Pigo kuu CHADEMA ni la kupuuzwa na wananchi sababu ya ndimi mbili na kutoomba radhi kwa ulaghai

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Wenye kumbukukumbu sawa mtakumbuka siku Lowassa anachukua fomu kugombea urais kwa tiketi ya Chadema kwa kuzidiwa na furaha ndugu Freeman Mbowe alizimia/ alipoteza fahamu na kulazwa hospitali ya Muhimbili, alipozinduka alikiri kuwa Lowassa ni ''mwanamabadiliko'' wa kweli. Siku za karibuni baada ya Edward Lowassa kuondoka CHADEMA anasema alikuwa mzigo.

Tundu Lissu, ghafla aliongoza wafuasi wa CHADEMA kutoa matusi kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema na mwalimu wake wa siasa Dr.Wilbroad Slaa. Zaidi, akajimilikisha ''utunzi wa orodha ya mafisadi'' akaenda mbali zaidi akasema kwa mujibu ujuzi wake kisheria kajiridhisha pasi na shaka kuwa EL alisingiziwa,alitegwa na hivyo akatangaza msamaha.

Ili kutilia mkazo hoja yake akasema kwa mujibu wa ripoti za utafiti wa ''wazungu'' EL ndiye anapendwa zaidi, hivyo wao hawaangalii tena maadili,uchapa kazi n.k wanazingatia taarifa za wazungu.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na vijembe na kejeli nyingi kwa wanaoondokka CHADEMA pasipo na kukiri makosa na kutubu kwa wananchi.

Wananchi si wajinga, wengi ukiwauliza sasa hivi wanakwambia ''hao wote ni CCM tu, ulaghai umezidi.

Kama mtapuuza kutoa tamko rasmi la kuomba msamaha wananchi kwa ulaghai mliofanya mwaka 2015 anguko liko palepale. Niwakumbushe tu, hata Mrema alikuwa na wafuasi wengi sana kiasi cha kusukuma gari lake lakini leo hana ushawishi.
 
Hizo ndizo siasa za Bongo. Lowasa allitwa fisadi na CDM Lakini akaenda huko. Kwanini?
CCM ikamsakama na hata kumwita mfu mtarajiwa, kajinyea nk. Mwishowe wamempokea. CCM wanaita CHADEMA manyumbu lakini inawakaribisha na kuwapa vyeo. Kwa nini?

Ukiwa na akili ya kupima mambo unatazama tu kama komedi ktk tv. Mambo ni sitaki nataka au sizitaki mbichi hizi huku unazirukia upate kula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ndizo siasa za Bongo.
Lowasa allitwa fisadi na CDM Lakini akaenda huko. Kwanini?
Ccm ikamsakama na hata kumwita mfu mtarajiwa, kajinyea nk. Mwishowe wamempokea.
Ccm wanaita CDM manyumbu lakini inawakaribisha na kuwapa vyeo. Kwa nini?
Ukiwa na akili ya kupima mambo unatazama tu kama komedi ktk tv.
Mambo ni sitaki nataka au sizitaki mbichi hizi huku unazirukia upate kula

Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa za maji taka hizo.
 
Wakudadavuwa,

Kwa taarifa yako Magufuli ameharibu demokrasia na kuishia kulazimisha yeye na ccm wakubalike, lakini hilo halijatokea, na sasa hivi pita kwenye vituo vya kujiandikisha kupiga kura hamna watu, mmebaki kusema ccm inakubalika huku wananchi hawawapigii kura!

Wewe hapo ulipo umebaki kuleta mabandiko yasiyo na tija yoyote dhidi ya cdm badala ya kuangalia ccm mnakwamwa wapi mpaka watu wapuuza uchaguzi.
 
Mlaghai number moja duniani ni CCM:

1. Ni chama cha ujamaa huku wanachama woote mabepari.
2. Wanatuita nyumbu eti hatuna akili wakitununua wanatuita professor
3. Wananunua watu huku wanadai wanapambana na rushwa.
4. Hawana akili na hawajitambui maana wanashangilia mauaji, utekaji in the umbrella of uzalendo wakati wanajua wao si wazalendo Bali ni "wazarendo"
 
Kwa mtazamo wangu ni kwamba Chadema ni chuo cha kutengeneza raslimali watu. Ona CCM inavyohaha kuwatamani watu toka Chadema. Yaani mtu akitoka Chadema leo anaonekana ameiva vizuri kuwa kiongozi ndani ya CCM na ndani ya serikali kiasi cha kutokuwa na mpinzani ndani ya CCM.

Hongera sana Chadema. Nawaasa vijana na watu wote wanaotaka kuwa lulu katika nchi hii basi wajiunge haraka na Chadema ili ukpikwe na uwatoe udenda CCM na serikali kutamani kukuhitaji kwa gharama yoyote!
 
Wakudadavuwa,
Ukiwa na akili ndogo za kuvukia barabara utadhani unachokiwaza ni sahihi lakini kama ungekuwa na akili timamu wala hutothubutu kusema chadema imepuuzwa na wananchi, iliyopuuzwa na wananchi ni ccm inayolazimisha wananchi kwa kutumia vyombo vya dola. Be serious kijana mwenzangu
 
Wakudadavuwa,
Ukiwa na akili ndogo za kuvukia barabara utadhani unachokiwaza ni sahihi lakini kama ungekuwa na akili timamu wala hutothubutu kusema chadema imepuuzwa na wananchi, iliyopuuzwa na wananchi ni ccm inayolazimisha wananchi kwa kutumia vyombo vya dola. Be serious kijana mwenzangu
Kejeli haziwezi kupunguza adhabu ya karma
 
Nyie Lumumba nawashauri kama mkitaka walau CDM iyumbe yumbe kidogo hebu mnunueni Mh. Mbowe...hawa wengine mtamaliza hela zetu za kodi bure na chama kinasonga mbele kila kukicha.
Huko CCM kunatokota wahamiaji wanalamba teuzi wanaCCM wanapiga miayo wasijue ni nini kinaendelea hahahaaa!!!
 
Back
Top Bottom