Pinda aumbuliwa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda aumbuliwa bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 13, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ZIARA iliyofanywa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imezua tafrani jana baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili (CHADEMA), kudai kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo aliwakamata na kuwaweka ndani watendaji wa vijiji kwa kushindwa kutoa mbuzi kama zawadi kwa waziri huyo.

  Wakati akiuliza swali bungeni, bila kutaja jina, Kamili alisema mkuu huyo wa wilaya alifanya hivyo, baada ya watendaji hao kushindwa kuchangia mbuzi tisa kwa Waziri Mkuu, aliyefanya ziara mkoani humo Februari 23, mwaka huu.

  Hata hivyo, aliyekuwa mkuu wa wilaya wakati huo, ni Kapteni mstaafu, James Yamungu ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara.

  Swali la mbunge huyo lilimfanya Waziri Pinda, kuduwaa huku akiwa ameshika tama, na kuzua minong'ono na miguno kutoka kwa wabunge wengi.

  "Mheshimiwa Spika, ninahitaji ufafanuzi wa kisheria kwa hili la baadhi ya ma-DC, ambapo huwaagiza watendaji kufanya mambo kinyume cha sheria na pindi wasipofanya huwaweka ndani kwa muda wa siku saba.

  "Na mfano halisi ni hili lililotokea wilayani Maswa, katika ziara ya Waziri Mkuu Februari mwaka huu, katika Mkoa wa Shinyanga, ambapo mkuu huyo wa wilaya aliwaweka ndani watendaji wa kata kwa kushindwa kukusanya mbuzi tisa kwa ajili ya zawadi kwa Waziri Mkuu."

  Swali hili lilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumtaka mbunge huyo kuthibitisha kwa ushahidi kutokana na jambo hilo kugusa hisia kali kwa Bunge na taifa kwa ujumla, hivyo kutaka kuleta ushahidi.

  Mbunge huyo alisema kuwa anao ushahidi, na kwamba hata jambo hilo lilitangazwa na baadhi ya runinga hapa nchini, hoja ambayo hata hivyo ilionekana kuwa nyepesi kiasi cha Spika Makinda, kuwataka wabunge kuwa makini katika maswali na hoja wanazozitoa bungeni.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri, alisema serikali haijawahi kumwagiza mtendaji yeyote wa serikali kuchangisha wananchi kwa nguvu katika ziara za viongozi wa juu wa serikali.

  Hata hivyo, alisema hoja ya mbunge huyo si ngeni kwani iliwahi kuibuliwa na ikamlazimu aliyekuwa Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika, kwenda hadi Maswa kuzungumza na wananchi ili kupata maelezo ya kina.

  "Baada ya kufanya mkutano na wananchi hao, ilibainika kwamba si la kweli. Lakini kama mbunge ana ushahidi mpya tunamuomba atuletee na huyo DC tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria," alisema Mwanri.

  Alifafanua kuwa wakuu wa mikoa na wilaya wana haki ya kuingilia kati utendaji wa ngazi za chini, zikiwemo halmashauri, ikiwa tu kuna hatari ya usalama ama mali ya taifa, vinginevyo hawaruhusiwi kuzuia ama kutoa maelezo mengine nje ya maamuzi sahihi ya kisera na kikanuni yaliyoamriwa na mamlaka za halmashauri za miji ama vijiji.

  "Majukumu ya Mkuu wa Wilaya yametajwa katika kifungu namba 14, 1 hadi 3 cha sheria za Serikali za Mikoa namba 19 ya mwaka 1997 kwamba yeye ndiye msimamizi mkuu wa serikali katika wilaya yake.


