Pima udongo katika shamba lako mwenyewe, fahamu njia za kutambua udongo wenye rutuba

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
230
402
NAMNA YA KUTAMBUA UDONGO WAKO

WhatsApp-Image-20160615.jpg

Kupima udongo kwa kutumia vidole

 Chukua sampuli ya udongo kwenye kiganja cha mkono kisha ondoa mizizi, changarawe kubwa kubwa na mabaki ya mimea.

 Kanda udongo kwenye kiganja chako. Kama udongo ni mkavu sana unaweza kuulainisha kwa maji kidogo

 Fikicha udongo kwa kutumia vidole na hakikisha kila kitu kimelainika (pima ugumu); Finyanga mpira (pima uwezo wa kuundwa); zungusha kutengeneza mnyoo kisha kandamiza kurudi chini (pima mnato na uwezo wa kupasuka/kupata ufa).

Udongo wa mfinyanzi:

Mwepesi na unanata sana. Ni rahisi kufinyanga mpira na haupasuki wala kupata ufa, unaweza kutengeneza. Udongo huu unaweza kuunda bonge/donge kubwa na likakauka.

Tifutifu:

Hujishika pamoja lakini hapasuka katika vijipande vidogodogo, chembe za mchanga haziwezi kushikika.

Mchanga:

Chembe za mchanga zinashikika na kuonekana. Udongo haunati na hauwezi kufinyangwa.

Namna ya kupima udongo kwa kutumia chupa ya plastiki.
Mahitaji

1. Chupa za plastiki tatu za saizi inayolingana, zenye mifuniko na zisizokuwa na rangi ili kuweza kuona vilivyomo ndani kwa urahisi.

2. Maji safi

3. Chumvi

Hatua
 Weka udongo ndani ya chupa hadi kufikia theluthi ya chupa.

 Ongeza maji mpaka kufikia theluthi mbili ya chupa.

 Weka chumvi kidogo kisha tikisa chupa kwa nguvu kwa muda wa dakika moja kisha ziache zitulie kwa saa moja.

 Baada ya lisaa limoja, tikisa chupa tena kisha ziache zitulie kwa muda wa masaa manne.

 Baada ya masaa manne udongo utakuwa umejigawa katika matabaka hivyo unaweza kuupima: Tabaka laini kabisa la juu ni mfinyanzi, linalofuatia ni mchangatope, linalofuatia ni mchanga na mwisho kabisa tabaka lenye chengachenga ni changarawe.

 Tafuta asilimia ya kila sehemu ndogo ya udongo (mfinyanzi, mchangatope, mchanga na changarawe) kwa kugawanya unene wa kila tabaka la udongo kwa jumla ya unene wa udongo wote kisha zidisha kwa mia moja (100%).

Snapshot.png

Aina za udongo
Changarawe (gravel): chembe zenye ukubwa wa zaidi ya 2 mm

Mchanga (sand): chembe zenye ukubwa wa zaidi ya 0.02 mm lakini zisizozidi 2 mm

Chembe za mchanga huchukua nafasi ndogo ukilinganisha na mchangatope au mfinyanzi. Uwezo wa kuhifadhi maji ni mdogo sana kwenye mchanga na hali ya utendaji wa kikemia ni ndogo.

Mchangatope (silt): chembe zilizo na ukubwa wa kati ya 0.02 mm na 0.002 mm

Chembe za mchangatope huchukua nafasi kubwa zaidi ya mchanga na zina uwezo mdogo kwenye hali ya utendaji wa kikemia. Mchangatope huathirika kwa urahisi na migandamizo ya vitu vizito hivyo kuathiri uwezo uingizaji wa hewa na mzunguko wa maji kwenye udongo.

Udongo wa mfinyanzi (clay): chembe zisizozidi 0.002 mm

Chembe za udongo wa mfinyanzi huchukuwa nafasi kubwa sana na zina hali kubwa sana ya utendaji wa kikemia. Virutubishi pamoja na maji hujishikisha kwenye huu udongo lakini havipatikani mara zote kwa mimea. Udongo wa mfinyanzi unauwezo wa kutuna na hufaa kuundia vitu mbalimbali kwa sababu ya asili yake ya kunata.

Mchanganyiko wa mchanga, mchangatope na udongo wa mfinyanzi huleta udongo tifutifu (loam) wenye rutuba. Udongo huu ni mzuri na hufaa kwenye kilimo.

Umuhimu wa mboji kwenye udongo
 Kusambaza virutubishi kama vile nitrojeni (N), fosforasi (P) na salfa (S) kwenye mimea ambayo inavihitaji.

