake hao walikuwa wana mafaili machafu kwanini hakuwaambia mapema kinagaubaga ili waache kutangaza nia ili kuwaepushia kupata aibu kama waliyoipata mbele ya wananchi ya kushindwa hata na mtoto mdogo kama January Makamba kwa uadilifu? Lakini ni kweli Asha Migiro ni mchapakazi na mwaminifu kuliko Pinda, Bilali, Mwakyembe, Sitta na Wasira? kwani kafanya nini kikubwa mno kwenye taifa hili kuwazidi Bilali, Pinda, Mwakyembe, Sitta na Wasira?
Huu ni udhalilishaji wa wazee wetu hawa wakuu ambao nao Kama mzee Kingunge hawana budi kutoa neno japo moja kwa wananchi ili kusafisha makoo yao. Kitaaluma kutoa dukuduku hadharani (mental ventilation) kunaongeza afya ya mtu kuliko kunyamaza na dukuduku moyoni. Wakikaa kimya namna hii ni dalili tosha za wazi kuwa kweli ni wachafu na wasioaminika kupewa urais kama kamati yao ya maadili ilivyoona, hivyo waondoke wapishe wengine waliosafi kwa taifa.