  Concern
  Hapo ni waziri mkuu je na rais huwa inakuwaje
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  ndio ukweli

  kuna waganga wa wilaya wanalazimika kuruhusu bajeti za afya kusaidia mbio za mwenge au hata kulipia ubwabwa wa wanasiasa
   
 3. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni habari ya kushtua kusikia Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda a.k.a mtoto wa mkulima amewakamua watoto wa wakulima wenzake tena wanaotumia jembe la mkono wilayani Maswa kwa kuchangisha mbuzi 9 kama zawadi kwake. Haijalishi ni nani aliyemwamuru Ofisa Mtendaji kutafuta mbuzi hao bali hali hiyo imedhihirisha katika ziara za wakubwa hawa zimekuwa zikiendana na kuwakamua wananchi masikini mali zao.

  Hivi kweli kiongozi kama waziri Mkuu anakosa pesa ya kununua mbuzi 9? hadi asubiri wanakijiji walazimishwe kuchanga vijisenti vyao wanavyovipata kwa tabu huku kila siku wakitawaliwa na vifo vya watoto kwa kukosa hata shilingi mia moja ya kununua PANADOL.

  Jamani! Kweli! kwelin Pinda unayafanya haya???

  Mambo haya tumeyazoea kuyaona kwa marais wasiokuwa na haya wala aibu wanapostaafu nyadhifa zao katika Chama na nchi wanachangiwa vitu mbalimbali kila mkoa bila kuhoji mali hizo zimetoka katika fungu lipi la bajeti. Tuliyashuhudia mwaka 2007 wakati Mkapa anaachia Uenyekiti taifa wa CCM.
   
 4. J

  Jadi JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  eti na Mwanri anamlazimisha mbunge alete ushahidi,kweli kazi, wao ndo walitakiwa wamchunguze DC wao,inawezekana huyu DC ni mpya anafikiri TZ bado ipo enzi za ukoloni
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nani kakwambia pinda ni maskini? Unadhani kukusanya mbuzi 9 katika kila kata kwa mikoa yote kuna maskini hapo?
  Ahh pinda Mzee wa Mbuzii kuwa na huruma basi
   
 6. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  duuuuuuuuuuuuuuuee
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Pinda awakamua mbuzi? nilielewa vibaya kumbe ila wote tu ni wezi wanatofautiana tu namna na aina ya wizi
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  niliisikia hii bungeni jana mbunge wa viti maalumu aliibua ni aibu kwa watendaji, waziri mkuu na serikali kwa ujumla
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hivi hili lina tofauti gani na lile la baadhi ya vyama vya siasa kuwakamua wapiga kura kwa kutembeza bakuli eti kwa madai kuwa hawana pesa, wakati tunajua wazi kuwa vinapata ruzuku, misaada toka ndani na nje ya nchi na vyanzo vingine vyingi.
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ZIARA iliyofanywa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imezua tafrani jana baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili (CHADEMA), kudai kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo aliwakamata na kuwaweka ndani watendaji wa vijiji kwa kushindwa kutoa mbuzi kama zawadi kwa waziri huo.Wakati akiuliza swali bungeni, bila kutaja jina, Kamili alisema mkuu huyo wa wilaya alifanya hivyo, baada ya watendaji hao kushindwa kuchangia mbuzi tisa kwa Waziri Mkuu, aliyefanya ziara mkoani humo Februari 23, mwaka huu.Hata hivyo, aliyekuwa mkuu wa wilaya wakati huo, ni Kapteni mstaafu, James Yamungu ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara.Swali la mbunge huyo lilimfanya Waziri Pinda, kuduwaa huku akiwa ameshika tama, na kuzua minong’ono na miguno kutoka kwa wabunge wengi.“Mheshimiwa Spika, ninahitaji ufafanuzi wa kisheria kwa hili la baadhi ya ma-DC, ambapo huwaagiza watendaji kufanya mambo kinyume cha sheria na pindi wasipofanya huwaweka ndani kwa muda wa siku saba.“Na mfano halisi ni hili lililotokea wilayani Maswa, katika ziara ya Waziri Mkuu Februari mwaka huu, katika Mkoa wa Shinyanga, ambapo mkuu huyo wa wilaya aliwaweka ndani watendaji wa kata kwa kushindwa kukusanya mbuzi tisa kwa ajili ya zawadi kwa Waziri Mkuu.”Swali hili lilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumtaka mbunge huyo kuthibitisha kwa ushahidi kutokana na jambo hilo kugusa hisia kali kwa Bunge na taifa kwa ujumla, hivyo kutaka kuleta ushahidi.Mbunge huyo alisema kuwa anao ushahidi, na kwamba hata jambo hilo lilitangazwa na baadhi ya runinga hapa nchini, hoja ambayo hata hivyo ilionekana kuwa nyepesi kiasi cha Spika Makinda, kuwataka wabunge kuwa makini katika maswali na hoja wanazozitoa bungeni.Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri, alisema serikali haijawahi kumwagiza mtendaji yeyote wa serikali kuchangisha wananchi kwa nguvu katika ziara za viongozi wa juu wa serikali.Hata hivyo, alisema hoja ya mbunge huyo si ngeni kwani iliwahi kuibuliwa na ikamlazimu aliyekuwa Waziri wa Tamisemi, George Mkuchika, kwenda hadi Maswa kuzungumza na wananchi ili kupata maelezo ya kina.“Baada ya kufanya mkutano na wananchi hao, ilibainika kwamba si la kweli. Lakini kama mbunge ana ushahidi mpya tunamuomba atuletee na huyo DC tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria,” alisema Mwanri.Alifafanua kuwa wakuu wa mikoa na wilaya wana haki ya kuingilia kati utendaji wa ngazi za chini, zikiwemo halmashauri, ikiwa tu kuna hatari ya usalama ama mali ya taifa, vinginevyo hawaruhusiwi kuzuia ama kutoa maelezo mengine nje ya maamuzi sahihi ya kisera na kikanuni yaliyoamriwa na mamlaka za halmashauri za miji ama vijiji.“Majukumu ya Mkuu wa Wilaya yametajwa katika kifungu namba 14, 1 hadi 3 cha sheria za Serikali za Mikoa namba 19 ya mwaka 1997 kwamba yeye ndiye msimamizi mkuu wa serikali katika wilaya yake.

