Pilipili ni dawa?

Lady.A

JF-Expert Member
Dec 13, 2013
392
191
habari zenu.
najua wengi mtakubaliana na mimi kwamba kiungo pilipili ni mojawapo ya vitu viletavyo hamu ya kula. lakini kuna wengine wanasema pilipili sio nzuri kwa afya, na wengine usema ni dawa, hata mimi naunga mkono kwamba ni dawa, kwani hutibu kwa wale wa Kigoma, wale funza wasiotibika, basi dawa yao ni pilipili. sasa je wewe unasemaje? pilipili ni dawa ama la?
 
na kwa wale wanaosema ni hatari kwa afyaje?

Kama una vidonda vya tumbo ndiyo huwa ni hatari tofauti na hapo pilipili ni dawa, inaongeza mzunguko wa damu, huongeza hamu ya kula, huondoa sumu mwilini na vile vile huongeza nguvu za kiume (waulize wahindi watakuambia).
 
aisee, asante sana mkuu maana nilikuwa nakula kwa hofu, ila nikiona wahindi wanavyozibugia nilikuwa nashindwa kuelewa. napenda sana pilipili.
 
Ahahahaaaa...mwaka huu tutalishwa hadi vinyesi kisa nguvu zetu wanaume....

Na kunguru weusi wa zanzibar supu yao inaongeza nguvu za kiume balaaa...waulize wahindi watakuambia kule kwao wanavyoitumia...ni noumerrr.
 
Na kama inasadikika kufanya yote hayo kwa nn wanamicjezo hawashauriw au wao ndo hawataki hzo faida za pilpil>>>>>!
 
habari zenu.
najua wengi mtakubaliana na mimi kwamba kiungo pilipili ni mojawapo ya vitu viletavyo hamu ya kula. lakini kuna wengine wanasema pilipili sio nzuri kwa afya, na wengine usema ni dawa, hata mimi naunga mkono kwamba ni dawa, kwani hutibu kwa wale wa Kigoma, wale funza wasiotibika, basi dawa yao ni pilipili. sasa je wewe unasemaje? pilipili ni dawa ama la?

PILIPILI HUIMARISHA UJASIRI NA NGUVU MWILINI!

attachment.php

Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na

faida kiafya mwilini, pilipili nayo ni moja wapo. Licha ya kuogopwa na baadhi ya watu, lakini ina kiasi kingi cha vitamin C.

attachment.php

Umuhimu wa Vitamin C mwilini, humfanya mlaji awe imara na ndiyo maana wala pilipili siyo waoga, ni watu wenye

kujiamini, hawaugui hovyo na huimarisha nguvu za mwili kwa ujumla.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, pilipili ina asili ya Marekani. Wafanyabiashara wa Ulaya waliipeleka barani Asia

ambako nako Waarabu katika pilikapilika za biashara ya utumwa wakajikuta wameileta Afrika Mashariki, ikiwemo

Tanzania.

Aidha, pilipili inadaiwa kudhibiti uzito, ingawa haijathibitishwa rasmi kama inaweza kupunguza uzito wa mwili. Hata

hivyo, pilipili ina faida lukuki za kiafya ambapo inajulikana kwa uwezo wake wa kudhibiti maumivu ya viungo na

ugonjwa wa kisukari.

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani na Chama cha Watafiti wa Ugonjwa wa Saratani, umegundua kuwa upo

uwezekano wa pilipili kuua na kutokomeza viini vya saratani ya uzazi na mapafu, endapo italiwa chini ya usimamizi na

maelekezo ya daktari.

Ili kupata faida za pilipili kama zilivyoainishwa hapo juu, hakikisha mlo wako unakuwa na pilipili kwa kiwango

utakachoweza kukimudu, na inapendekezwa pilipili iwe mbichi, na kama utaipika pamoja na kitoweo au mboga,

hakikisha unatumia pilipili halisi na siyo ya kwenye makopo.

Hata hivyo, unaweza usiipate pilipili halisi kutokana na mazingira au usile kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo

ya kiafya. Upo msaada wa tibalishe za ‘Go!’ ambazo zinaweza kufanya kazi mbadala wa pilipili. Zipo Go! za aina nne

yaani, Man, Woman, Focus na Workout ambazo zipo madukani karibu nchi nzima.

Go! Man itakuongezea kinga ya kupambana na maradhi kwa mwaka mzima huku ikiboresha uhai wa moyo. Itafukuza

maumivu ya mgongo, kiuno na miguu pia. Itakusafisha ubongo na kurejesha kumbukumbu na kuimarisha afya kwa

ujumla.

‘Go! Woman’ itampa mwanamke vitu vyote hivyo ila imeongezwa vikorombwezo vitakavyomfanya mwanamke

mrembo kwa kukarabati kucha zake, ngozi na nywele pia. Tibalishe ni msaada mkubwa wa kurekebisha afya zetu kwa

sababu katika hali ya kawaida hatuwezi kukidhi mahitaji ya miili yetu kwa chakula pekee.

Tibalishe nyingi zipo madukani, iwapo utashindwa kuzipata tafadhali tuwasiliane tukusaidie kuzipata. Ila, kumbuka kula

pilipili daima uwe THABITI.

Attachments

  • pilipili2.jpg
    pilipili2.jpg
    55.9 KB · Views: 831
  • pilipili.jpg
    pilipili.jpg
    48.7 KB · Views: 1,439
Ogopa plpl zinazoota kuelekea juu (ile sehemu ambapo ua hukatikia kuelekea upande wa jua) mfano ni zile plpl kichaa. Naishi na muhindi anasema wao wanakula plpl kwa afya na wanatumia plpl zinazoangalia chini!
 
Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na

faida kiafya mwilini, pilipili nayo ni moja wapo. Licha ya kuogopwa na baadhi ya watu, lakini ina kiasi kingi cha vitamin C.
Umuhimu wa Vitamin C mwilini, humfanya mlaji awe imara na ndiyo maana wala pilipili siyo waoga, ni watu wenye

kujiamini, hawaugui hovyo na huimarisha nguvu za mwili kwa ujumla.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, pilipili
asante sana dr, na vipi kwa wanaosema kuwa m.ke akila sana pilpil anaweza kupata shida ya maumivu makali wakati wa hedhi, pia muwasho sehemu za siri, ni kweli?
 
Ogopa plpl zinazoota kuelekea juu (ile sehemu ambapo ua hukatikia kuelekea upande wa jua) mfano ni zile plpl kichaa. Naishi na muhindi anasema wao wanakula plpl kwa afya na wanatumia plpl zinazoangalia chini!

embu muulize vizuri huyo mhindi basi, hizo zinazoangalia juu zinafanyaje?
 
embu muulize vizuri huyo mhindi basi, hizo zinazoangalia juu zinafanyaje?

Zinaitwa 'hot chill' na zinazoangalia chini ni 'cold chill'. Cold chill ni nzuri na zimependekezwa kuliwa kiafya lkn hot not recommended hata wao wanaozingatia afya hawazitumii sana ukilinganisha na cold chill
 
embu muulize vizuri huyo mhindi basi, hizo zinazoangalia juu zinafanyaje?

Huyu jamaa ananifunza kupika beef ni noma, yani nusu kilo ya steki viungo km 10 hivi plpl inclusive. Kitunguu kama ngumi yani kizima kinaunga nusu kilo!
 
Back
Top Bottom