 Kushikilia na kuhifadhi virutubishi hivyo kuzuia kuchujishwa/kuondoshwa kwa rutuba kutoba kwenye udongo.

 Husaidia kushikilia chembe za udongo pamoja hivyo kukinga dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

 Huboresha uwezo wa udongo kupitisha hewa na kuhifadhi unyevunyevu kwenye udongo.

 Huboreha uwezo wa udongo kuhifadhi maji.

 Huvipa virutubisho viumbe hai viishivyo kwenye udongo.

Rangi ya udongo na kiasi cha rutuba kilichopo
Snapshot%25284%2529.png

Namna ya kuongeza kiasi cha rutuba kwenye udongo
WhatsApp-Image-20160615.jpg

 Tumia mboji au samadi iliyochanganya na mabaki ya mazao.

 Tumia mbolea za kijani

 Badilisha mzunguko wa mazao

 Hifadhi/tunza vijidudu viishivyo kwenye udongo

 Fanya kilimo mchanganyiko na miti

 Jitahidi kuhakikisha kuwa udongo umefunikwa wakati wote

 Punguza uwezekano wa mmomonyoko wa udongo

nimeeleza kwa ufupi namna ya kupima udongo wako lakini hapo ni mwanzo tuu kwani kuna vipimo vingine vinahitaji vifaa maalumu kama kupima Ph na unyevu katika udongo wako

makala itakayo fuata itaeleza vizuri namna ya kupima Ph na unyevu(moisture content)

ni muhimu kufahamu vizuri kuhusu udongo katika shamba lako ili wataalamu waweze kufanya design na kukushauri kuhusu matumizi ya maji katika kumwagilia na pia aina ya mazao unayotakiwa kulima katika udongo husika kwani ardhi ndio inabebe chakula cha mimea

Eng(T) Octavian Justine Lasway

Bsc Irrigation and Water Resources Engineering

0763347985

octavianlaswai@gmail.com

greenagriculturetz@gmail.com

One Drop,More Production
 
Attachments

  • WhatsApp-Image-20160615.jpg
    WhatsApp-Image-20160615.jpg
    155.1 KB · Views: 235

www.greenagricultureskills.blogspot.com

One Drop,More Production
Safi sana, nimeipenda hii
 
Udongo sidhan kama tunapima aina ili mazao ya stawi. Ila virutubiasho ndani ya udongo. Acid nk
 
Ingekuwa mada ya sukari ungekomaa mpaka basi
sinywi chai mie kwahiyo sukari haijaniathiri, and by the way mtaani kwetu inauzwa 2200 na iko ya kumwaga.................

na kukufahamisha tuu hii mada niliipenda na nimeandika hilo neno ili iwe rahisi kwa mimi kuitafuta leo nikiwa hapa ofisini niisome kwa kina kwa sababu moja ya malengo yangu kwa sasa ni kilimo...

kwahiyo uache kuropoka ropoka huku mitandaoni,,
 
Ndugu yangu Mungu akubariki kwa kutoa elimu hii adimu kwa watanzania wenzako,ila nasikitika elimu hii itatumiwa na usiowatarajia....
kwa sababu ndugu zako wapo bize na kusubiri matukio ya kisiasa.
 
Nimekusoma vizuri mkuu na njia zote mbili nimezielewa vema,
Njia ya kwanza naona ni nzuri inaokoa muda sema haitoi majibu mengi kama njia ya pili.

Njia ya chupa ni nzuri japo inatumia masaa matano na dk 1 lakini unapata majibu ya matabaka matatu ya udongo.

Special thanx kwako, maana maabara za serikali ukipeleka kupima leo week ya tatu washakula 240,000 yangu na majibu sijapewa nazungushwa tu.
 
sinywi chai mie kwahiyo sukari haijaniathiri, and by the way mtaani kwetu inauzwa 2200 na iko ya kumwaga.................

na kukufahamisha tuu hii mada niliipenda na nimeandika hilo neno ili iwe rahisi kwa mimi kuitafuta leo nikiwa hapa ofisini niisome kwa kina kwa sababu moja ya malengo yangu kwa sasa ni kilimo...

kwahiyo uache kuropoka ropoka huku mitandaoni,,
Mh mbona povu hivyo mi nimekuuliza bei ya sukari mtaan kwenu? Mura mbona unajibu usiyoulizwa acha umbea mura
 