  Tanzania daima
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Na wale wanaotembezaga bakuli wakati wa kambeni nao walikuwemo.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Si afadhali za pinda zinafahami zinakwenda wapi, zile zinazochangishwaga kwenye mikutano ya kampeni kwa bakuli huwa zinakwenda wapi jamani?
   
 13. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  najisikia kutukana
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  za pinda huwa zinaenda wapi na hizo wanazo changishwa wakati wakapeni ni hiari au lazima kama ilivyojionyesha kwa pinda
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi kumbe tanzania kuna waziri mkuu?
  au ni jina kama majina mengine?mdogo wangu anaitwa god lakini halina uhusiano na mungu.
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Mmmhh mi si msemaji wa CDM japo ni mwanachama wa CDM
   
 17. k

  kajembe JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Lakini wao wananchi wananchangia kwa hiari tu na kupenda sera zao maana siyo za wizi na kukumbatia mafisadi,wanaonekana ni wakombozi wa kweli! na wala hawafungwi jela wasipotoa!
   
 18. D

  Dabudee Senior Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huko siyo kuchangishwa bali ni kunyang'anywa. Lakini haya ni mambo yanayofanywa bila kificho sehemu nyingi nchini.Uonevu na dhuluma hizi haziwezi kwisha bila magamba kupumzishwa moja kwa moja.
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,389
  Likes Received: 19,678
  Trophy Points: 280
  mbuzi wa kutambika nini hao?
   
 20. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tofauti ni kua hawa wa ccm wamelazimishwa na waliposhindwa kufanya hivyo wakaswekwa ndani, isitoshe hawa wanalazimishwa kumpa waziri mkuu zawadi wakati wale wa M4C huchangia harakati za ukombozi bila shuruti na tena hakuna hatua zozote zinazochukuliwa iwapo mtu hajisikii kuchangia kwa hiari yake.
   
Loading...