Pinda asiwe kondoo wa kafara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda asiwe kondoo wa kafara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Oct 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  21st October 2009

  Si siri kwamba katika miaka ya hivi karibuni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekumbwa na dhoruba nyingi, miongoni mwanzo ni watu wanaohoji mamlaka yake katika baadhi ya mambo.

  Ni kama kumekuwa na kampeni ambayo ilianza chini kwa chini lakini baadaye ikaibuka hadharani juu ya mamlaka ya Serikali ya Muungano juu ya baadhi ya mambo yanayotajwa kuwa ni orodha ya mambo ya Muungano.

  Katika kampeni hizo mengi yamesemwa, kubwa ya yote ni haki ya Zanzibar kujitambulisha kama nchi, kelele zimepigwa hadi kusababisha viongozi mbalimbali kutoa kauli, mmojawapo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juu ya hadhi ya Zanzibar kama ni nchi au la.

  Kwa mujibu wa Pinda, akijibu maswali bungeni mapema mwaka huu, aliweka wazi kwamba Zanzibar haiwezi kujitambulisha kwamba ni nchi kwa sababu kwa uelewa wake nchi ni Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya nchi inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hii ni kauli ya kweli, ya dhati hata kama wapo wanaoichukia. Sheria na katiba ya Tanzania ndivyo inavyotamka. Hakuna nchi inayoweza kuwa nchi mbili kwa wakati mmoja, au sehemu moja ya nchi ikajitangaza kuwa ni nchi huru wakati huo huo ikiwa sehemu ya taifa hilo kubwa.

  Pinda alikuwa mkweli na kwa kweli huo ndio ukweli. Lakini kwa bahati mbaya watu wenye ajenda zao, wamemwandama wakimwelekeza kila aina ya mashambulizi, kwa hekima zake aliliambia Bunge kwamba alikuwa amewaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na yule wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wakae ili kupata tafsri sahihi ya maneno ya Kiingereza ya Nation na State, ambayo yamekuwa yakisababisha kutokuelewana huko.

  Kutokana na ukweli aliousema Pinda, wapo watu walidiriki hata kumkosea adabu kwa kumkejeli, wengine kuthubutu hata kutaka akapimwe akili. Maneno hayo ya ovyo kabisa yalitamkwa ndani ya vikao vya Baraza la Wawakilishi, yaani na viongozi ambao si tu wana wajibu wa kulinda na kuheshimu sheria za nchi, lakini pia kuonyesha utii kwa viongozi wa dola walioko madarakani kwa sababu hata na wao ni sehemu ya mfumo huo wanaoutukana!

  Jana kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hili tulikuwa na habari iliyozungumzia malalamiko ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Kamati ya Mwinyi, ambayo iliundwa kuchunguza chanzo cha chuki miongoni mwa wabunge wa CCM na Wakilishi baina yao na dhidi ya serikali yao.

  Malalamiko hayo yalielekezwa kwa Pinda kwamba amekuwa akiwakera kwa kauli zake ndiyo maana wamekuwa wakitoa kauli kali kali za kumbeza na pengine kuashiria kutoweka kwa maelewano baina ya wajumbe hao na kiongozi huyo.

  Sisi tunasema kauli za Wawakilishi hawa ni za bahati mbaya. Kumbebesha Pinda lawama ni kukwepa wajibu; hatuoni chochote kinachostahili Pinda kubebeshwa lawama kwa suala la hadhi ya Zanzibar.

  Alichosema Pinda ndio ukweli wa kisheria kuhusu hadhi ya Zanzibar. Kama hadhi hiyo haiwafurahishi baadhi ya wawakilishi dawa si kumkejeli na kumtwisha mzigo usio wake Pinda.

  Kufanya hivyo si tu kuwa ni kumuonea, ila ni kutafuta visingizio ambavyo havina nguvu katika suala nyeti, tete na zito kama makubaliano ya Muungano.

  Rais Kikwete alipata kusema kelele hizi za hadhi ya Zanzibar za sasa zina nini? Alitaka wenye jambo lao waliseme, lakini wasijifiche nyuma ya hadhi ya Zanzibar na kulalamika ni nchi au si nchi.