Udongo sidhan kama tunapima aina ili mazao ya stawi. Ila virutubiasho ndani ya udongo. Acid nk

sio kwel ndugu aina ya udongo ina relation kubwa sana na mazao yanayostawi katika udongo huo hapa ukiongea udongo wa kichanga,mfinyanzi na tifutifu kila zao lina aina yake ya udongo ambao likipandwa hustawi vizur mfano mdogo tuu huwezi kupanda mpunga kwenye udongo wa kichanga (hapa naongelea soil texture and structure ambazo kwa kiswahili tunazo tatu lakn ukiingia deep zaid aina za udongo yaan texture zipo zaid ya kumi na tano, sasa katika kilimo kitu cha kwanza cha kuangalia ni texture na structure ya udongo wako then ukishajiridhisha nao ndipo utatakiwa kutafuta soil mineral or chemical properties ambazo mara nyingi tunapima kiasi cha NITROGEN,POTASIUM NA PHOSPHOROUS, ukimalza hapo ndipo utapima soil cation exchange properties au wanaiita soil Ph .......... ukiwa na soil report yenye vitu vyote hivyo ndipo utapata mwongozo ya kuw ulime zao gan? au ufanye nn ili kuweka uwiano sawa na mzuri wa vitu nilivyotaja hapo juu
 
Bravo kwa ku share elimu bure na jamii mkuu. Ila kuna kitu umechanganya hapa kwenye comment i.e cation exchange properties. Watu wanaiita hiyo ni pH kimakosa. Ungewaongezea na EC (Electrical Conductivity au uwezo wa kupitisha umeme/chaji) na CEC (Cation Exchange Capacity au uwezo wa ku exchange virutubisho chanya ). Kwenye kujua rangi ya udongo mtu anaweza kuingi net ukadownload Munsell Soil colour chart ambayo ukipewa maelezo kidogo unafanya simple classification mwenyewe.
 
asante sana nazidi kuelimika
 
NAMNA YA KUTAMBUA UDONGO WAKO
mr hebu tueleze kitaalamu mmea kama nyanya kwa siku unahitaji maji kiasi gani

Kupima udongo kwa kutumia vidole

 Chukua sampuli ya udongo kwenye kiganja cha mkono kisha ondoa mizizi, changarawe kubwa kubwa na mabaki ya mimea.

 Kanda udongo kwenye kiganja chako. Kama udongo ni mkavu sana unaweza kuulainisha kwa maji kidogo

 Fikicha udongo kwa kutumia vidole na hakikisha kila kitu kimelainika (pima ugumu); Finyanga mpira (pima uwezo wa kuundwa); zungusha kutengeneza mnyoo kisha kandamiza kurudi chini (pima mnato na uwezo wa kupasuka/kupata ufa).

Udongo wa mfinyanzi:

Mwepesi na unanata sana. Ni rahisi kufinyanga mpira na haupasuki wala kupata ufa, unaweza kutengeneza. Udongo huu unaweza kuunda bonge/donge kubwa na likakauka.

Tifutifu:

Hujishika pamoja lakini hapasuka katika vijipande vidogodogo, chembe za mchanga haziwezi kushikika.

Mchanga:

Chembe za mchanga zinashikika na kuonekana. Udongo haunati na hauwezi kufinyangwa.

Namna ya kupima udongo kwa kutumia chupa ya plastiki.
Mahitaji

1. Chupa za plastiki tatu za saizi inayolingana, zenye mifuniko na zisizokuwa na rangi ili kuweza kuona vilivyomo ndani kwa urahisi.

2. Maji safi

3. Chumvi

Hatua
 Weka udongo ndani ya chupa hadi kufikia theluthi ya chupa.

 Ongeza maji mpaka kufikia theluthi mbili ya chupa.

 Weka chumvi kidogo kisha tikisa chupa kwa nguvu kwa muda wa dakika moja kisha ziache zitulie kwa saa moja.

 Baada ya lisaa limoja, tikisa chupa tena kisha ziache zitulie kwa muda wa masaa manne.

 Baada ya masaa manne udongo utakuwa umejigawa katika matabaka hivyo unaweza kuupima: Tabaka laini kabisa la juu ni mfinyanzi, linalofuatia ni mchangatope, linalofuatia ni mchanga na mwisho kabisa tabaka lenye chengachenga ni changarawe.

 Tafuta asilimia ya kila sehemu ndogo ya udongo (mfinyanzi, mchangatope, mchanga na changarawe) kwa kugawanya unene wa kila tabaka la udongo kwa jumla ya unene wa udongo wote kisha zidisha kwa mia moja (100%).

Aina za udongo
Changarawe (gravel): chembe zenye ukubwa wa zaidi ya 2 mm

Mchanga (sand): chembe zenye ukubwa wa zaidi ya 0.02 mm lakini zisizozidi 2 mm

Chembe za mchanga huchukua nafasi ndogo ukilinganisha na mchangatope au mfinyanzi. Uwezo wa kuhifadhi maji ni mdogo sana kwenye mchanga na hali ya utendaji wa kikemia ni ndogo.

Mchangatope (silt): chembe zilizo na ukubwa wa kati ya 0.02 mm na 0.002 mm

Chembe za mchangatope huchukua nafasi kubwa zaidi ya mchanga na zina uwezo mdogo kwenye hali ya utendaji wa kikemia. Mchangatope huathirika kwa urahisi na migandamizo ya vitu vizito hivyo kuathiri uwezo uingizaji wa hewa na mzunguko wa maji kwenye udongo.

Udongo wa mfinyanzi (clay): chembe zisizozidi 0.002 mm

Chembe za udongo wa mfinyanzi huchukuwa nafasi kubwa sana na zina hali kubwa sana ya utendaji wa kikemia. Virutubishi pamoja na maji hujishikisha kwenye huu udongo lakini havipatikani mara zote kwa mimea. Udongo wa mfinyanzi unauwezo wa kutuna na hufaa kuundia vitu mbalimbali kwa sababu ya asili yake ya kunata.

Mchanganyiko wa mchanga, mchangatope na udongo wa mfinyanzi huleta udongo tifutifu (loam) wenye rutuba. Udongo huu ni mzuri na hufaa kwenye kilimo.

Umuhimu wa mboji kwenye udongo
 Kusambaza virutubishi kama vile nitrojeni (N), fosforasi (P) na salfa (S) kwenye mimea ambayo inavihitaji.

 Kushikilia na kuhifadhi virutubishi hivyo kuzuia kuchujishwa/kuondoshwa kwa rutuba kutoba kwenye udongo.

 Husaidia kushikilia chembe za udongo pamoja hivyo kukinga dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

 Huboresha uwezo wa udongo kupitisha hewa na kuhifadhi unyevunyevu kwenye udongo.

 Huboreha uwezo wa udongo kuhifadhi maji.

 Huvipa virutubisho viumbe hai viishivyo kwenye udongo.

Rangi ya udongo na kiasi cha rutuba kilichopo

Namna ya kuongeza kiasi cha rutuba kwenye udongo

 Tumia mboji au samadi iliyochanganya na mabaki ya mazao.

 Tumia mbolea za kijani

 Badilisha mzunguko wa mazao

 Hifadhi/tunza vijidudu viishivyo kwenye udongo

 Fanya kilimo mchanganyiko na miti

 Jitahidi kuhakikisha kuwa udongo umefunikwa wakati wote

 Punguza uwezekano wa mmomonyoko wa udongo

nimeeleza kwa ufupi namna ya kupima udongo wako lakini hapo ni mwanzo tuu kwani kuna vipimo vingine vinahitaji vifaa maalumu kama kupima Ph na unyevu katika udongo wako

makala itakayo fuata itaeleza vizuri namna ya kupima Ph na unyevu(moisture content)

ni muhimu kufahamu vizuri kuhusu udongo katika shamba lako ili wataalamu waweze kufanya design na kukushauri kuhusu matumizi ya maji katika kumwagilia na pia aina ya mazao unayotakiwa kulima katika udongo husika kwani ardhi ndio inabebe chakula cha mimea

Eng(T) Octavian Justine Lasway

Bsc Irrigation and Water Resources Engineering

0763347985

octavianlaswai@gmail.com

greenagriculturetz@gmail.com
www.greenagricultureskills.blogspot.com

One Drop,More Production
 
Hizo ni very partial methods, udongo ni lazima upelekwe maabara ndio utapata matokeo sahihi na kuweza kufanya management practices ktk Shamba lako
 
lab bei ghali sana so kwa wakulima wetu bora wakaanza na hizo kwanza itawasaidia
 
Hizo ni very partial methods, udongo ni lazima upelekwe maabara ndio utapata matokeo sahihi na kuweza kufanya management practices ktk Shamba lako
4fd427b8cfcc780ba567ae1fb45cdd2a.jpg

Maabara ipo ya kisasa kabsaa karibu
0763347985 Eng Octavian Lasway
 
Back
Top Bottom