  Nasi leo baada ya kuona kwamba sasa Pinda ndiye amegeuza fuko la kujifunzia masumbwi, tunasema hapana. Hapana, si vema wala haki kumbebesha lawama zozote katika hili; hajawa chanzo cha hisia hizi dhidi ya Muungano, ila watu wanatafuta pa kutokea tu.

  Ni kwa maana hii tunafikiri kama kuna watu ndani ya visiwa vya Zanzibar wanaodhani wamechoka ndani ya mfumo wa Muungano, ni vema na haki kabisa wakajitokeza hadharani na kusema hivyo. Wawe na ujasiri watoke vifua mbele ili wahesabike kuwa ni wakweli wa dhamira zao, kuliko kujaribu kutafuta visingizo ambavyo haviwasaidii kutimiza hicho wanachokusudia.

  Tumesimama wazi kumtetea Pinda kwa sababu moja tu, alichosema bungeni juu ya hadhi ya Zanzibar na mambo mengine yoyote juu ya mambo ya Muungano ni sahihi kwa sababu ndivyo sheria inavyosema hadi sasa.

  Hakuna sababu yoyote ya msingi na wala si haki kumgeuza Waziri Mkuu huyu kondoo wa kafara. Mwacheni Pinda achape kazi!


  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. w

  wasp JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Mheshimiwa Peter Kayanza Pinda. Hata International Law inasema hivyo. Wenye chuki na wajinyonge
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu naye kazidi kuropoka bwana acha wamtoe kafara kama mbuzi wa shughuli
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  eeh kigogo
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teh teh mi ananichanganya sana huyu PM, mara nisivae suti,mara tupande baja ma v8 ni expensive nchi maskini,mara uwa albino ,mara zenji sio nchi,mara ooh kama mnataka si mvunje tu muungano muone..sasa huyu wa nini FirstLady1.in short hana utulivu wa mawazo kwenye kuzungumza mambo ya msingi
   
 6. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nyie ndo walewale......
  Sasa hapo karopoka kitu gani au we ndo unaropoka???
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wanaokerwa na huyu bwana ni kwamba wanaguswa negatively kabisa na kauli zake...huh..i sniff harufu ya ufisadi kwa wanaolalamika!
   
 8. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  hivi wa TZ tunataka kiongozi wa aina gani au mtu afanyaje? wakinyamaza ooh kihiyo, anachekacheka, mjomba kazi haiwezi...akisema anaropokaaa, nguvu ya soda

  kaazi kwelikweli TZ
   
 9. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  unaonekana hufuatilii anachoongea huyo Pinda na mawazo yenu yaliyopinda..ngoja nikuulize wewe kwa niaba yake maana unaonekana ni msaidizi wake..yako wapi matokeo ya kura za albino!!
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na uta sniff sana hiyo harufu ya ufisadi.huwezi ukawa waziri mkuu unatoa matamshi ya kipuuzi..tusivae suti ili iweje?amechangia sh ngapi kwa mimi kununua suti zangu!!!atawaongoza nyie wenye mawazo ya kikulima kama yeye..sisi mabepari haituhusu
   
 12. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Naona wazi kabisa una chuki binafsi na huyu PM! Sasa kama we ni bepari shida yako nini? Nahisi uelewa wako sio kama ambavyo nilidhania mwanzo. Anyway forgive me to say I only see arrogance and ignorance in analysis of crucial issues.

  Step out of the box and think once and forall!!.... Wisen up!?
   
 13. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  watanzania meshawagundua sana tuna kakiji roho ka korosho mtu akiwa anafwata misingi ya haki na sheria basi utaskia anajipenekeza, anazidioropoka Nk...mara nyingine hata mtu anaefanya ufisadi ndo anaonekana mjanja
  watu wakoradhi waaribu mambo kazini ili kiongozi fani asipate sifa..kwa pinda mpaka sasa wazungu wanasema so far so good
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  To hell..my analysis is that he is not qualified and deserve to be a PM.
   
Loading...